Muziki ni UtangamanoNi siku nyingine tunaelekea kuimaliza Makapuku wenzangu. Hongera kwetu bila kujali siku ilikuwa vipi kwa mmoja mmoja.
Siku zote ninapenda kufurahi na kutabasamu sababu ikiwa 'maisha yangu ni mimi na ninajikubali'. yeah, ila leo nimefurahi zaidi maana, kwanza, ni tarehe ya mwisho wa mwezi kuelekea nusu mwaka. Maana yake, mwenye nyumba wangu amekuwa akinisalimia mara nyingi sana wiki hii na hasa leo, nadhani ana lake jambo,,,, oh, kodi ya nyumba. Pili, nimepata shati la mikono mirefu la kumechisha na saa yangu. naamini huna tatizo na masuala yangu binafsi, private matters.
Turudi kwenye muziki, leo tunaenda Senegal. Ndiyo, kule kule kwa kina Bauba Diop na kina Mame, lakini hawa ni wacheza soka na kakipenegele ketu ka muziki kako mbali sana nao.
Namuongelea Youssou N'Dour. Mwanamuziki nguli si tu barani Afirca bali sehemu nyingi duniani. Anatajwa kuwa ni mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi kupita wanamuziki wengi Africa. Utaamua mwenyewe.
Ni mcheza sinema (itafute "return to Goree 2007, utaipenda mimi nilishaiona pia na pia ipo Amazing grace). Hizi zote zina umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa sinema.
Keshawahi kuwa waziri nchini Senegal na sasa ni mshauri maalum wa rais wa nchi yake. Anasifika kwa kuhimiza utangamano si tu nchini kwake bali duniani kote na ndiyo maana keshafanya kazi na UN pamoja na mshirika yake karibia yote. Hii ndo faida ya kuwa mwanamuziki wa muziki wako (Unanielewa?)
Aliandika na kutumbuiza wimbo mahsusi wa FIFA world Cup 1998 na keshashinda tuzo ya Grammy.
na zaidi, kutokana na kazi yake ya muziki, chuo kikuu cha Yale kilimtunukia udaktari wa falsafa (honorary doctorate) na kwa niaba ya Makapuku wote basi tunamtunukia PhD pia (swali kaa nalo, hoja ilete)
Hapa tumwangalie katika wimbo wake maarufu kabisa Birima na usijesema mbona sijaongelea gitaa leo, no, mpiga gitaa lililoendana na sauti nzuri kabisa ya Youssou anaitwa Jimi Mbaye.
Jukwaa huru hili, kama unaona naandika sana badala ya kuweka muziki, unajua namna ya kutoa maoni
Burudika