Makapuku Forum

Makapuku Forum

Usiku mwema makapuku. Tuonane kesho panapo majaliwa. Zingatieni ushauri huu hapa chini ‍♂️‍♂️‍♂️
6f420b7e8d51baadf91d113e54ea5437.jpg
 
Pamoja sana Mkuu, umeweza kufanikisha top 10 japo tumekushtukiza.

Pia kwa nyongeza chache, kuna D.B Cooper ambaye mpaka leo hajulikani alipo.

Camilo Cienfuegos wa Cuba ndege aliyopanda haikuwahi kuonekana tena licha ya msako mkali wa kutafuta Ndege hiyo!

Mkuu Bitoz asante!!
D.B Cooper alikuwepo nje ya Top 10
Alikuwa # 14
Pia ningemuandika yaani ningemweka kwenye top 10 ila stori yake nafikiri humu wengi walishaisoma kule kwa "bwana yule" hivyo afadhali hao wengine stori zao baadhi hazijasikika
.....
 
D.B Cooper alikuwepo nje ya Top 10
Alikuwa # 14
Pia ningemuandika yaani ningemweka kwenye top 10 ila stori yake nafikiri humu wengi walishaisoma kule kwa "bwana yule" hivyo afadhali hao wengine stori zao baadhi hazijasikika
.....
Halafu ukimtaja si ajabu "bwana yule" akataka acknowledgement... Ni mkali kweli kweli kwenye haya mambo!
 
D.B Cooper alikuwepo nje ya Top 10
Alikuwa # 14
Pia ningemuandika yaani ningemweka kwenye top 10 ila stori yake nafikiri humu wengi walishaisoma kule kwa "bwana yule" hivyo afadhali hao wengine stori zao baadhi hazijasikika
.....


Niombe kitu mdau, kila mmoja ana aina yake ya uandishi. Zipo source kadhaa zinatofautiana so, kwa hili. Ukipata muda hebu muandike huyu Cooper, una style nzuri ya kuandika na inavutia.

Well, ni jambo zuri ukiandika na ukaweka humu. Binafsi uandishi wako na suportives unanifanya nipende kusoma unapopost. Take your time buddy, hata aya tatu tu zinatunufaisha Makapuku
 
Muziki na Kukumbushana

Habari Makapuku wenzangu, ni siku nyingine tena inayoishilia, yeah, ikawa asubuhi, mchana na sasa ni usiku lakini kama mnavyoijua JF na Makapuku forum, unaweza kuta kuna sehemu saa hizi ni saa mbili asubuhi watu wanapata stafutahi (hili neno linaendana na astashahada?)

Well, kuna muda unakuwa unatamani uwe tajiri sana na wakati mwingine uwe kichaa usitozwe kodi, hayo ndo maisha. Kutamani sio kosa, kosa linakuja pale unapotamani kitu kwa husuda.

Usiku huu kwenye muziki na utamu wa gitaa, sina maneno mengi sana. Nakuletea mwanamuziki maaruu kabisa wa Afro-Zouk Oliver N'Goma almaarufu Oliva Ngoma.

Wengi tunamkubuka kwa sauti yake tu bila kujua jamaa alikuwa ni mpiga gitaa mkali tu na aliwahi kufanya muziki wa reggae japo si kwa kiwango kikubwa sana maana baadaye alimezwa na kazi yake ya ukameraman hadi pale alipokutana na mkongwe Manu Lima huko paris ambapo waliandaa album iliyofanya vema na akaendelea kutoa nyimbo nzuri hadi pale alipofariki mwaka 2010. Ndo maisha.

Hebu mcheki hapa na kibao chake Adia

hadi wakti mwingine tena watu wema wa Makapuku.


Mpaka leo sijaona wa kumfananisha katika muziki wa zouk.

Ahsante umenikumbusha mbali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom