Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Sifa ya Nguru sio Chumvi

Inakaribia kabisa Ijumaa, TG. Na kwa hali hii basi naamini kabisa wote tunaokutana hapa tumekuwa na wakati mzuri sana leo, Makapuku ni kama kokoro, ukute wengine walipo ni Ijumaa tayari na kwa walio Kigoma saa hizi jua linawaka sana. Shukurani kwa kutembelea hapa muda huu.

Well, kipengele chetu kama ilivyo ada, oh yeah, ada ni mtihani kweli kweli, kwa wote waliosoma sekondari na wakabahatika kula ada au japo kuidokoa kidgo mnajua kabisa ugumu wa kuirudisha bila kurudishwa nyumbani 😀😀😀, ha hahaha, hata mimi ninayeandika hapa nimepata kicheko cha aina yake maana ada ni ada tu, ndo maana mzazi alipokuwa ananipa ada lazima nihesabu mbele yake. Sio kwamba simuamini, ila ada haina adabu, na kuihesabu lazima nihakikishe kila noti kwa mate, yaani kama mfanyakazi wa bank vile. Hongera sana wote mliowahi kula au kudokoa ada, nyinyi ni wapambanaji halisi.

Turudi kwenye muziki, na kama kawaida hapa ni gitaa kwa kwenda mbele. Gitaa bila kujali ni la solo, lead au rhythm dhumuni kubwa ni kuleta ladha kwenye muziki. likipigwa sawasawa hutoacha kutikisa kichwa na ukishakuwa na akili za balehebalehe basi hukatazwi kutikisa kiuno. Muziki ni burudani.

Ndala Kasheba, yes, namuongelea mkongoman huyu aliyekuja Bongo mapema tu baada ya uhuru wa nchi yetu na akafanya muziki kwa mafanikio makubwa kabisa hapa nchini. Alijulikana ndani na nje ya nchi kwa aina yake ya kipekee ya kupiga gitaa akizidonoa zaidi zile nyuzi tatu za kwanza.

Unaikumbuka Dezo Dezo, Kesi ya kanga, Marashi ya Pemba na ukipata muda Kapuku mwenzangu hebu sikiza Yellow Kadi (hii ni ballad ) ina mashairi ambayo kiukweli utayapenda sana na kwa hadhari tu sikiliza huku unapata kahawa moto, chai au kama wewe ni mlipakodi halisi sikiza huku unakunywa bia.

Sikiza hizi zote na utausikia utamu wa gitaa lake la nyuzi 12

Ni bahati mbaya sana Ndala katutoka na zaidi kama walivyokuwa wanamuziki wengine hapa nchini hakufaidika sana na matunda ya muziki wake kutokana na wengi wetu kutosapoti muziki wa dansi enzi kabla ya miaka ya 2000 na hata vijana wa sasa full kudownload (pirating ). alianzisha band naamini ikiitwa Zaita ambayo haikufanya vema sana na udhoofu wa mwili ulimlaza nje ya game kwa muda hadi mauti yalipomkuta.


Nikupe nafasi sasa ya kusikiza kibao kimoja wapo na naamini utakipenda maana mida hii Makapuku forum ni burudani na utani wa kutoyafanya maisha kuwa magumu sana kama kula ada ilhali ikijulikana kabisa sifa ya nguru sio chumvi, maana chumvi nguru anapakazwa tu, uvundo ndo sifa yake kuu.




kash.jpg

Bhinamu asante umenikumbusha enzi za mzee akiwa kijana ...

Sema binamu uliponiacha ata sehemu yetu pendwa kuna goma limepigwa naomba utuwekee si unajua kapuku twapendana ...jina dj hajatambulishaa ila unaimba hivi..

Pacha wangu ....(.gitaa linakunwaaa)...umeamua ..kuniacha peke yang mama kwa ajili ya pesa. (..giitaa linakunwaaa)
 
Bhinamu asante umenikumbusha enzi za mzee akiwa kijana ...

Sema binamu uliponiacha ata sehemu yetu pendwa kuna goma limepigwa naomba utuwekee si unajua kapuku twapendana ...jina dj hajatambulishaa ila unaimba hivi..

Pacha wangu ....(.gitaa linakunwaaa)...umeamua ..kuniacha peke yang mama kwa ajili ya pesa. (..giitaa linakunwaaa)


nalijua hilo goma anko ha hahhahahaha.

Hivi kumbe uliendelea kubaki pale pale, nilimuona na yule teller ukiwa kwenye mkao wa kupokea ripoti ya tatu ya makanikia😀
 
nalijua hilo goma anko ha hahhahahaha.

Hivi kumbe uliendelea kubaki pale pale, nilimuona na yule teller ukiwa kwenye mkao wa kupokea ripoti ya tatu ya makanikia😀
Ha ha ha nilikuona unazunguka kama pia kule jikoni ila wewe kiboko yule mhudumu nasikia kaja jana unataka usajili wa namba E kabisaa. ..ila kumbuka hii vita sikuteteii make yule mhudum nayemtaniaga profesa wako kwa kuvaa miwan kidogo ashtukie ila nikampozaa

Mm bado nipo na usajili wangu mpya DXY ...CM namba nimedaiivet kwakoo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom