Katika dondoo za bbc leo hii ....

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May, amesema yuko tayari kubadilisha sheria yoyote ya haki za binadamu ambayo inazuia polisi na vikosi vya usalama kupambana ipasavyo na tishio la ugaidi

Rais Trump ameungana na nchi ya Saudi Arabia katika mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea na Qatar, huku akiusifu msimamo wa nchi hiyo ya tawala ya kifalme wa kuitenga nchi jirani baada ya Qatar kutuhumiwa kusaidia kifedha makundi yenye msimamo mkali

Mkutano wa 69 wa vyombo vya habari Duniani,leo utafunguliwa rasmi
na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ili kulinda uhuru wa vyombo vya habari na pia
kulinda uhuru wa kujieleza

Ingawa ufugaji ndio tegemeo la uchumi wa taifa la Somalia, biashara ya uvuvi pia imekuwa ikishika kasi kutokana na uwepo wa soko ya samaki katika mataifa ya nchi za kigeni.

Wanaume nchini Uganda wamehimizwa kwenda kupimwa kwa hiari kuona ikiwa wanavirusi vya ukimwi au laa ili kuupiga vita katika juhudi za kuwa na Uganda isiyokuwa na UKIMWI ifikapo mwaka wa 20130

Serikali ya Burundi imetoa tangazo la kuishutumu jumuia ya ulaya kwa kuhusika katika machafuko yaliyo ikumba Burundi tokea mwaka 2015.

Katika kesi inayoendelea dhidi ya watuhumiwa kwa vitendo vya mauaji katika mji wa BENI mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya congo ,kanali mmoja wa cheo cha juu amehukumiwa miezi 32 jela
AMKA NA BBC KWA TAARIFA ZAIDI