Majina ya Ali (Ally) Katika Historia ya Kupigani Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MAJINA YA ALI (ALLY) KATIKA HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Katika vibao hivyo vitatu kimoja kimekosekana.
Kimesosekana kibao cha Ali Masham wa Magomeni Mapipa.

Ali Masham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilifanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya viongozi wa serikali ya mtaa hawajaona umuhimu kwa kuhifadhi jina la mzalendo huyu.

Bado nasubiri kibao cha nne cha Ali Msham nikamilishe historia ya akina Ali katika historia ya TANU.

1709924968881.png
1709925010981.png

1709925045900.png

We mzee sikupingi na siwezi kuja kukuvunjia adabu mwanazuoni kama wewe ILa wako vijana wenzangu humu ndani ambao wanadiriki kukutukana na kusema wewe mdini kitu ambacho mimi sijaona.

MUNGU aendelee kukupa uhai na afya Tele mwanadar es salaam yake.. Ofisi yako iko wapi nipe address Zake niweze kufika siku Moja inshaalah
 
Ndege...
Amin kwa sote.
Karibu ndugu yangu.
 
We mzee sikupingi na siwezi kuja kukuvunjia adabu mwanazuoni kama wewe ILa wako vijana wenzangu humu ndani ambao wanadiriki kukutukana na kusema wewe mdini kitu ambacho mimi sijaona.

MUNGU aendelee kukupa uhai na afya Tele mwanadar es salaam yake.. Ofisi yako iko wapi nipe address Zake niweze kufika siku Moja inshaalah
Mdini tu, na hapati faida yeyote
 
MAJINA YA ALI (ALLY) KATIKA HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Katika vibao hivyo vitatu kimoja kimekosekana.
Kimesosekana kibao cha Ali Masham wa Magomeni Mapipa.

Ali Masham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilifanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya viongozi wa serikali ya mtaa hawajaona umuhimu kwa kuhifadhi jina la mzalendo huyu.

Bado nasubiri kibao cha nne cha Ali Msham nikamilishe historia ya akina Ali katika historia ya TANU.

Umenikumbusha kipindi kile naenda MKOA WA LINDI kwa kina ENGELBERT, kulikuwa kuna jamaa mmoja anaitwa ALLY. Jirani na BIBI AKIDA pale LINDI MJINI 😀
 
MAJINA YA ALI (ALLY) KATIKA HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Katika vibao hivyo vitatu kimoja kimekosekana.
Kimesosekana kibao cha Ali Masham wa Magomeni Mapipa.

Ali Masham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilifanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya viongozi wa serikali ya mtaa hawajaona umuhimu kwa kuhifadhi jina la mzalendo huyu.

Bado nasubiri kibao cha nne cha Ali Msham nikamilishe historia ya akina Ali katika historia ya TANU.

Mimi nina historia nzuri na BIBI AKIDA kupitia kwa ALLY wa LINDI MJINI 🙏🏾😄
 
Charles...
Wanasema chini ya kila paa kuna historia.
Tuwekee historia hiyo.

Mimi nakuwekea hapo chini historia ya Ali Ibrahim Mnjawale:

''Tawi la Lindi lilikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, na lilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere na uongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam.

Salum Mpunga, mwanachama muasisi wa TANU, na Ali Ibrahim Mnjawale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kama wajumbe kutoka Jimbo la Kusini.

Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekeza wajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere aje kufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajili ya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwa zikitawanywa na Yustino Mponda.

Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kama mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikiano wake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani ya serikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Huu ulikuwa Mkutano Mkuu wa kwanza wa TANU uliofanyika Hindu Mandal Gandhi Hall, Dar es Salaam 1955.

Angalia picha hapo chini:

1710185843858.png
1710186084018.png

Salum Mpunga
1710186510404.jpeg

Back
Top Bottom