Makapuku Forum

Makapuku Forum

UF...

338d19c7dfb5fcf6d6b50c7e2dacd5dd.jpg
Aisee
 
[emoji524] ZABURI 133

1 Tazama ulivyo vema na kupendeza Ndugu wakae pamoja kwa umoja

2 Ni kama mafuta mazuri kichwani Yashukayo ndevuni ndevu za Haruni Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake

3 Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni maana ndiko BWANA aliko amuru Baraka Naam uzima hata milele

[emoji523] Kupitia wimbo huu wa mfalme Daudi, tunakumbushwa kuwa na UMOJA katika maisha ya kila siku katika familia jamii na taifa MUNGU anapendezwa na UMOJA kama alivyodhihirisha katika UTATU wake wa BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU

[emoji120] MUNGU BABA asante kutuamsha tena asante kwa NENO "UMOJA"wewe uliye asili ya mema yote utupe huo UMOJA na UPENDO maishani mwetu utuimarishe kila mmoja kwa mwenzake katika familia na jirani zetu na hata taifa letu kipekee ulibariki kundi hili la MAKAPUKU lidumu katika kujifunza bariki kazi za mikono yetu biashara na wanaotutazama wauone Ukuu wako wapate kukutukuza katika jina la Yesu Kristo Amen Asante[emoji120]

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA IBADA NJEMA MBARIKIWE[emoji7] [emoji7]
Ahsante sana mama mchungaji
 
Back
Top Bottom