Nakuunga mkono, kuandaa makala hata ya aya moja tu (a sounding/meaningful para) sio kazi rahisi.
Ninapoweka Muziki na Gitaa zile blah blah ninazoandika-ga kabla huwa naandaa masaa si chini ya matatu na hapo ninakuwa-ga na maandalizi ya wiki nzima niandike nini. Kumbuka huwa naandika J3-Ijumaa
Lengo ni kuifanya Makapuku iwe ni sehemu ambayo baada ya kusogoa kidogo basi kunakuwa na vitu vizuri vya afya ya ubongo.
Tukikutana kunywa supu ya utumbo basi sio mara zote mazunguzo yote yawe utumbo na hata yakiwa utumbo ndo maana utumbo tunakula na ndizi.
Makapuku hutembelewa na wengi wenye malengo tofauti na wanakuja huku tu kwa sababu kuna vitu wanavikosa sehemu nyingine, burudani, elimu, ustadi, mahusiano, siasa, sogozi na taja chochote utakipata hapa na bila kuwasahau wahamiaji haramu, makinikia na smelters