Makapuku Forum

Makapuku Forum

Fatakiiiii !!!
3f3f338ade53e03eb32bb2a96b5d65cc.jpg
Huku anungua
 
ISAYA 54

10.Maana milima itaondoka,na vilima vitaondolewa;Bali wema wangu hautaondoka kwako,wala agano langu la amani halitaondolewa ;asema BWANA akurehemuye

MUNGU AWABARIKI USIKU WA LEO ,DAMU YA YESU IWAFUNIKE ,MALAIKA WALINZI WAZUNGUKE NYUMBA NA VITANDA VYETU WOTE MBARIKIWE
 
Inaweza kuwa ndiyo au siyo kutegemea na umemaanisha nini. Niko kwenye fani kama mpenzi msikilizaji tu au mtazamaji na mahudhurio yangu kwa kweli si haba.

Sijui kupiga gitaa ukafurahia ila napenda kusikia likipigwa ndilo linanivutia.

Naimani nawe kama haupo kwenye fani basi kuna kitu kinakuunganisha na muziki wa mataifa au kaswida au gospel
sawa mukulu,
basi nilijua utakuwa unalikung'uta solo guitar au bass
 
Muziki: Sifa ya Nguru sio Chumvi

Inakaribia kabisa Ijumaa, TG. Na kwa hali hii basi naamini kabisa wote tunaokutana hapa tumekuwa na wakati mzuri sana leo, Makapuku ni kama kokoro, ukute wengine walipo ni Ijumaa tayari na kwa walio Kigoma saa hizi jua linawaka sana. Shukurani kwa kutembelea hapa muda huu.

Well, kipengele chetu kama ilivyo ada, oh yeah, ada ni mtihani kweli kweli, kwa wote waliosoma sekondari na wakabahatika kula ada au japo kuidokoa kidgo mnajua kabisa ugumu wa kuirudisha bila kurudishwa nyumbani 😀😀😀, ha hahaha, hata mimi ninayeandika hapa nimepata kicheko cha aina yake maana ada ni ada tu, ndo maana mzazi alipokuwa ananipa ada lazima nihesabu mbele yake. Sio kwamba simuamini, ila ada haina adabu, na kuihesabu lazima nihakikishe kila noti kwa mate, yaani kama mfanyakazi wa bank vile. Hongera sana wote mliowahi kula au kudokoa ada, nyinyi ni wapambanaji halisi.

Turudi kwenye muziki, na kama kawaida hapa ni gitaa kwa kwenda mbele. Gitaa bila kujali ni la solo, lead au rhythm dhumuni kubwa ni kuleta ladha kwenye muziki. likipigwa sawasawa hutoacha kutikisa kichwa na ukishakuwa na akili za balehebalehe basi hukatazwi kutikisa kiuno. Muziki ni burudani.

Ndala Kasheba, yes, namuongelea mkongoman huyu aliyekuja Bongo mapema tu baada ya uhuru wa nchi yetu na akafanya muziki kwa mafanikio makubwa kabisa hapa nchini. Alijulikana ndani na nje ya nchi kwa aina yake ya kipekee ya kupiga gitaa akizidonoa zaidi zile nyuzi tatu za kwanza.

Unaikumbuka Dezo Dezo, Kesi ya kanga, Marashi ya Pemba na ukipata muda Kapuku mwenzangu hebu sikiza Yellow Kadi (hii ni ballad ) ina mashairi ambayo kiukweli utayapenda sana na kwa hadhari tu sikiliza huku unapata kahawa moto, chai au kama wewe ni mlipakodi halisi sikiza huku unakunywa bia.

Sikiza hizi zote na utausikia utamu wa gitaa lake la nyuzi 12

Ni bahati mbaya sana Ndala katutoka na zaidi kama walivyokuwa wanamuziki wengine hapa nchini hakufaidika sana na matunda ya muziki wake kutokana na wengi wetu kutosapoti muziki wa dansi enzi kabla ya miaka ya 2000 na hata vijana wa sasa full kudownload (pirating ). alianzisha band naamini ikiitwa Zaita ambayo haikufanya vema sana na udhoofu wa mwili ulimlaza nje ya game kwa muda hadi mauti yalipomkuta.


Nikupe nafasi sasa ya kusikiza kibao kimoja wapo na naamini utakipenda maana mida hii Makapuku forum ni burudani na utani wa kutoyafanya maisha kuwa magumu sana kama kula ada ilhali ikijulikana kabisa sifa ya nguru sio chumvi, maana chumvi nguru anapakazwa tu, uvundo ndo sifa yake kuu.




kash.jpg

Asante sana Obe ubarikiwe uaiku mwema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom