Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki na Kutokelezea

Piga pamba unavyoweza, tokelezea unavyoweza, jipambe upambike na usishau kutumia muda wako kwenye kioo ili kutambua kuwa kila mmoja wetu ni kichaa kwa aina yake.

Sijui kama ninarudia hiki ninachoandika, lakini hata kama ninarudia hakuna ubaya maana maana inaweza kubadilika kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwemo siku. Ukiwa katika siku zako basi unaweza kuona rangi zote na kama hauko kwenye siku zako basi usishangae ukijikwaa na kulaumu ulipoangukia.

Salama lakini humu ndani? Nilitingwa kidogo, si unajua tena mambo ya kuitafuta siku uimalize mapema, sasa leo nilikuwa kwenye siku yangu, niliiona yaani tight ile mbaya lakini nimeimaliza na sasa nausubiri mwezi, nipokee mshahara. Kadri unavyoimaliza siku yako ndivyo mshahara unakaribia, haijalishi unalipa au unalipwa.

Turudi kwenye muziki, jana nilikwambia kuwa wanamuziki waanzilishi wa Les Wanyika kina Ngereza na Kinyonga walikimbilia Kenya kutokana na ugumu wa uchumi katika tasnia ya muziki, well, hizi mambo ukiona kwako kugumu mwingine anatamani aje. Wakongo kibao walimiminika Bongo miaka ya 70, 80 na 90 na kuendelea hadi kesho.

Mmoja wao alikuwa ni mpiga gitaa mzuri tu ambaye ukisikiza anavyopiga gitaa na kuimba utampenda sana, sauti na gitaa lake, solo hilo. Anaitwa Nguza Viking.

Unajua yanayoendelea kwake na watoto wake, na hii si mada ya leo. Leo tunawmangalia tu katika muziki na gitaa. Aliwahi kupiga gitaa na nguli wetu wa bongo komandoo Hamza Kalala.

Nguza mbali ya kupiga muziki alikuwa ni mtunzi mzuri na moja ya kibao kilichompatia umaarufu ni Seya na hasa pale alipokiboresha na mwanae Papi kocha

tizama hii clip ya YouTube ufurahie, hadi wakti mwingine tena

Asante Obe kwa music
 
Mfano wa kariakoo..

Unakuta majengo mengi ni 7 to 10 floors...all over the street..

Lakini upepo unapovuma toka baharini hakuna mpangilio mzuri wa majengo ili yote yapate natural ventilation..

Majengo yanapaswa kuwa na skyline inayoanzia chini toka usawa wa bahari na kwenda juu...

Yaani majengo yawe marefu kutoka iliko bahari kurudi nyuma..

Majengo mafupi yalipo nyuma ya majengo marefu kutoka iliko bahari ni matatizo sana...There is no ventilation

Kwa mfano nenda ishi kariakoo ama kinondoni ni tofauti na mbezi beach...

Just mpangilio wa majengo hasa overall heights...
 
Nimepoteza kipenzi changu hapa JF
Kama kule MMU sijui
Kama kule MYW sijui
Kama kule intelejensia sijui
Ama kule J photos nitarudi nimtafute............
Daah!

Pole kaka!

I offer you my thoughts, prayers and well-wishes during this dark time in your life...

May my condolences bring you comfort and all jf members...

R i p
 
Unajua. Haya mambo ukiyawaza sana unaweza ukafika mahali ukakufuru na hata kukubaliana na maracist wa Ulaya wanaodai kwamba pengine sisi weusi tuliwahishwa wakati wa evolution na hatukumalizia ngwe yetu sawasawa; au pengine tumelaaniwa kama baadhi ya maandiko matakatifu yanavyodaiwa kusema. Haiwezekani popote pale tulipo hapa duniani (Afrika, Caribbean, Papua New Guinea, Australia, Haiti na hata Marekani kwenyewe) matatizo yetu ni yale yale - UMASIKINI, ubinafsi uliopindukia kimo, uvivu, umbea, ushirikina, kulalamika, kutojali ...). Why? Huwa natafuta sana kisababishi cha jumla lakini huwa sikipati. Tumelaaniwa? Hatuna akili sawasawa? Tatizo hasa ni nini? Kwa nini mtu anasaini mkataba ambao kimsingi ni kuuza kabisa madini yetu kisa tu yeye na familia yake wametajirika? Hawa wengine je?

Kuendelea kuwalaumu wazungu ni execuse tu isiyo na mashiko; na ni ishara kwamba bado tuko kwenye denial na pengine hata hatujui ni kwa nini tumo katika hii paradox ya kushangaza (utajiri mkubwa wa natural resources lakini masikini wa kutisha). Usije nifanya matestosterone yakaanza kunitetemesha bure kwa hasira.

Ni lazima turudi nyuma kabisa na kujichunguza upya pamoja na kujenga mifumo mipya ya kifikra na kifalsafa. Ni lazima tujue sisi ni nani na nafasi yetu ni ipi katika dunia hii ya jaza ujazwe. Mungu katupa kila kitu tulichohitaji kwa ajili ya maendeleo yetu. Ila nadhani Alisahau kutupa akili, upendo, moyo wa uadilifu pamoja na ubinadamu!
c8af5c9314b884e825f8b99b77ffa81d.jpg
 
Kuna kitabu kimoja cha prof mkenya jina limenitoka, nitaandika tena nikikumbuka. Kaongea sana haya mambo kama ulivyoyaeleza, inakera sana.

Tukirudi sisi kwa sisi ndo tatizo kubwa zaidi na wala hatuhitaji kuwasingizia wazungu, ni mindset zetu tu. Haiwezekani hadi leo bado tuendelee kusema matatizo yetu yanaletwa na wazungu. Hivi ni kweli tunapokuwa na tatizo la kukosa umeme tuseme ni wazungu? Hawa si wanauza majenereta? Tunatoa kodi ilhali tunakosa shule zeney kujitosheleza, barabara mbovu, maji shida, na hii kweli tuwasingizie wazungu? Nipe mapumziko tafadhari.

Yaani viongozi kula rushwa na kwenda kuficha mali wanaoztuoibia huko Yuropa na Marikani, tuwasingizie wazungu? No way, tusiangushe lawama zetu kwa mwingine, hii si njia nzuri ya kupambana na stress zetu.

tuseme kweli, sheria za migoodi zisizotunufaisha tuwasingizie wazungu? tembo wetu kuuliwa tusingizie wachina? halafu ukiwmi tunasingizia sokwe😱, sokwe mtu labda.

Shimba na Makapuku asante kwa kuchokoza hii kipenegele kwa leo
Kama ni Mkenya basi nadhani atakuwa Prof. Ali Mazrui (RIP) kama siyo Ngugi. Ana vitabu vingi vyenye mawazo ya kiAfrocentric; na sasa first born wake (Ali Mazrui Jr - Prof wa Rutgers University) ndiye anaendeleza libeneke!
 
Muziki na Kutokelezea

Piga pamba unavyoweza, tokelezea unavyoweza, jipambe upambike na usishau kutumia muda wako kwenye kioo ili kutambua kuwa kila mmoja wetu ni kichaa kwa aina yake.

Sijui kama ninarudia hiki ninachoandika, lakini hata kama ninarudia hakuna ubaya maana maana inaweza kubadilika kutokana na sababu kadha wa kadha ikiwemo siku. Ukiwa katika siku zako basi unaweza kuona rangi zote na kama hauko kwenye siku zako basi usishangae ukijikwaa na kulaumu ulipoangukia.

Salama lakini humu ndani? Nilitingwa kidogo, si unajua tena mambo ya kuitafuta siku uimalize mapema, sasa leo nilikuwa kwenye siku yangu, niliiona yaani tight ile mbaya lakini nimeimaliza na sasa nausubiri mwezi, nipokee mshahara. Kadri unavyoimaliza siku yako ndivyo mshahara unakaribia, haijalishi unalipa au unalipwa.

Turudi kwenye muziki, jana nilikwambia kuwa wanamuziki waanzilishi wa Les Wanyika kina Ngereza na Kinyonga walikimbilia Kenya kutokana na ugumu wa uchumi katika tasnia ya muziki, well, hizi mambo ukiona kwako kugumu mwingine anatamani aje. Wakongo kibao walimiminika Bongo miaka ya 70, 80 na 90 na kuendelea hadi kesho.

Mmoja wao alikuwa ni mpiga gitaa mzuri tu ambaye ukisikiza anavyopiga gitaa na kuimba utampenda sana, sauti na gitaa lake, solo hilo. Anaitwa Nguza Viking.

Unajua yanayoendelea kwake na watoto wake, na hii si mada ya leo. Leo tunawmangalia tu katika muziki na gitaa. Aliwahi kupiga gitaa na nguli wetu wa bongo komandoo Hamza Kalala.

Nguza mbali ya kupiga muziki alikuwa ni mtunzi mzuri na moja ya kibao kilichompatia umaarufu ni Seya na hasa pale alipokiboresha na mwanae Papi kocha

tizama hii clip ya YouTube ufurahie, hadi wakti mwingine tena

Seya wa mivalo

Umeufanya usiku uwe mwanana mkuu Jorowe
 
Ikawaje ukajiita Bitoz mkuu?

Mwenyewe nilimpenda Thomas Muller tangu 2010 so wakati najiunga JF jina lake ndo likaja fasta
Sijajiita bali watu wananiita
Ndugu + marafiki kuanzia shule hadi chuo waliniita hivyo kutokana tu na jinsi ninavyovaa
Si unajua "majungu" ukiwa smart wanakuita bishoo/tozi...ukiwa rachafu/rafurafu wanakuita mshamba

Hivyo kwangu wala sikumind kuitwa toz
Na ndo sababu nalitumia hata hapa JF
.......
 
Weweweeeee
Obe inaonekana kaokota embe dodo chini ya mwembe kwa ulaini kama analia au kuna kingine kinachoendelea? Tangu jana nililiona fukuto la chini kwa chini likifukuta na sasa mnunurisho wa fukuto lile umeanza kutoa joto lenye kusisimua fikra. Na shemeji mtu naona nishapigwa chenga ya mwili. Mapenzi hata hivyo ni kikohozi. Ngoja tusubiri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom