Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Kwa ushauri nchimbi ongeza ulinzi nakumbuka JK alikuita kwake nahisi huko ndiko alishinikizwa ujiuzulu ili wapachike mtu wao hapo tutekemee mwigulu chemba kuwa makamu afu waziri mkuu atapewa mtoto wa jakaya
 
Umeunganisha doti kiintelijensia sana! Kumbuka hata ile kauli yake ya nyuma kuhusu katiba mpya ilivyoleta mtikisiko. Lazima kuna trap ilitegwa na mshkaji akaingia mzima mzima mzima.

Ukiangalia kwa jicho la tatu, utagundua kabisa kuwa mchezo ulichezwa kimkakati sana. Hakuna kiongozi wa ngazi hiyo anayeachia ngazi kirahisi hivyo nchini kwetu bila kushikwa pabaya. Security threats au hata tishio la kuchafuliwa vibaya kisiasa lazima vilikuwepo mezani, naona kabisa aliamua kupiga hesabu za haraka akaona it's not worth the fight.
Nafikiri Nchimbi mwenyewe alikuwa ameamua kujitenga nao usiniambie alikuwa hajui gravity ya kauli zake alizokuwa anatoa mara kwa mara. Alikuwa na option ya kukaa kimya na akaendelea kula mema ya nchi, hivyo ni dhahiri alijua nini kinafuata na alijiandaa kwa hilo.
 
Naombeni ufafanuzi baada ya hili, utaratibu wa kumpata Makamu wa Rais mwingine upoje?

WanaCCM tufikirieni Watanganyika, msituumize kwa Maslahi binafsi mnapoenda kuchagua Makamu wa Rais mwingine.

Binafsi machungu ya October 2025 hayajaisha mpaka leo sasa msizidi kutuumiza.

Hakuna mtu wa kukufikiria mkuu.
 
Nguvu ya Rais ni kubwa Mkuu.
Kauli yake ni amri.

Huwezi shindana naye kwa waziwazi labda kama umeamua kushindwa.
Kauli ya Raisi nchi nyingine ni tafsiri ya "utii wa sheria" lakini kwa Tanzania neno "Raisi" tafsiri yake ni power isiyokuwa na ukomo wa kimamlaka.

Makamu wa Rais ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kwa kura, hivyo Raisi hana mamlaka kisheria ya kumshinikiza ajiuzulu.

Marekani ambapo tunakubali kwamba Trump ndiye Raisi powerful pengine kuliko wote, lakini bado hana mamlaka kisheria kumshinikiza makamu wake ajiuzulu.

Mchakato wa Makamu wa Raisi kujizulu huanzia bungeni na kuhitimishwa kwenye Baraza la Maseneta.

Huku kwetu Raisi anaweza kukushinikiza akijua kuwa ukijidai kukataa kwa kusimamia sheria, ataenda kwa familia yako.

Au laa anaweza kuweka mikakati ya hata kukuua.

Sasa hiyo ni abusing of power, sidhani kama hata inastahili kuiita "nguvu ya Raisi"
 
Back
Top Bottom