Makapuku Forum

Makapuku Forum

Utafiti huu wa Makamu wa rais wa Zimbabwe kiboko. Baada ya miaka mitano mizima hatimaye utafiti wake umebainisha kuwa mayatima wengi nchini humo hawana wazazi walio hai!
e899a4915ac2c091b8e365f5a9cae2ff.jpg
 
Muziki ni UtangamanoNi siku nyingine tunaelekea kuimaliza Makapuku wenzangu. Hongera kwetu bila kujali siku ilikuwa vipi kwa mmoja mmoja.

Siku zote ninapenda kufurahi na kutabasamu sababu ikiwa 'maisha yangu ni mimi na ninajikubali'. yeah, ila leo nimefurahi zaidi maana, kwanza, ni tarehe ya mwisho wa mwezi kuelekea nusu mwaka. Maana yake, mwenye nyumba wangu amekuwa akinisalimia mara nyingi sana wiki hii na hasa leo, nadhani ana lake jambo,,,, oh, kodi ya nyumba. Pili, nimepata shati la mikono mirefu la kumechisha na saa yangu. naamini huna tatizo na masuala yangu binafsi, private matters.

Turudi kwenye muziki, leo tunaenda Senegal. Ndiyo, kule kule kwa kina Bauba Diop na kina Mame, lakini hawa ni wacheza soka na kakipenegele ketu ka muziki kako mbali sana nao.

Namuongelea Youssou N'Dour. Mwanamuziki nguli si tu barani Afirca bali sehemu nyingi duniani. Anatajwa kuwa ni mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi kupita wanamuziki wengi Africa. Utaamua mwenyewe.

Ni mcheza sinema (itafute "return to Goree 2007, utaipenda mimi nilishaiona pia na pia ipo Amazing grace). Hizi zote zina umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa sinema.

Keshawahi kuwa waziri nchini Senegal na sasa ni mshauri maalum wa rais wa nchi yake. Anasifika kwa kuhimiza utangamano si tu nchini kwake bali duniani kote na ndiyo maana keshafanya kazi na UN pamoja na mshirika yake karibia yote. Hii ndo faida ya kuwa mwanamuziki wa muziki wako (Unanielewa?)

Aliandika na kutumbuiza wimbo mahsusi wa FIFA world Cup 1998 na keshashinda tuzo ya Grammy.

na zaidi, kutokana na kazi yake ya muziki, chuo kikuu cha Yale kilimtunukia udaktari wa falsafa (honorary doctorate) na kwa niaba ya Makapuku wote basi tunamtunukia PhD pia (swali kaa nalo, hoja ilete)

Hapa tumwangalie katika wimbo wake maarufu kabisa Birima na usijesema mbona sijaongelea gitaa leo, no, mpiga gitaa lililoendana na sauti nzuri kabisa ya Youssou anaitwa Jimi Mbaye.

Jukwaa huru hili, kama unaona naandika sana badala ya kuweka muziki, unajua namna ya kutoa maoni

Burudika


Asante Obe, namkubali sana
 
Wakuu leo kuna mkanganyiko mkubwa wa data
Navyosonga mbele nakuta na kujiua pia kunahesabiwa
Sehemu nyingine kujua pekee
Hivyo naishia hapa maana siwezi kuandika kitu kisichojitosheleza au kilicho tofauti na utangulizi

Hivyo tukutane kesho
************************
Ni tatizo tu lililojitokeza hivyo litanikomaza na kunifanya nizidishe umaskini siku nyingine

Samahani kwa usumbufu na post nilizopost nadelete maana siku zote huwa naandika kitu kisicho na shaka au kupotosha
............
I like your integrity, work ethic and character. Asante sana!
 
Tunahitaji kuwa na taasisi imara za usimamizi, ili kuepukana na haya ya kwenda kusaini mikataba London

Too late. Ni suala la kifalsafa zaidi na kimfumo kama jamii. Bila kubadili mfumo na falsafa ya jamii kuhusu dhana nzima ya uongozi, utajiri na elimu hizo taasisi imara nazo zitafanya yale yale as long as zinaongozwa na watu ambao ni zao la falsafa na mfumo ule ule...
SHIMBA huwa unanifurahisha pia najifunza mengi kila unapoongelea siasa,uchumi.historia n.k
Kiufupi nchi imeoza au km ni kansa basi imeshafika kichwani na tukimpasua mgonjwa ana % ndogo ya kupona na tukiamua kumuacha anateseka na maumivu na hachelewi kufa

Tuliipuuza misingi aliyotuwekea Kambarage

.......
 
SHIMBA huwa unanifurahisha pia najifunza mengi kila unapoongelea siasa,uchumi.historia n.k
Kiufupi nchi imeoza au km ni kansa basi imeshafika kichwani na tukimpasua mgonjwa ana % ndogo ya kupona na tukiamua kumuacha anateseka na maumivu na hachelewi kufa

Tuliipuuza misingi aliyotuwekea Kambarage

.......
Kweli, mimi mwenyewe nimemsoma nikamuelewa

Tatizo ni mkwapa kufuta kabisa jkt, hapo uzalendo ndio ikawaje by by
 
Kweli, mimi mwenyewe nimemsoma nikamuelewa

Tatizo ni mkwapa kufuta kabisa jkt, hapo uzalendo ndio ikawaje by by
Sizonje kachagua kuwapasua wagonjwa vichwa matokeo yake wengi wamekufa(makampuni,biashara,ajira n.k)
Tunamlaumu lakini madaktari waliomtangulia walizembea kututibia wagonjwa wetu pindi dalili za kansa zilipoanza

Kinga ni bora kuliko tiba

......
 
Utakuta hapo kavaa tu na wanaoelewa wala hawamwambii maana yake bali wanaishia kumcheka na kumpiga picha. Not cool!
Ndio tulivyo lakini,katika hili mara nyingi hatuwasaidii wale tunaokutana nao kwa kuhofu watapokeaje au kwa kuona sio wajibu wetu,Mungu atusaidie kuwa tayari kuwasaidia wenzetu wasiingie katika mitego hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom