Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
- Thread starter
- #1,221
Na miye niweke 50 cents zangu.
Alichoandika Bw. Said kwenye simulizi la kila ambacho anakiita "historia" kwa kweli siyo historia kwa maana ambayo inakubalika. Ndio maana toka mwanzo wa mnakasha huu nimekuwa nikiuliza maswali ambayo yanahusiana na ukusanyaji wa taarifa mbalimbali. Napenda zaidi maana ya neno "history" inavyotolewa kwenye wikipedia - History (from Greek ἱστορία - historia, meaning "inquiry, knowledge acquired by investigation"[SUP][2][/SUP]) is the discovery, collection, organization, and presentation of information about past events. History can also mean the period of time after writing was invented.
Kamuni ya "The Pocket Webster School & Office Dictionary" inasema kuwa "history" ni a. A narration or description of facts and events arranged chronologically with their causes and effects. b. A knowledge of facts c. all of the known past and d. A scientific study of the past.
Kumbe historia siyo simulizi kama hadithi. La hasha! Historia ni somo linaloongowa na kanuni za kisayansi na kanuni ya kwanza kabisa ni kuwa objective. Manake nini? Maana yake ni kwamba unapoenda kuangalia matukio ya nyuma unakuwa huru kutoka katika biases zako, stereotypes zako na kwa hakika kabisa kuzigundua hivyo vikwazo vya kuwa objective. Hapa ndipo tunapokutana na kosa kuu kabisa la mzee wetu.
Bw. Said hakuisogelea historia katika mwanga wa mtu ambaye ni objective. Alisimuliwa maneno na wazazi wake, aliyaona mambo kadha wa kadha akiwa na umri mdogo, na kwa bahati mbaya sana alikulia na kufundishwa chini ya wale ambao waliamini kabisa kuwa Nyerere alikuwa ni mdini toka siku ya kwanza anaingia Dar. Hivyo anapokua na kupata Ilimu tayari ameshajengewa hisia hii kutokana na masimulizi mbalimbali. Mara kwa mara hurudia kutuambia jinsi alivyosimuliwa na "wazee" wake. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.
Kosa lake la pili mzee wetu ni kuwa alipoanza kufanya utafiti hakuwa anafanya utafiti ili kuwathibitisha wazee wake au kuwakanusha. Hakuwa anafanya utafiti ili kujua ukweli wote kabla ya kujenga maoni yake. Badala yake yeye alienda kuangalia historia ili kuthibitisha kile ambacho alishaaminishwa tangu akiwa kijana mdogo hadi leo hii. Hivyo, chochote ambacho angekutana nacho kinyume na kile alichosimuliwa alikiweka pembeni. Na matokeo yake ni kuwa simulizi zima halihusiani na historia hata kidogo linahusiana na MAJINA YA WAISLAMU.
Umenisoma vizuri.
Bw. Said kwa kweli hajali kabisa kama hao wanaoitwa "waislamu" wa wakati ule walikuwa kweli wanashika dini au wanaitwa tu kwa majina. Hilo kwake si hoja hata kidogo. Alipofanya utafiti alipoona jina la Kiislamu alihitimisha ni "MUislamu" na hivyo hata kama watu hao kihistoria walikuwa hawashiki dini au hata kufuata imani ilivyo yeye kwake haikuwa hoja alimradi tu wale walijiita "Waislamu" sasa hiki ukiangalia ni kigezo kidogo sana kukifikia. Nguruvi ameonesha mahali fulani hapa - kwamba Bw. Said anatumia majina ya Waislamu kuwapa watu "Uislamu" lakini ikija kwenye BAKWATA au mtu mwingine yeyote anayempinga ambaye anajina la Kiislamu kipimo chake hicho hukitupa mbali. Anaingiza kipimo kingine kabisa nacho ni "kukubaliana nasi". Yaani, Muislamu ambaye anaampinga si Muislamu ila yule wanayekubaliana naye. Matokeo yake kwake BAKWATA haiwezi kuwakilisha maslahi ya Waislamu kwa sababu hata kama wote waliomo mle wanaamini katika Uislamu; wanamuamini Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na Mshirika na wanaamini kuwa ni Mtume Mohammed (SAW) ni mjumbe wake.
Hili linashangaza. Hakuna kipimo chochote kingine cha Muislamu zaidi ya imani yake katika mambo haya mawili ya msingi na mengine yanayotokana na hayo. Hakuna siasa, hakuna rangi, hakuna uanachama wa chama fulani n.k
Hata hivyo kosa la tatu ambalo linavunja kabisa hii dhana kuwa anachosimulia ni historia ni kuwa haandiki ili kuwaleta watu pamoja kuweza kufahamu ukweli . Nina bahati kuwa nimesoma maandishi yake mengi sana na katika yote yeye anazungumzia ugomvi kati ya Waislamu na Wakristu au kati ya Uislamu na Kanisa. Na katika hili kwa kweli amefanikiwa sana. Siyo kuwaamsha Waislamu bali kuwapotosha watu kuamini kuwa adui yao ni Kanisa! Hazungumzii umaskini, magonjwa na ujinga uliokithiri kati ya watu wetu - Waislamu, Wakristu na Wapagani; hazungumzii matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zinatokana na kodi za walio BAKWATA NA wale walio nje ya BAKWATA; hazungumzii haja ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yatawaleta wananchi wetu pamoja kuubomoa na kuuvunjilia mbali mfumo wa utawala wa kifisadi. Anachofanya yeye ni kuwafanya baadhi ya Waislamu - na inasikitisha wapo ambao wanamini -kuwa adui yao ni Kanisa!
Matokeo yake ni kweli wapo watu wanalichukia kanisa katoliki; wapo watu ambao wanachukia hata Wakristu kwa sababu ya mafundisho ya Bw. Mohammed. Ndio nikaonesha juzi kwamba anachofanya ni kinyume hata na mafundisho ya Qurani. Analeta faraka siyo tu kati ya Waislamu na Waislamu (wale wa BAKWATA NA WALE NJE YAKE) bali pia faraka kati ya wanadamu tulioumbwa na Mwenyezi Mungu ili "tujuane" siyo tuchikiane, tuogopane au hata tudhulumiane. Angekuwa kweli kabisa lengo lake ni kutafuta umoja na ukweli asingedai kuwa ameandika kwa ajili ya "kuwatuhumu" watu fulani.
Na hata kama angetaka kutuhumu watu basi tungeona kweli kabisa angejiunga na wengine na kuleta mashtaka Mahakamani.
Bw. SAid na wale wanaoamini kuna mfumo Kristu wangeweza kabisa kuleta hata kesi mahakamani. Kushtaki Baraza la Maaskofu Katoliki kwa kuwa wanafanya ubaguzi. Wangeweza kufungua mashtaka dhidi ya Wizara ya Elimu ili kuonesha kuwa inafanya kazi kibaguzi. Hadi leo hii hakuna kesi hata moja iliyowahi kufunguliwa dhidi ya kanisa au serikali au hata mtu yeyote mwingine kudai kuwa kuna watu wanabaguliwa. Nilimuambia mtu mmoja juzi humu humu ambaye alidai kuwa kuna ubaguzi wa kidini NSSF - nikasema kama yeye ni mwathirika leteni mashtaka.
Sitaraji kama kuna mtu yeyote upande wa Bw. Said ambaye anaweza kuleta mshtaka nchini ya kudai kuwa Waislamu wanadhulumiwa. Hakuna ushahidi unaoweza kusimama mahakamani wa jambo hilo. NONE. Wapo ambao wanapenda uwepo ushahidi ili waweze kusema "tuliwaambia" lakini kwamba kuna ushahidi unaoweza kuoneshwa wa mfumo rasmi wa kibaguzi wenye kupendelewa Wakristu (mfumo kristu) haupo.
Kwa hiyo, kwa ufupi mjadala huu unatuonesha tu hatari tuliyonayo kama taifa. Hasa uwepo wa watu ambao wanaamini yanayodaiwa bila kuuliza. Mwanahistoria wa Kiarabu aliyeishi 1337 Ibn Khaldun - ambaye anatajwa kama Baba wa Sayansi ya Historia na mmoja wanafalsafa wa hali ya juu toka katika Ulimwengu wa Kiislamu - aliandika kuhusu makosa saba ambayo waandishi wa historia wanayafanya. Lakini kwa sehemu hii itoshe kunukuu maneno yake ni kukosoa kile aliachokiita "idle superstition and uncritical acceptance of historical data" kama mojawapo ya makosa ya wanahistoria.
Tumeona humu wapo watu ambao hawataki kuuliza maswali sahihi kwa sababu majibu yake yanavunja hoja zao. Matokeo yake ni kuwa watu wanakubali bila kupatiwa uhakika na hasa vijana ambao huenda kumsikiliza nawaonea huruma kwa sababu wengi wanajikuta wanaamini kile lisemwalo kwa sababu aliyelisema anatumia authority ya kuwa amezungumza sehemu nyingi duniani, anakubalika na majarida mbalimballi duniani. For untrained minds hii ni authority tosha. It is sad that some people among "great thinkers" wako hivyo hivyo. Wanakubali kitu wanachoambiwa bila kukihoji kwa sababu tayari wanakiamini.
Kwa hiyo, tafuteni kazi za Bw. Said mzisome lakini mkae mkijua hamsomi historia bali masimulizi ya kijana kuhusu wazazi na wazee wake. Mtu anayesoma akiamini anasoma historia hatuna jinsi ya kumsaidia bali kumuonea huruma.
Mwanakijiji,
Sitanii hii ni kweli.
Katika hii "critique" yako nakiona kitabu kileeee kinakuja.
Usipuuze ushauri wangu.
Wewe una uwezo wa kuandika hebu tazama ulivyosimama na mimi "toe to toe" kama Waingereza wasemavyo unadhani ni kitu kidogo.
Matani ya nondo zote nilizokushushia hukufa bado unakuja tu.
Hilo si mchezo si unaona rafiki yako Mag3 kakimbia karudi leo anauliza hivi mnakasha bado unaendelea?
Andika kitabu unitoe makosa na dunia nzima ijue Mohamed Said kakutana na saizi yake.
Bila kitabu bado ushindi uko kwangu.
Mohamed