Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170615-WA0005.jpg
 
Muziki na Kutokelezea


Piga pamba unavyoweza, tokelezea unavyoweza, jipambe upambike na usishau kutumia muda wako kwenye kioo ili kutambua kuwa kila mmoja wetu ni kichaa kwa aina yake.

Sijui kama ninarudia hiki ninachoandika, lakini hata kama ninarudia hakuna ubaya maana maana inaweza kubadilika kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwemo siku. Ukiwa katika siku zako basi unaweza kuona rangi zote na kama hauko kwenye siku zako basi usishangae ukijikwaa na kulaumu ulipoangukia.

Salama lakini humu ndani? Nilitingwa kidogo, si unajua tena mambo ya kuitafuta siku uimalize mapema, sasa leo nilikuwa kwenye siku yangu, niliiona yaani tight ile mbaya lakini nimeimaliza na sasa nausubiri mwezi, nipokee mshahara. Kadri unavyoimaliza siku yako ndivyo mshahara unakaribia, haijalishi unalipa au unalipwa.

Turudi kwenye muziki, jana nilikwambia kuwa wanamuziki waanzilishi wa Les Wanyika kina Ngereza na Kinyonga walikimbilia Kenya kutokana na ugumu wa uchumi katika tasnia ya muziki, well, hizi mambo ukiona kwako kugumu mwingine anatamani aje. Wakongo kibao walimiminika Bongo miaka ya 70, 80 na 90 na kuendelea hadi kesho.

Mmoja wao alikuwa ni mpiga gitaa mzuri tu ambaye ukisikiza anavyopiga gitaa na kuimba utampenda sana, sauti na gitaa lake, solo hilo. Anaitwa Nguza Viking.

Unajua yanayoendelea kwake na watoto wake, na hii si mada ya leo. Leo tunawmangalia tu katika muziki na gitaa. Aliwahi kupiga gitaa na nguli wetu wa bongo komandoo Hamza Kalala.

Nguza mbali ya kupiga muziki alikuwa ni mtunzi mzuri na moja ya kibao kilichompatia umaarufu ni Seya na hasa pale alipokiboresha na mwanae Papi kocha

tizama hii clip ya YouTube ufurahie, hadi wakti mwingine tena


Daaaa masikini babu seya sizonje angemtoa tu km ni kuteseka kashateseka imetosha sasa
 
Lee una maoni gani
Morning mkuu ...

Hope unataka maoni kuhusu lukaku ??

Maoni yangu tanaweza kujikita kwenye ushabiki na uhalisia ila yote ikaletea maana ...kwanza kabisa Lukaku ni moja wa wamaliziaji wazuri hasa mipira ya mwisho na apa ndo utamtofautisha yeye na Costa hasa uzuri wake unanoga kwa kuwa na uwezo wa kukokota mpira na guu lake la dhahabu na nguvu zake alizonazo ...huwezi kumzungumzia Lukaku bila kumzungumzia Jose M huyu baba wanayemuita master mind japo mm yupo kwenye list ya makocha bora kwangu popote alipo

...alichokianza Conte ndicho anachokimaliza Lukaku make Costa mbali na kuwa na msimu mzuri lakini lazima aangalie upande mwingine japo na darajan bado panamfaa ...

Anachojaribu kukifanya Conte ni kuwa na mshambuliaji tegemezi na wa kutegemewa kila mara hii costa amekikosa japo mchango wake ni mkubwa

Bwaaaaanaaaaaah pembeni akae William uku hazard katikati mzee wa pasiii lukaku utampenda ...anatulizaa anafinya kambaniiiiiiii

Moja ya kitu kinachoweza kumsaidia lukaku ni kutaka kumuonesha yule bilionea A kuwa yeye darajan ndo panamfaa japo yule mzee aliona hapamfaii ......

Karibu lukaku panakufaa sana ...


Lakini vipi costa najua utaniulizaaa ...

Twende sawa kiongoziii Jose Mourinho alifanikiwa kutimiza ndoto za Adebayor na Essien kwenda Madrid....
Mourinho akafanikiwa kumrudisha Matic Chelsea...... Jose huyo huyo akafanikiwa sana alipokuwa na muitaliano mweusi Mario Ballotel pale Inter Milan....... Mourinho huyo huyo aliweza kuwagawa waspain ndani ya Real Madrid....... Jose huyo huyo akafanikiwa katika kuuangusha ufalme wa Icar Cassilas pale Bernabeu..... Na sasa kafanikiwa tena kuuangusha ufalme wa Zlatan Ibrahimovic pale Manchester united.

Kama alifanikiwa kwa Emanuel Adebayor na Michael Essien pale Madrid...... Unaweza kushangaa kufanikiwa kwa Diego Costa kuvaa jezi ya United Msimu kesho...? Mourinho ni mwanadamu anayejielewa yeye mwenyewe na baadhi kama mimi na wewe ndio tunaweza kumuelewa....japo ni muhumin sana wa kile anachokiamini na hapa ndo lukaku anajaribu kumuonesha mzee falsafa zake mda mwingine zinafell

Meseji ile ya Conte kwa Costa hope ilikuwa faraja kwa Lukaku ns Jose Mourinho wake ila tkumbuke mda nao una majibu sahih
 
Obe inaonekana kaokota embe dodo chini ya mwembe kwa ulaini kama analia au kuna kingine kinachoendelea? Tangu jana nililiona fukuto la chini kwa chini likifukuta na sasa mnunurisho wa fukuto lile umeanza kutoa joto lenye kusisimua fikra. Na shemeji mtu naona nishapigwa chenga ya mwili. Mapenzi hata hivyo ni kikohozi. Ngoja tusubiri!
Hamna kitu shemeji yule ni just friend hamna kingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom