Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Lowasa alipotaka kujiuzulu alisoma hotuba,
Kwa rank ya makamu wa rais barua pekee yake inaweza kuwa kweli kaamua kujiuzulu au kuna watu wameandika barua wake, huku akiwa chini ya ulinzi wa wasiojulikana kwa raia?
 
Umeunganisha doti kiintelijensia sana! Kumbuka hata ile kauli yake ya nyuma kuhusu katiba mpya ilivyoleta mtikisiko. Lazima kuna trap ilitegwa na mshkaji akaingia mzima mzima mzima.

Ukiangalia kwa jicho la tatu, utagundua kabisa kuwa mchezo ulichezwa kimkakati sana. Hakuna kiongozi wa ngazi hiyo anayeachia ngazi kirahisi hivyo nchini kwetu bila kushikwa pabaya. Security threats au hata tishio la kuchafuliwa vibaya kisiasa lazima vilikuwepo mezani, naona kabisa aliamua kupiga hesabu za haraka akaona it's not worth the fight.
Na hapo ukianza kurudi nyuma kuunga dots kupitia wale mercenaries kule Bungeni walikuwa wakimuita Yuda.

Hapo unaweza kupata pattern kuwa those actions were a ticking bomb.
 
Simlikuwa mnamjaza humu kwamba ni kachero mbobevu hashindwi kitu now imekuwaje Tena !? 😆😆😆😆😆

Ila samuya licha ya madudu yake mazito it seems like she's scary more than a lion

Wana muogopa mnooo

Hahaaa nacheka kama mazuri
Sio Samia, ni wale walioko nyuma yake ndiyo wanatisha

Kuna uwezekano 2030 tukapata Rais kutoka Jimbo la Chalinze
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 50(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa nafasi ya Makamu wa Rais itakuwa wazi kutokana na kifo au kujiuzulu, utaratibu ni huu:

  • Makamu wa Rais anajiuzulu → nafasi yake inakuwa wazi.
  • Rais anamteua mtu mwingine kuwa Makamu wa Rais.
  • Uteuzi huo unatakiwa kufanyika mapema iwezekanavyo na, kwa mujibu wa Ibara ya 50(4), ndani ya siku zisizozidi 14 tangu nafasi hiyo iwe wazi.
  • Mtu huyo mpya lazima athibitishwe na Bunge kwa kura za Wabunge walio wengi.
  • Baada ya kuthibitishwa na Bunge, anaapa na kuanza rasmi kutekeleza majukumu ya Makamu wa Rais.
 
Naombeni ufafanuzi baada ya hili, utaratibu wa kumpata Makamu wa Rais mwingine upoje?

WanaCCM tufikirieni Watanganyika, msituumize kwa Maslahi binafsi mnapoenda kuchagua Makamu wa Rais mwingine.

Binafsi machungu ya October 2025 hayajaisha mpaka leo sasa msizidi kutuumiza.
kunywa brufen tu upooze maumivu mumy wana ccm hata hawawezi kusikia kilio chako
 
Huu ushauri wako ni mzuri natamani, sijapata platform wapi na weza kujifunza guitar especially Base Guitar
Ahaa Kidogo Mimi nilianza kwq kununua Acoustic kisha Electrical guitar baadae...ni mtu wa kanisani muda mwingi nahudhuria ibada zote nikajiunga na Team na kwaya kadhaa huku nikijfunza zaidi mpaka ikawa ndo maisha kila mara unaitwa kufanya sehemu mpaka sasa harusi dinner binafsi za watu nk

kama una pesa ya ziada nunua Bass Guitar na Combo yake
ingia youtube pata basic knowledge baada ya hapo ulimwengu wa mziki utakuvuta tu
 
Kwenye sayansi ya siasa hii ni 1 ya njia ambayo hutumika.. [if you not fight them join them] hapo kunamtu anatafutwa kwa manati akijaa tu kwenye mfumo watu wanakula kichwa...

Rudi nyuma kwa edo, slow na waleeeee.. chuo kipo pale kibaha.. naona na majirani wameanza kuisoma siasa yetu ni kama wanaona inalipa saannaa..
 
Back
Top Bottom