Msibani imesemwa Hayati Lowassa alikuwemo JWTZ hadi Ukapteni na akashiriki vita vya Uganda. 2015 mzee Makamba alisema Lowassa hakwenda jeshini

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400

View: https://www.youtube.com/watch?v=SH9ks-0_wQ8

Mimi ni mmoja wa watu tulobahatika kuhudhuria msiba wa marehemu Edward Ngoyai Lowassa na nikawa na shauku kubwa ya kusikia historia ya mwanasiasa huyu.

Bila shaka protokali ya msiba haikukosa kuwa na kasehemu ka kueleza wasifu wa mzee huyu ili wengine kama mimi tulokuwa hatufahamu uzuri historia ya mzee huyu tungepewa fursa ya kufahamu historia hiyo.

Mwelezaji akaingia na wasifu wa marehemu Lowasa na kwa hakika historia hiyo ilikuwa imetayarishwa kwa umakini huku ikiwa imepangwa kwa üstadı katika sehemu ndogondogo kama vile elimu yake, kazi zake kama mwanasiasa, ubunge, utumishi wake wa jeshi la wananchi wa Tanzania, uwaziri wake na uwaziri mkuu.

Pia tuliambiwa kuwa Marehemu Lowasa amewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama cha mapinduzi kama za ukatibu mikoa na hata ndani ya sekretarieti.

Lakini ni sehemu ya utumishi wake ndani ya jeshi letu la wananchi wa Tanzania ambayo ilinifanya nisikilize kwa umakini.

Kwanza katika sehemu hii tulielezwa kwamba kati ya mwaka 1973-1974 marehemu Lowasa alitumikia Jeshi la kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria na hiyo ilikuwa ni kabla hajajiunga na masomo ya chuo kikuu baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita.

Kisha mwelezaji wetu akatuambia waombolezaji kuwa kati ya mwaka 1978 na 1980, marehemu Edward Lowasa aliwahi kutumikia jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha ukapteni huku akiongoza brigedi na pia akashiriki vita vya Uganda. Pia yaonyesha kwamba alikuwemo ndani ya jeshi kwa muda kidogo kama miaka miwili hivi.

Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 17 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.

Kupigiwa mizinga 17 na shughuli nzima kufanywa na JWTZ si tukio geni, lakini ni kutokana na mazungumzo na mijadala mbalimbali juu ya historia ya kiongozi huyu khasa na baadhi ya wanasiasa wengine na ambao pamoja nao walikuwa na urafiki na ukaribu mkubwa na marehemu.

Sasa basi, nikajaribu kudadisi kumbukumbu zangu na nikatua kwenye kampeni za kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 ambapo kampeni zilikuwa zikipita sehemu mbalimbali hapa nchini.

Lakini katika kampeni zake huko Morogoro CCM ikiwa imempitisha mgombea wao hayati John Magufuli, mzee Yusufu Makamba alipewa nafasi ya kueleza machache kabla hajampisha mgombea wa CCM Magufuli.

Ni katika maelezo yake ambayo yamo katika video ya Youtube, mzee Yusuf Makamba (kuanzia dakika ya 15) alidai kuwa marehemu Edward Lowasa alikuwa mwongo na alidanganya kwa kusema kwamba alikwenda jeshini na alipigana vita vya Uganda.

Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusikia wasifu ule mimi nikachukua "note book" yangu na nikaandika hii mada ili nije niwaletee hapa wakuu wa JF tuijadili.

Je, pale wanasiasa wanapoamua kuwaghilibu wananchi kwa minajili tu ya kutaka kura je, ni lazima binadamu wenzetu tuwashuhudie uongo hata ikiwa ni kwa gharama zozote?
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=SH9ks-0_wQ8

Mimi ni mmoja wa watu tulobahatika kuhudhuria msiba wa marehemu Edward Ngoyai Lowasa na nikawa na shauku kubwa ya kusikia historia ya mwanasiasa huyu.

Bila shaka protokali ya msiba haikukosa kuwa na kasehemu ka kueleza wasifu wa mzee huyu ili wengine kama mimi tulokuwa hatufahamu uzuri historia ya mzee huyu tungepewa fursa ya kufahamu historia hiyo.

Mwelezaji akaingia na wasifu wa marehemu Lowasa na kwa hakika historia hiyo ilikuwa imetayarishwa kwa umakini huku ikiwa imepangwa kwa katika sehemu ndogondogo kama vile elimu yake, kazi zake kama mwanasiasa, ubunge, utumishi wake wa jeshi la wananchi wa Tanzania, uwaziri wake na uwaziri mkuu.

Pia tuliambiwa kuwa Marehemu Lowasa amewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama cha mapinduzi kama za ukatibu mikoa na hata ndani ya sekretarieti.

Lakini ni sehemu ya utumishi wake ndani ya jeshi letu la wananchi wa Tanzania ambayo ilinifanya nisikilize kwa umakini.

Kwanza katika sehemu hii tulielezwa kwamba kati ya mwaka 1973-1974 marehemu Lowasa alihuduhuria Jeshi la kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria na hiyo ilikuwa ni kabla hajajiunga na maosmo ya chuo kikuu baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita.

Kisha mwelezaji wetu akatuambia waombolezaji kuwa kati ya mwaka 1978 na 1980, marehemu Edward Lowasa aliwahi kutumikia jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha ukapteni huku akiongoza brigedi na pia akashiriki vita vya Uganda.

Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 21 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.

Kupigiwa mizinga 21 na shughuli nzima kufanywa na JWTZ si tukio geni, lakini ni kutokana na mazungumzo na mijadala mbalimbali juu ya historia ya kiongozi huyu khasa na baadhi ya wanasiasa wengine na ambao pamoja nao walikuwa na urafiki na ukaribu mkubwa na marehemu.

Sasa basi, nikajaribu kudadisi kumbukumbu zangu na nikatua kwenye kampeni za kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kampeni zilikuwa zikipita sehemu mbalimbali hapa nchini.

Lakini katika kampeni zake huko Morogoro CCM ikiwa imempitisha mgombea wao hayati John Magufuli, mzee Yusufu Makamba alipewa nafasi ya kueleza machache kabla hajampisha mgombea wa CCM Magufuli.

Ni katika maelezo yake ambayo yao katika video ya Youtube, mzee Yusuf Makamba (kuanzia dakika ya 15) alidai kuwa marehemu Edward Lowasa alikuwa mwongo na alidanganya kwa kusema kwamba alikwenda jeshini na alipigana vita vya Uganda.

Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusikia wasifu ule mimi nikachukua "note book" yangu na nikaandika hii mada ili nije niwaletee hapa wakuu wa JF tuijadili.

Je, pale wanasiasa wanapoamua kuwaghilibu wananchi kwa minajili tu ya kutaka kura je, ni lazima binadamu wenzetu tuwashuhudie uwongo hata ikiwa ni kwa gharama zozote?

Pia umesahau kusema Lowasa hakuwahi kugombea urais kupitia Chadema, historia za Tanzania zimejaa uongo, je Tanzania iliwahi kuwa koloni la mwingereza?
 
Ni kweli mwelezeaji aliongelea hilo la marehemu Lowasa kugombea uraisi kupitia Chadema.

Nimefupisha mada ila wasifu umeeelezea kazi nyingi alozifanya marehemu Lowasa ikiwemo ukurugenzi wa AICC.

Lakini kusudio la mada ni kuonyesha namna michezo ya siasa inavyofanyika ikiwemo kusema uongo.
 
Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 21 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.
Haikupigwa mizinga 21 imepigwa mizinga 17 na hiyo ni heshima alipewa kama mtu aliyewahi kushika nafasi ya waziri mkuu akiwa ni mmoja wa viongozi wenye hadhi ya kufanyiwa mazishi ya kitaifa.
 
Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.
Ameniacha hoi
Wanamtuhumu lakini hawakumchukulia hatua za kisheria, kama ni mwizi kwanini waliendelea kumfuga kwenye chama?
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=SH9ks-0_wQ8

Mimi ni mmoja wa watu tuliobahatika kuhudhuria msiba wa marehemu Edward Ngoyai Lowassa na nikawa na shauku kubwa ya kusikia historia ya mwanasiasa huyu.

Bila shaka protokali ya msiba haikukosa kuwa na kasehemu ka kueleza wasifu wa mzee huyu ili wengine kama mimi tulokuwa hatufahamu uzuri historia ya mzee huyu tungepewa fursa ya kufahamu historia hiyo.

Mwelezaji akaingia na wasifu wa marehemu Lowasa na kwa hakika historia hiyo ilikuwa imetayarishwa kwa umakini huku ikiwa imepangwa kwa üstadı katika sehemu ndogondogo kama vile elimu yake, kazi zake kama mwanasiasa, ubunge, utumishi wake wa jeshi la wananchi wa Tanzania, uwaziri wake na uwaziri mkuu.

Pia tuliambiwa kuwa Marehemu Lowasa amewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama cha mapinduzi kama za ukatibu mikoa na hata ndani ya sekretarieti.

Lakini ni sehemu ya utumishi wake ndani ya jeshi letu la wananchi wa Tanzania ambayo ilinifanya nisikilize kwa umakini.

Kwanza katika sehemu hii tulielezwa kwamba kati ya mwaka 1973-1974 marehemu Lowasa alitumikia Jeshi la kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria na hiyo ilikuwa ni kabla hajajiunga na maosmo ya chuo kikuu baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita.

Kisha mwelezaji wetu akatuambia waombolezaji kuwa kati ya mwaka 1978 na 1980, marehemu Edward Lowasa aliwahi kutumikia jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha ukapteni huku akiongoza brigedi na pia akashiriki vita vya Uganda. Pia yaonyesha kwamba alikuwemo ndani ya jeshi kwa muda kidogo kama miaka miwili hivi.

Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 21 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.

Kupigiwa mizinga 21 na shughuli nzima kufanywa na JWTZ si tukio geni, lakini ni kutokana na mazungumzo na mijadala mbalimbali juu ya historia ya kiongozi huyu khasa na baadhi ya wanasiasa wengine na ambao pamoja nao walikuwa na urafiki na ukaribu mkubwa na marehemu.

Sasa basi, nikajaribu kudadisi kumbukumbu zangu na nikatua kwenye kampeni za kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kampeni zilikuwa zikipita sehemu mbalimbali hapa nchini.

Lakini katika kampeni zake huko Morogoro CCM ikiwa imempitisha mgombea wao hayati John Magufuli, mzee Yusufu Makamba alipewa nafasi ya kueleza machache kabla hajampisha mgombea wa CCM Magufuli.

Ni katika maelezo yake ambayo yao katika video ya Youtube, mzee Yusuf Makamba (kuanzia dakika ya 15) alidai kuwa marehemu Edward Lowasa alikuwa mwongo na alidanganya kwa kusema kwamba alikwenda jeshini na alipigana vita vya Uganda.

Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusikia wasifu ule mimi nikachukua "note book" yangu na nikaandika hii mada ili nije niwaletee hapa wakuu wa JF tuijadili.

Je, pale wanasiasa wanapoamua kuwaghilibu wananchi kwa minajili tu ya kutaka kura je, ni lazima binadamu wenzetu tuwashuhudie uongo hata ikiwa ni kwa gharama zozote?

Alipigiwa mizinga 17
 
Back
Top Bottom