Makapuku Forum

 
WAFILIPI 4

1 Basi ndugu zangu, wapendwa wangu, ninawaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika BWANA, wapenzi wangu.

4 Furahini katika BWANA siku zote tena nasema furahini

5 Upole wenu na ujulikane na watu wote BWANA yu karibu

6 Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na MUNGU

7 Na amani ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu

MUWE NA JIONI NJEMA MBARIKIWE
 
Ndoo maana mm kiroho safi napachika picha tu


Ha ha ha ahaha, hata hiyo kupachika picha tu ingekuwa rahisi kila mmoja wetu angeweza. Si lazima uisome picha na uone kamainaweza kuwa na maana hapa jukwaani.

Unafanya kazi sana anko na tunaipenda, sio rahisi na ingekuwa ni hivyo hata mimi ningeweza, sema nilichonacho ni saa na simu ya tachi tu, sio simu ya kamera
 

Asante BH, kufurahia ni haja ya kila mmoja ila la kujiuliza unafurahia nini? Ukifurahi katika Bwana basi hiyo ni heri sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…