1962 - Wafungwa Frank Morris, na ndugu wawili Clarence na John Anglin wanakuwa wafungwa pekee kufanikiwa kutoroka katika Gereza la kisiwa la Alcatraz huko Marekani.
Gereza la Alcatraz lipo kisiwani na limezungukwa na maji yenye baridi kali na kina kirefu sana lakini Wafungwa hawa walifanikiwa kutoroka na hawakuwahi kuonekana tena.
Licha ya msako mkali wa kwenye maji, ardhini na anga wafungwa hawa hawakuwahi kupatikana tena, licha ya tetesi kudai walifanikiwa kutoroka na kwenda Brazil ila kuna wengine wanaamini wafungwa hao walikufa kutokana na baridi kali ya maji japo hakuna maiti iliyowahi kupatikana.