Mbunge Dorothy George Kilave afanya kikao na viongozi wa vyama vya siasa Temeke

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
03/08/2023. JIMBONI.

Mhe. Dorothy George Kilave Mbunge wa Jimbo la Temeke, amekutana na kuzungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa Temeke. Kikao cha Kuwasilisha Taarifa ya Maendeleo na Kupokea Maoni na Ushauri Kwa Maendeleo Jimboni.

Kikao kimehusisha Viongozi wa Vyama Vya Siasa wakiongozwa na Viongozi wa CCM Wilaya ya Temeke. Katika Kikao Hiki, Ndugu George Daniel Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke amesema kuwa Baraka za kikao zimetolewa na Chama cha Mapinduzi CCM, Baada ya Mhe Mbunge Kutoa Taarifa ya Kukaa na Viongozi wa Vyama Vingine Vya Siasa kwani Chama na Serikali Vinatambua Umuhimu wa Vyama Vingine Vya Siasa Kwa Maendeleo ya Wananchi.

Mhe Dorothy George Kilave Mbunge, Amesema kuwa hatopuuza wala kutokuzingatia Ushauri na Maoni ya Viongozi wa Vyama Vya Siasa Katika Utekelezaji wa Majukumu yake ya Kibunge, Kwani, Viongozi wa Vyama Vya Siasa ni Muhimu Sana kwasababu wamebeba Sauti za Wananchi Jimboni.

Pia, Mhe Mbunge Ameahidi kuwa, ataendelea Kupiga kazi Kwa Uaminifu na kwakuzigatia Wajibu wake, Kuwawakilisha Wananchi katika Serikali, ili iendelee kuleta Maendeleo Jimboni.

Vyama vilivyohudhuria: NCCR MAGEUZI, DIRA MAKINI, AAFP, UDP, UMD, TLP, ADC, CCK, NLD, SAU, CHADEMA, CUF, ACT.

Mwisho Mbunge huyo akishirikiana na Viongozi Wote Wa Vyama Vya Siasa Temeke wameahidi kumuunga Mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa Kazi Kubwa na Nzuri anayoifanya katika kuwaletea Maendeleo Watanzania.
 
Back
Top Bottom