Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170622-WA0013.jpg
 
Katika dondoo za bbc. ...

Majeshi ya Iraq na Marekani yamesema wapiganaji wa Islamic State wameulipua msikiti mkubwa wa al- Nuri uliopo mjini Mosul na pamoja na mnara wake mkongwe uliodumu karne na karne.

Viongozi wandamizi wa mataifa makuu matano yanayojumuika katika ushirika wa bonde la mto Nile wanakutana nchini Uganda kujaribu kutanzua tofauti zilizosababishwa na mapatano ya Entebbe kuhusu matumizi ya maji yamto huo.

Wakimbizi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo walioko katika kambi za wakimbizi nchini Rwanda wanalalamikia kupungua kwa idadi ya wanaohamishwa kutoka kambini na kwenda kuishi nchini Marekani.

Mahakama ya kikatiba nchini A-Kusini ambayo ndio yenye uamuzi wa juu kabisa leo itaamua iwapo kura ya siri inaweza kutumika bungeni kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani .

Nchini Tanzania ,Dr.Askwari Hilonga mtaalamu wa masuala ya Uhandisi wa kemikali ameamua kutumia taaluma yake kutatua matatizo yanayosababishwa na maji kutokuwa safi na salama katika jamii inayomzunguka.

Uchafuzi wa mazingira ya ziwa Tanganyika kwa upande wa Burundi umekua ukitia wasiwasi mashirika ya kimataifa na hata ya raia wa nchi hiyo ya kulinda mazingira kwa ujumla.
Hongera Dr.Askwari Mungu akutangulie katika kazi yako.

Uchafuzi wa Ziwa Tanganyika unazuilika hatua zichukuliwe.

Mungu asaidie kuepusha vita ,maafa,na kuwa na mzingira mazuri kuishi,Majeshi ya islamic state hayatakuwa na nafasi na pia ukimbizi utapungua

ZUMA mashakani

Ubarikiwe mkuu Lee kwa UF,BBC na Baraka uwe na siku njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom