Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
MAMBO YANAYOFANYA VIJANA WA KARNE YA 21 WASIENDE KANISANI.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Anayeandika hapa ni kijana msomi mbobevu wa Biblia, na vitabu mbalimbali.
Mbali na hivyo ni msomi wa ngazi ya shahada. Hivyo anaandika akiwa na Uelewa wa kiwango cha juu wa kile akisemacho.

Vijana hawaendi kanisani na wala siwashauri waende.
Haiwezekani mahali pa Mungu pakose mvuto. Haiwezekani!

Yaani unafika Kanisa limezubaa!
Waumini wamezubaa!
Wahudumu wamezubaa!
Wachungaji wamezubaa!!

Yaani katika vitu sivipendi ni kuona mtu aliyezubaa zubaa, au Mazingira yaliyozubaa.

Ukiingia Kanisa lililozubaa lazima nawe uzubae. Lazima ukitoka uwe umezubaa. Upo upo tuu.

Inakuwaje watu wa Mungu wanazidiwa maarifa na Wale watumishi wa kishetani. Wengi wanafanya kazi Kwa mazoea, watu wa Shetani hawafanyi vitu Kwa mazoea,

Siku moja nimeingia Casino maarufu jijini DAR ES SALAAM huko Jamani ni Raha tuu, watu wabunifu, mazingira mazuri, Raha juu ya Raha!

Lakini upande wa makanisa mengi yaani wamezubaa, Khaa! Ubunifu sifuri.
Yaani Bora liende. Alafu Vijana wasipokuja kanisani wanatoa vitisho Kama wendawazimu,
Yaani mtu aje kanisa limezubaa ili naye azubae kisa Sijui Pepo sijui mbinguni, embu kuweni Sirius.

Kuweni wabunifu, acheni kuzabaa.
Wekeni program za kueleweka,
Alafu hizi Dini kubwa sasa Kama taasisi kubwa zimeshindwa kuyaendesha ni Bora wazibinafsishe Kwa watu watu waonyeshe ubunifu wao Kwa kufuata utaratibu wa Kidini na kiimani.

Jambo lolote lisilo na mvuto ujue halina maana yoyote.

Sio kila mtu awe mchungaji jamani!
Sio kila mtu awe mhubiri jamani!
Sio kila mtu awe Mnenaji jamani!

Hii ndio inasababisha Kanisa kuzubaa.
Unakuta mtu anapanda mimbarani Hana karama ya kuhubiri, kunena au kuzungumza mbele za watu, kazi kuzubaisha waumini na kuwafanya walale.

Kuhubiri hajui,
Kufanya-reflection hajui,
Historia ya nchi na Dunia hajui,
Kazi kuzubaisha watu na upuuzi tuu.

Ninyi mnaoenda kusomea uchungaji au mambo yote yanayohusu kusimama mbele za waumini nawasihi hakikisheni mnavipaji vya kuhutubu mbele za watu. Sio mlete mambo ya hovyo hovyo hapa.

Hakuna Jambo linakera na kuudhi mmehamasisha watu kutoa michango Kwa ajili ya mikutano, watu wamejiminya mpaka wakachanga alafu kwenye mkutano mnamleta mhubiri asiyejua kuhubiri, aliyezubaa zubaa, yaani mnazingua acheni Leo niwape vipande vyenu.

Jueni watu wanatoa pesa zao sio tuu Kwa kazi ya Mungu Bali pia na Nafsi zao zifurahia pesa zao.
Waumini ndio wateja, sasa watu wanatoa pesa alafu wewe unaenda kuwazubaisha. Pumbavu!!

Ni wakati sasa wa Dini zifanye Vetting na kuwachuja wahubiri wasioweza kuhubiri, wasio na karama za kuhubiri.

Mungu kaweka karama Kwa kazi hizo, mtu Hana karama ya kuhubiri mnampaje ahubiri?
Kisa kasomea siyo!! Embu acheni hizo!

Hivi Kama ingekuwa ni biashara yako wewe ungekubali umpandishe mhubiri asiyeweza kuhubiri katika Kanisa lako?

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Nitakuja ku-comment baadae nmeitwa na bishop hapa mara moja
 
Kuna wachungaji kadhaa wa kiume na kike kule tik tok wanachokihubiri ni vituko vitupu, kuna ambao wamejikita kufundisha mapenzi na mahaba bila aibu
 
Mafundisho yanayofundishwa ni manyonge, na mengine yamejaa ulaghai na hadaa kwa wenye shida na uhitaji. Sasa kuna maana gani kwenda kusomea theolojia? Ni kuja kudanganya na kupumbaza watu? Wengine wanataka kujaza watu tu ili kutunisha fuko la sadaka na michango huku wakirudi wakavu majumbani mwao bila kupata mahubiri yenye upako wa Mungu
 
Ukiingia nyumba za ibada sku hizi kelele za mziki unaopigwa hapo hata bar huwez zisikia. Kwaya za sku hizi hata sio bongo fleva ni bolingo na zile za twanga pepeta.
Kwa sisi makanisa ambayo tunakuwa na vitabu sku hizi hata uspoenda navyo sawa tuu.
Mimi binafsi Nabarikiwa sana na nyimbo za kitabuni rather than miziki wanayoita kwaya, hasa kipindi hiki tunachoendea cha majilio, kuna nyimbo nzuri ambazo kwa mwaka tunaimba mara moja.

I miss old days.. when..
 
Asante Sana robert.wengi hawajakuelewa .mvuto unahitajika hasa wa kiroho.karama na vipawa NI muhimu.watu wanasinzia kwa sababu hakuna neno lilolo hai.Neno linaandaliwa.wachungaji wengi NI wachivu kwa kazi na mishe tu.anakunguta bible.ujumbe anapatia madhabahuni
 
Umenikumbusha Lutheran ya zamani. Dah. Nyimbo za vitabuni zina raha yake aisee
 
Asante Sana robert.wengi hawajakuelewa .mvuto unahitajika hasa wa kiroho.karama na vipawa NI muhimu.watu wanasinzia kwa sababu hakuna neno lilolo hai.Neno linaandaliwa.wachungaji wengi NI wachivu kwa kazi na mishe tu.anakunguta bible.ujumbe anapatia madhabahuni

KAZI ya Mungu zinafanywa Kwa Ulegevu na watu wasio na karama.

Mtu Hana karama ya uhubiri unampaje ahubiri, huoni atakera watu??
 
Ukiingia nyumba za ibada sku hizi kelele za mziki unaopigwa hapo hata bar huwez zisikia. Kwaya za sku hizi hata sio bongo fleva ni bolingo na zile za twanga pepeta.
Kwa sisi makanisa ambayo tunakuwa na vitabu sku hizi hata uspoenda navyo sawa tuu.
Mimi binafsi Nabarikiwa sana na nyimbo za kitabuni rather than miziki wanayoita kwaya, hasa kipindi hiki tunachoendea cha majilio, kuna nyimbo nzuri ambazo kwa mwaka tunaimba mara moja.

I miss old days.. when..

Ogopa kitu inaitwa Karama
 
Mafundisho yanayofundishwa ni manyonge, na mengine yamejaa ulaghai na hadaa kwa wenye shida na uhitaji. Sasa kuna maana gani kwenda kusomea theolojia? Ni kuja kudanganya na kupumbaza watu? Wengine wanataka kujaza watu tu ili kutunisha fuko la sadaka na michango huku wakirudi wakavu majumbani mwao bila kupata mahubiri yenye upako wa Mungu

KAZI ya Mungu inahitaji watu wenye akili za juu, ili ifanywe Kwa weledi na sio Ulegevu
 
Kanisani kifupi sio sehemu ya burudani Ni sehemu ya kumwabudu Mungu

Mbinguni hakuna mahubiri lakini walioko kuke huabudu Mungu usiku na mchana bila kuwepo mahubiri

Ibada yaweza kuanzia Mwanzo Hadi mwisho bila mahubiri watu wakamwimbia Mungu kumsifu ,wakamsujudia,wakamuomba wakaondoka zao
 
Unataka kusema Mbinguni pamezubaa??
 
Mafundisho yanayofundishwa ni manyonge, na mengine yamejaa ulaghai na hadaa kwa wenye shida na uhitaji. Sasa kuna maana gani kwenda kusomea theolojia? Ni kuja kudanganya na kupumbaza watu? Wengine wanataka kujaza watu tu ili kutunisha fuko la sadaka na michango huku wakirudi wakavu majumbani mwao bila kupata mahubiri yenye upako wa Mungu
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu inayoadhimishwa Jumapili ya 34 ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa. Waamini tunaalikwa kuendelea kuwa ni mashuhuda wa Ufalme wa Mungu unaosimikwa katika Ukweli, Uzima, Utakatifu, Neema, Haki, Mapendo na Amani

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom