Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo Katika Historia:

1970 - Nyimbo ya The Long and Winding road iliyoimbwa na kikundi cha The Beatles inakuwa nyimbo ya mwisho ya kundi hilo kushika namba 1 katika chat za muziki nchini Marekani.
f69cdd3c54ac7eafb89a0267ba33a2d3.jpg
e1bf665c63882da6fec40dc445e99ae8.jpg

Ni kundi la vijana wanne mabishoo wa miaka ya 60's
Ndiyo chimbuko la vijana watanashati na kuitwa matozi
Baada ya hapo kila mtu anafanya kazi kivyake Solo artist
......
 
1971 - Wakati wa Vita ya Vietnam: Gazeti la The New York Times linaanza kuchapa taarifa za siri za Marekani katika vita hiyo zilizojulikana kama The Pentagon Papers!
2001ca26523fab608befb84145acb883.jpg
c8e302a320fc3c16563c81e278a2841d.jpg

Ikumbukwe USA aliharagazwa huko Vietnam wakati ya vita kati ya Kusini na Kaskazini amvapo yeye alikuwa anasapoti upande mmoja wenye maslahi yake
.....
 
1942 - Walter Rodney anazaliwa.

Alikuwa ni msomi, mwanaharakati kutoka nchini Guyana.

Moja ya kazi yake ni kitabu cha " How Europe Underdeveloped Africa ". Kitabu ambacho Wazungu hawakukipenda.

Alifundisha chuo kikuu cha Dar Es Salaam miaka ya 1970's.

Aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari lake mwaka 1980.
 
1955 - Alan Hansen anazaliwa.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Scotland.

Alipostafu kabumbu akaenda kuwa mchambuzi wa soka wa BBC katika kipindi cha Match of the Day.

Moja ya kauli zake maarufu ni " You can't win anything with kids, ni baada ya timu ya Man Utd ilipofungwa 3-1 mechi ya ufunguzi wa ligi na Aston Villa msimu wa 1995/96.

Katika mechi hiyo Man Utd iliwapandisha makinda wake katika kikosi cha kwanza baada ya kuuza wachezaji wake mastaa kama Mark Hughes na Paul Ince, na kuwapandisha makinda ambao ni Gary na Phil Neville, Ryan Giggs, Nick Butt na David Beckham.

Lakini pamoja na kauli hiyo, makinda hao walikuja kutwaa Ligi na Kombe la F.A mwisho wa msimu na kumfunga mdomo Hansen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom