Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nipo anko, jana si unakumbuka nilikuambia nahama kama tulivyoongea, maana huu mtaa wahamiaji haramu wanataka kuleta zengwe kusikia kuna Noah inakuja toka acasicia.

Vipi lakini
Mimi nilishtuka mapema nkajikataa kwa wale japo wewe uliona umefikaa kumbe umefikwa ...mm nilichofurahia ni kuona dalili za kupewa za mafuta make sethi na rugemalila wake hawachomokiii....

Niko poa lakin
 
Kama ndo yule jamaa mpya afadhali tu ushemeji ufe. Nilifikiri kuwa baada ya brother Shedede ungekuwa angalau na kipindi cha ku-cool off kidogo na kuangalia upepo unakwendaje. Kumbe unaunganisha tu ka treni lisilo na breki from one relationship to another. Goodluck mama japo nahisi kama safari hii umelamba gharasha
Love cant be destroyed ...just transmitted from one to another
 
Muziki: Kuhama Mtaa

Ninyi ni watu wema sana, huwa nakuwa na wakati mzuri sana nikiwa hapa na hili si uongo wala makidai, Ndo ukweli na ukweli siku zote hata ukifukiwa futi sita chini utaibuka tu, huwa ni suala la muda tu na wala si kitu kingine. Hongera kwetu tunaojitahidi angalau kusema kweli japo mara chache kuliko nyingi za uongo. Sisi ni binadamu.

Nimefurahia segment ya Makapuku TV, hii itakuwa ni bomb, hoping itapangwa muda mzuri ili zisiingiliane na nyingine.

Jana nilipotea, yeah, ni vizuri nikashare nanyi maana tangu mwenye nyumba aanze kunisalimia kila siku (salamu maana yake anakumbushia nilipe kodi ya nyumba, ni haki yake lakini si kwa salamu zinazozidi kipimo). Nimeamua kuhama, naamu nahama maana kwanza nimesikia tetesi anaongeza kodi ya nyumba. Ni nyumba yake afanye analotaka na kodi ni yangu naamua navyotaka.

Mnakumbuka mwezi jana ulikuwa wa neema kwangu, kwanza nilinunua saa mpya, solar automatic. Then, baadaye yaani after that nikapewa simu ya tachi na funga kazi sasa nimeingiza flat scrini ndani na hapo sasa ndo maneno yalipoanza na vituko. Dirisha la chumbani limechwana mtindo wa sambusa, walitaka kupora simu wakaondoka na chaja, kama kuna member yeyote anakodisha chaja aweke tangazo, au vipi aniazime bila kuweka sharti la kurudishiwa. Mkopaji jeuri.

Nisikuchoshe bhana maana najikuta naongea sana. Kuna mtu aliniambia naongea sana kwa sababu nilichelewa kutembea, sio kosa lake maana ndo aliyenizaa.

Muziki na kuhama leo, nimekupigisha sound mvua hapo juu lakini lengo langu nataka tu umsikize Shaggy, yeah Mr Lavalava. Enzi hizo miziki ya kutengenezwa studio ndo inawika sanaa na japo huu wimbo ni wa studio lakini nimewahi kuwaona jamaa hapa mjini wanaucheza live gitaa nyingi na vinanda, utapenda.

Hadi hapo wakati mwingine Makapuku ni sehemu nzuri kwa sababu tu wewe u sehemu yake



Tahadhari: Muziki huu raha yake uwe na simu zile za kichina zenye spika nane na subufa, wenye Samsung, LG, Iphone na nyingine za makabila ya original inabidi muwe wataulivu sisi wenye Samsing, Itel6, Yutong4 tufaudu

Asante bhinamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom