Makapuku Forum

Makapuku Forum

Na hivyo humu tupo watu tunajuani hadi viwanda tunavyoishi
Kipimo kimojawapo cha urafiki ni pale unapovutiwa na mtu hata kwa mwandiko wake tu
Humu tunajaliana na kufarijiana pengine kuliko WhatsApp group za wana ndugu ambao unaweza kuwaambia "unaumwa" na wakauchuna tu
Naamini ni bora rafiki anayenijali kuliko ndugu wa damu asiyenithamini
.......
Kweli kabisa bwana madenge
 
Siyo "couple za humu" kuna watu ni mapenzi kweli mdau
Endelea kung'aa tu sharubu


......

SEHEMU YA 03

"Dooh! nimepoteza kila kitu shaabash!" Nilisema mwenyewe nilipobaini kuwa lazima nilividondosha kwenye hekaheka ile hasa nilipokumbuka kuwa hata kwenye daladala nauli sikulipa wala konda hakunidai punde niliposhuka kule njiani. Nilishusha pumzi na kumshukuru tena Mungu na kuwazia hata nitaponunua simu sitokuja kuirejesha namba yangu wala sitomtafuta tena Mariamu kivyovyote. Niliwasha jiko la mchina na kuchemsha maji kisha nilielekea moja kwa moja bafuni kwa zoezi la kujikanda na kujisafisha kabla ya kwenda famasi kununua dawa za kutuliza maumivu.

* * * * *

Ilipita wiki nzima nikiwa mnyonge sana kuanzia kazini mpaka mitaani sikuwa na shauku hata ya kutaka kujua maendeleo ya Mamu wala sijapata salamu zozote kutoka kwao. Upande wa pili moyoni nilikubaliana na maneno ya yule bwana kuwa inawezekana kuwa kweli wanawake ni wauaji. Nilijiuliza endapo yule baunsa angenizimisha ama kuniua yote ingekuwa kwa sababu ya Mamu. Pia niliwaza kuwa ina maana Mamu alidhamiria muda mwingi kufanya vile ama alifanya kama kulipa kisasi kwa maneno yangu? Lakini ikawaje iwe mapema vile tena siku ile ile?
Nilichoka na kuendelea kumlaani licha ya ukweli kuwa nilimpenda sana. Miezi ilipita na hatimaye ilikatika miezi nane nikiwa sijawahi kuwa na mahusiano mengine yoyote wala kukutana kimwili na mwanamke. Na katika siku hizo tulipata safari kikazi mkoani Arusha na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Arusha.
Jiji la Arusha lilikuwa tofauti sana na Dar kuanzia hali ya hewa hadi tabia za watu. Sio siri katika kipindi kifupi nilijikuta nalipenda sana jiji lile. Lakini mara kwa mara usiku nilikuwa naandamwa na ndoto kuhusu wanawake. Na kubwa zaidi nakumbuka siku moja usiku nikiwa nimelala niliota kuna sehemu tumeenda kufanya kazi muda wa mapumziko mchana tulizunguka eneo moja ambapo nilikutana na msichana mzuri sana na katika maongezi nilipomuuliza jina alinambia kuwa anaitwa Zai. Nilishtuka usingizini na kuifikiria sana ile ndoto lakini mwishowe niliipuuza nikiamini huenda ni kutokana na kutofanya mapenzi muda mlefu ndio maana ndoto za wasichana ziliniandama. Lakini cha ajabu siku mbili baadae nilishangazwa tulipofika eneo ambalo lilifanana kabisa na lile nililoliota na kilichokuja kunishangaza zaidi na zaidi nikiwa na mshikaji wangu tunatembea tulipishana na msichana mmoja mzuri sana na tuliangaliana huku sura yake ikiwa haina tofauti kabisa na yule niliyemuota.
"ZAI!" Sauti iliita ubongoni baada ya kukumbuka jina la yule niliyemuota na kujikuta nikiliropoka kumwita yule binti tuliyepishana naye.
“Oyaa unamjua au ndio unaleta uroporopo kwenye miji ya watu?”
Aliniuliza rafiki yangu lakini kabla sijamjibu kitu niliita mara ya pili kwa sauti zaidi ya mwanzo na tulipogeuka tulishangaa kuona binti amesimama nae akiwa amegeuka akitutazama kwa mshangao. Nilipiga moyo konde na kumsogelea nikimuacha ndani ya bumbuwazi rafiki yangu.
“mambo Zai.” Nilimsalimu kwa kumhakikishia kuwa sikubahatisha kumwita ingawa nilificha mshangao wangu wa kuona kile nilichokiota kikienda mubashara.
“Poa, ila mbona sikukumbuki na sidhani kama tuliwahi kuonana!” kwa sauti tamu ya malaika binti alijibu kwa mshangao.
“Ni kweli unaweza kuwa sahihi kwa upande mwengine miili yetu haijawahi kuonana ila nafsi zetu ziliwahi.”
“kivipi mbona sikuelewi.”
“Utanielewa tu, kama hautajali chukua namba zangu hizi tuwasiliane kwasasa nina haraka.” Niliongea na kumkabidhi kikadi changu cha mawasiliano huku nae akikipokea akiwa bado ametaharuki nilimuaga na kuondoka. Sijui hata niliutolea wapi ujasiri wa majibu yangu pindi nilipokuwa nazungumza na yule binti. Nilimkimbilia rafiki yangu ambae alibaki ameduwaa muda wote niliposimama na yule mrembo.
“mwanangu mbona sikusomi?”
“hahahaaa hamnaaa utanisoma tuu.”
“heee! Hayaa, sema mtoto mkali kishenzi, umemjuaje?”
“nitakwambia tu usiogopee” Nilimzuga rafiki japo bado alionesha hajaridhika na majibu yangu na kujikuta akienda anageuka nyuma kumtazama yule binti na kunitaarifu kuwa bado alikuwa amesimama akitushangaa. Sikutaka kugeuka zaidi ya kujiuliza sana kichwani imekuaje nimeota ndoto na imetokea vilevile!
Nilihisi ujinga kama nitamwambia mshkaji eti simjui yule demu ila nilimuota na jina lake alinitajia ndotoni. Nilijua huo utakuwa ujinga ambao asingeniamini kabisa kwani si rahisi mtu kumuota mtu asiyemjua akamtajia mpaka jina halafu siku si nyingi wakakutana tena kiukweli na ikawa vilevile.
Tulirudi kuendelea na kazi huku muda mwingi nikiwa na shauku ya kupigiwa na yule mrembo lakini ajabu siku zilipita sikupigiwa simu na Zai wala kupata ujumbe wake na kwakuwa sikuchukua namba yake iliniwia vigumu kumtafuta na hata tulipotembelea tena yale maeneo sikuwahi kumuona. Nilijilaumu kutochukua namba yake lakini muda mwengine niliogopa hasa imani yangu ilipoenda mbali na kuhisi huenda atakuwa jini. Siku zilisonga hali ikiwa ile ile hadi muda wa kuwepo Arusha ulipoisha na safari ya kurejea Dar ilijili na kukusanya vitu vyetu kurudi rasmi pasipo kumuona tena Zai.

* * * * * *

Ilipita miezi minne sawa na mwaka mmoja tangu niachane na Mariam na nilikuwa nimehama kabisa lile eneo nililokuwa nakaa awali na nilipanga sehemu nyengine pembezoni mwa jiji. Maumivu ya kupenda yalisahaulika moyoni na kutamani kupenda tena. Upweke uliutesa mwili na kuhitaji mwenza ingawa hofu ya kutokea kama ya awali haikucheza mbali nami. Niliuvaa umakini machoni ili moyo usiteleze tena.
Siku hiyo nilipotoka kuoga baada ya kurudi kazini nilikuta simu ikimalizia kuita na nilipoitazama namba ilikuwa ngeni na kulikuwa na 'missed calls' nne. Nikiwa bado nina taulo niliamua kuipiga ile namba huku nikiwa nimesimama najiangalia kwenye kioo cha 'dressing table' na haikuchukua muda kuita sana upande wa pili mara ilipokelewa na sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni ilisikika.
‘’’Hallow, samahani naitwa Zai nipo hapa Arusha uliwahi nipa hii namba siku moja japo ni muda kidogo ulipita nilikuwa na matatizo nilisahau kukupigia.. nadhani naongea na mtu sahihi!”
Sio siri nywele zote zilinisisimka kusikia sauti ya mrembo wa ndotoni ambae niliwahi kukutana nae nilipokuwa Arusha kikazi na nilishakata tamaa ya kuonana nae tena. Eti leo kanitafuta mwenyewe baada ya kimya kingi kupita!?.
Kwa hamasiko na furaha nilijikuta namjibu harakaharaka.
“kweli kabisa ni mimi Hussein hapa upo wapi Zai?”
“Mi niko Kijenge na leo asubuhi nilipokiwa napangapanga nguo zangu kwaajili ya safari ndio nikaikuta namba hii kwenye begi langu moja niliihifadhi na nilishasahau lakini nilipoiona ndio nikakukumbuka hivyo nimeona vyema nikuage pia unikumbushe umenijuaje maana maneno yako siku ile yalinichanganya sana kama unaweza tuonane leo maana umenitia shauku ya kujua tulionana wapi.”
“Oooooh, unasafiri kesho..! wapi sasa?”
“naenda Dar”
“Dar!!! Haha Mungu mkubwa mi mwenyewe niko Dar huko nilikuwa kikazi tu.” Nilimjuza Zai na tukaongea mengi sana juu ya safari yake ambapo alinambia kuwa ndio mara yake ya kwanza kuja jijini na safari yake ni kwaajili ya masomo ya elimu ya juu na angefikia kwa shangazi yake huko Kinondoni.
Ingawa alinilazimisha nimwambie tulionana wapi lakini nilimzuga kuwa tutapoonana atapokuja nitamkumbusha.
Na kweli baada ya Zai kufika jijini Dar na ilipopita wiki moja tu alinijuza na siku ya jumapili ilibidi niende pande za Kinondoni kuonana nae hasa aliponiomba kwa madai ya ugeni wake asingeweza kutoka. Nilifika na kukutana nae kituo cha basi kama alivyohitaji. Moyoni nilifurahi japo kichwani sikuamini kama yule mrembo wa ndoto leo niko nae kwa mara ya pili tena hapa Dar. Baada ya salamu ndipo bila mbwembwe nyingi nilijikuta namwambia ukweli kwa fafanuzi kuwa hatukuwahi kuonana kimwili lakini niliposema nafsi zetu ziliwahi kuonana nilimaanisha kuwa niliwahi kumuota na akanitajia mpaka jina.
“hahahahahaaa usinichekeshe bwanaa hebu nambie kweli” Alicheka kwa kuamini yalikuwa maneno ya mzaha. Nilimtazama vyema alivyokuwa anacheka kwa mara ya kwanza niliushuhudia uzuri yakinifu na hata nafsi ilimpigia saluti binti alivyokuwa mrembo hadi nashindwa kuelezea.
“kweli Zai na ndivyo ilivyokuwa ila mi nahitaji tuwe karibu zaidi ya hapa” Nilikazia na kumshika mkono huku nikiivaa sura ya mahaba kama Sharukhan.
“kivipi..?” Kicheko kilimwisha ghafla na kunikazia macho punde nilipomshika mkono aliuputa na kusimama kiumakini baada ya kuniuliza.
“namaanisha tuwe na mahusiano ya ndani kabisa na endapo utakuwa radhi niko tayari kukuoa hata kesho Zai kwani naamini wewe ni mwanamke niliyeelekezwa na Mungu moja kwa moja kwenye maono” Niliongea kwa upole na sauti ya kumaanisha lakini maneno yangu safari hii hayakumfurahisha Zai.
"Lol! kumbe hilo ndilo lengo lako? kujizungusha kote sijui nimekuota sijui nini lol! samahani kakaangu naomba usipoteze muda wako na umwambie huyo aliyekutajia jina langu kuwa siko hivyo. Hiyo ndoto haipo na kutokea usahau...Kwaheri." Aliniaga baada ya kunishua na kuondoka huku kijungu chake mnato kikitingishika kimadoido. Nilijaribu kumzuia ili anisikilize zaidi lakini Zai hakusimama hata nilipomshika mkono aliuputa. Sikuwa na jinsi ilibidi nami nigeuze huku nikijilaumu upande wa pili kwa kuwahi kumwambia vile kabla hata sijamuweka karibu zaidiii.....

Next episode .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom