Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MtazamoWangu, Jul 3, 2010.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hali imekuwa ngumu upande wa Mzee Makamba baada ya wananchi wa Bumbuli kumkataa mwanae Januari Makamba na kumuunga mkono mtu mwingine katika nafasi ya ubunge.
  Mzee Makamba amepagawishwa na taarifa alizopatiwa na watu wake wakaribu jimboni kwamba hali ni ngumu na wananchi wengi wamekuwa wakimuunga mkono kijana Abdulkadir, wanafunzi wengi wa vyuo waliopo jimboni wamekuwa wakimtangaza bwana Abdulkadir na kikao cha wananchi wa jimbo la bumbuli wanaoihsi DSM kukutana na kutoa tamko la kumuunga mkono Abdulkadir kuwa ndio anayefaa kugombea nafasi hiyo, habari hizi zimekuwa ni mwiba kwa familia ya Makamba ambapo wiki iliyopita tulimuona mama yake mzazi Januari akienda jimboni na kuonana na wanawake, alifanya sherehe na kuchinga ngome na kuwaalika wanawake wengi kutoka maeneo mbalimbali jimboni, mbali na kuwaambia wanawake hao wamuunge mkono kijana wake, aliwapatia kila mmoja khanga na fedha taslimu shilingi 10,000, Huyu mama aliwaambia wananchi yeye atakufa na mtu mwaka huu na yupo tayari afilisike kuliko mwanae ashindwe...
  Leo mzee makamba ameingia jimboni akitokea dodoma na kuitisha kikao nyumbani kwake kilichohudhuriwa na watu zaidi ya 30, katika kikao hicho Mzee Makamba alimshambulia kijana Abdulkadir na kuwaambia watu kuwa kijana huyo ni mzururaji huko mjini na hana kazi wala nyumba ya kuishi na hawafai acheni kudanganywa...alikuwa pia amefuatana vijana wawili ambao alisema walikuwa kwenye kambi ya Abdulkadir na kuamua kujitoa..(ilibainika kwamba si kweli bali ni kuwahadaa wananchi vijana hao hawako kwa Abdulkadir), baada ya Mzee makamba kuwalaumu sana watu wake kwa kuacha Abdulkadir anakubalika zaidi ya mwanae,aliahidi kutoleta msaada wowote kama hawatamuunga mkono.
  mwisho wa kikao wajumbe walikabidhiwa kila mmoja shilingi 2000 na viongozo kupatiwa 5000.

  My take: Kwa namna hii je CCM itaweza kupambana na rushwa kwenye siasa?
  je wagombea wengine watatendewa haki kiasi gani kwenye mchakato ikiwa Januari ni mtoto wa katibu mkuu wa chama na anafanyiwa kampeni na viongozi wa chama?

  sisi tuliokuwepo huku jimboni tunaona yanayotokea huku na tunasubir tuone mamuzi ya chama kabla ya uchaguzi.....
  mpaka sasa bado inaonekana mchuano mkali utakuwa baina ya Januari Makamba na Abdulkadir kaniki kwani hakuna mtu anayemtaja tena Mzee Shelukindo


  taarifa zinasema Januari Makamba atakuwepo jimboni mwishoni mwa wiki ijayo baada ya mama yake na baba yake kupita kusafisha njia.....


  reporter wako;
  Bumbuli TV
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa CCM wanapenda sana kuwaacha wanachi wawe wategemezi wa misaada badala ya kuwaongoza wananchi ili wajitegemee. Huu utegemezi wa misaada ndio unaoiponza nchi hii. Siamini kabisa kuwa Makamba, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama chake anatumia misaada kama silaha ya kisiasa. Inaonyesha kuwa serikali ya chama cha CCM anachokiongoza, ambayo inategemea sana misaada kutoka nchi za nje, iko pale pia kutekeleza matakwa ya watoa misaada ile hata kama haikubaliani na matakwa hayo; hiyo siyo serikali ya wananchi.

  Nyerere alitaka kujenga taifa la kijamaa na lenye kujitegemea. Ingawa siasa ya ujamaa haikuwa sahihi sana kwa vile ilitegema zaidi mazingira yaliyokuwapo, siasa ya kujitegemea bado ni sahihi na itaendelea kuwa sahihi karne zote zijazo katika nchi yoyote duniani.
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapo ndo unapoona ni kwa kiasi gani sheria ya uchaguzi ilivyotungwa purposely kwa ajili ya wapinzani na si CCM. Kama CCM yenyewe ndo iliyokuja na wazo la sheria ya kuzuia aina yoyote ya rushwa katika uchaguzi, leo hii ndo inaongoza kwa kutoa rushwa, ina maana haikujua kwamba sheria hiyo itakuwa mwiba kwake? Hapo ndo ninapoona kwamba ilitungwa purposely kwa ajili ya kuwabana wapinzani. Na haikuwa na lolote la kufanya kwa ajili ya uchuguzi kwa ujumla. Halafu kingine, muda wa kampeni haujaanza, hiki kinachoendelea hivi sasa ni nini? Katika hali hii pia sisiti kuwashangaa wapinzani kwa kutokuanza na wenyewe kuuza watu wao ili kuweka usawa.
  Naamini wapinzani watakuwa wamenote hoja hii na kufuatilia ushahidi wake, ili ikiwezekana hatua mhimu zichukuliwe. Lakini ambacho kinaboa Tanzania ni kwamba hata kama wapinzani watanote hilo, watalipeleka wapi? Polisi wapo kwa ajili ya kuilinda CCM, jeshi kwa ajili ya CCM na mahakama ni kwa ajili ya kuilinda CCM. Sasa hao upinzani watampelekea nani kesi hiyo? Hii nchi ina safari ndefu sana kupitia ukombozi wake wa dhati.
  Tulipata uhuru kutoka kwa Waingereza lakini sasa tunahitaji watu makini watusaidie kutafuta uhuru kutoka kwa mkoloni CCM.
   
 4. p

  pareto 8020 Member

  #4
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How outhentic is this information? Mbona the whole of last week, huyo Mama alikuwa Johanesburg...imewezekanaje akawepo Jbg na Bumbulu at the same time? Sina uhakika na hiyo mikutano mingine unayoongelea, lakini kwa huo wa Mama ni UONGO..nathibitisha hilo... Again, inanifanya nitilie mashaka na the rest of the story.. Hebu tupatie uthibitisho wa watu unaowaongelea na vikao unavyoripoti ni sahihi..
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Makamba na mkewe washtakiwe kwa kutoa rushwa.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi hakuna wa kumshtaki Makamba maana CCM ndiyo imeshika utamu na hiyo NEC ni kitengo cha CCM wanaona kabisa rushwa nje nje katika majimbo mengi lakini kimyaaaaa! kama hawapo vile. Inauma sana kuona watu wanunua KULA kwa kutoa rushwa mchana kweupe na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao. Hata kura wataiba ili kuhakikisha January analitwaa jimbo 2010.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mimi nilidhani kama mmegutuka wenzangu kwanini Ridhiwani Kikwete na kundi lake wameongoza mapambano ya kumn'goa Masauni na baba yake akabariki, jibu limeshapatikana...fomu ya wadhamini na UVCCM walitakiwa wairandishe kwa fedha ya chama (tofauti na Kikwete na Makamba wanavyodai kuwa suala la kurandisha fomu ni lake binafsi na si la chama) Masauni hakuwa tayari kutumia rasilimali za UVCCM kurandisha kwa mpango huo wa mgombea na kwa taasisi hiyo kutumika, huku ikiwa haijuulikani kama mgombea mwengine atakayejitokeza kupambana na Kikwete atarandishiwa na nani fomu yake(wakati huo Shibuda hajatangaza kujitowa).

  Ukiangalia walioshiriki kuvuja jasho kurandisha fomu ya Kikwete ni Ridhiwani na Malissa anayekaimu kiti hicho (kama Masauni angekubali ingekuwa yeye) na karibu UVCCM yote ilipata mgongo wao.
  ANGALIZO: tusije kushangaa CCM kutumia mbinu hizo hizo kumtoa Mzee Shelukindo na "kumpotezea" kijana wa watu Abdulkadir, Makamba anatengeneza pensheni yake vizuri na kimkakati zaidi.
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Alitaka kujenga kujitegemea, then what happened? Nani akamzuia?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nani alitegemea CCm isiyo na rushwa?? tuache kudanganyana.... rushwa na CCM ni sawa na vumbi na stoo. hakuna mwana CCM kiongozi asiyetoa wa la kupokea rushwa

  ACTUALLY RUSHWA NA SIASA NI SYNONYMOUS [kwa vyama vyote tu!!!]
   
 10. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  inaonyesha unamfahamu kumbe basi kwa taarifa yako Mama yake januari alikuwepo Mahezangulu kuanzia wiki mbili zililozipita, alifanya mikutano pale na mikutano mingine alipanga ifanyike magoma bahati takukuru walipata taarifa na kuhamishia kikao nyumbani kwao, laifanya vikao vingnie kata ya soni ambapo aliwapatia kinamama pesa na khanga....vikao vingine vilikuwepo kata ya Vuga....na kama huamini mzee makamba bado yupo kule toka jana mtafute....
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hawa watoto wa viongozi watashikwa mikono mpaka lini? hata kama ni vilaza vipi. Hawawezi kutafuta njia zao wenyewe mpaka wategemee baba zao. Inakera ka nini vile. Halafu litasimama mbele za watu na kujidai. Hovyooooooooooooooooooooooooooo
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  With that situation then Abdulakadir can declare himself a winner......May god Bless him....
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
 14. A

  August JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  mnaweza tupatia cv ya Abdulkadir?
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama hakuna wa kumshitaki basi aongeze hilo dau analotoa... buku mbili ni kama anatania
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Very important question,

  As much as I don't like January and all his drunken entitlements, arrogance and sense of sultanate these political dynasties are creating, I woul d really like to know about the alternative.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  ..........swali la kitoto kweli hili.

  Yaani kweli una akili timamu unapojenga hoja dhaifu kudai kuwa kwa vile Nyerere hakufanikiwa kujenga taifa la kujitegemea miaka takribani 30 iliyopita basi hiyo iwe ni warrant ya kujenga jamii inayotegemea misaada karne hii?
   
 18. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hahaha! hilo la elfu 2 hata mimi limenichekesha si afadhali hata mama alietoa kumi kumi.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  DD, huwezi kujua labda huo ni mgao wa kwanza. Akiona hali kwa mwanae bado ni ngumu basi anaweza kupitisha mgao mwingine au mingine.

   
 20. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Januari Makama aliaandaa dinner moja pale Colar Beach na kuwwalika baadhi ya watu ili kuomba michango, na baadhi ya watu wakubwa waliohudhuria ni Rostam Aziz, Yusuph manji ambao walimchangia pesa za kampeni baada ya kufanya presentation ya kuonyesha matatizo ya jimbo bumbuli....pamoja na kushindwa kujibu baadhi ya maswali na kuonyesha uelewa wake wa jimo hilo na upinzani unaomkabili, alijikweza na ukudai kwamba anakubalika sana na itakuwa rahisi kwake kushinda.....
  Natumaini wahusika wataliona hili maana katika mabo sheria mpya ya uchaguzi inayogusa ni hii michango wanaopat wagombea, wanatakiwa watoe taarifa na pia kuonyesha matumizi yake....
   
Loading...