Makapuku Forum

Pamoja sana bitoz
 
1986 - Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico: Mechi ya robo fainali baina ya Uingereza dhidi ya Argentina inafanyika.

Diego Maradona, nahodha wa Argentina anafunga magoli mawili murua na kuitoa England kwa jumla ya magoli 2-1.

Goli la kwanza, Maradona alilifinga kwa mkono na goli hilo linajulikana kama Goli la Mkono wa Mungu.

Goli la pili, Maradona alipiga chenga wachezaji watano wa England kabla ya kufunga. Goli hili linajulikana kama Goli la Karne.

Hiyo ni moja kati ya mechi za kukumbukwa za wakati wote katika historia ya mchezo wa soka.
 
1903 - John Dillinger anazaliwa.

Alikuwa ni Jambazi sugu aliyesumbua nchini Marekani katika miaka ya 1930's kipindi cha Mdororo wa Uchumi.

Alikuwa na genge lake kubwa la kihalifu lililokuwa linavunja benki na kuiba.

Alikuja kuuliwa na FBI mara baada ya kutafutwa sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…