TheUchungu
Member
- Jan 17, 2010
- 21
- 0
Huu ni uamuzi mzuri alochukua kijana mwenzetu ingawa unakumbwa na maswali kutokana na kwamba yumo katika mfumo wa siasa ambao una "circles" zilizo na mtizamo wa kupata umaarufu na baadae kukusanya mali halafu mwisho kustaafu ukiwa hujafanya chochote kwa wananchi wako.
Tumeliona hilo kwa mgosi anaeshikilia kiti mzee Shelukindo na ushauri wangu wa bure kwa mgosi mwenzangu Januari ni kwamba endapo atapitishwa na wananchi na kuwa mbunge mpya wa Bumbuli basi awe na ofisi jimboni humo na awe anaishi Bumbuli na awe akienda Dodoma kwa shughuli za Bunge tu.
Kwa kufanya hivyo atakuwa karibu na wananchi na kufanya mambo yote ya maendeleo anayoyasema yeye akiwamo.
Nani kakuambia Januari ni Mgosi??? soma historia yake vizuri utajua....ni Mhaya kutoka kwa mama yake na hajawahi hata kuishi huko bumbuli..alipofika Bumbuli wazee walimshauri kama unavyomshauri wewe awe na makazi jimboni, alishauriwa anunue kiwanja na ajenge lakini akaleta usanii mpaka leo hajasema lolote...watu washamuona ni msanii na aliyetuma na kundi fulani...