Makapuku Forum

je wajua..??
Kuwa baba sio tu kuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito na kuzaa mtoto. Kuwa baba sio suala la kibaiolojia tu. Kuwa baba sio wadhifa. Kuwa baba ni jukumu na utayari wa kubeba majukumu. Kuwa baba ni nafasi ambayo sifa na pongezi huja baada ya matokeo, kuwa baba nikuwa na uwezo wa kujitoa mhanga kuhakikisha familia yako inatabasamu hata kama gharama ya tabasamu lao inatokana na wewe kununa au kuteseka. Kuwa baba ni uwezo wa kuhakikisha furaha ya watu wa familia yako inaitangulia furaha yako na sio kuitanguliza furaha yako mbele na kuisahau ya wanaokuita baba. Being a father is a serious business that deserve serious people.
 
Ahsante mama mchungaji



Ubarikiwe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…