Makala za Mohamed Said Katika Mwananchi: Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
19,656
28,328
Wanaukumbi,

Kuanzia leo Jumatano, 28 Septemba
Mwananchi limeanza "series" zangu na
za waandishi wengine kuhusu Miaka
50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Tusomeni kwa furaha.

Mohamed Said


========================
UPDATE 29/09/2011
========================
Na Mohamed Said

Historia ya kudai uhuru wa Tanganyika bado haijaandikwa kwa ukamilifu wake sasa miaka 50 toka nchi ijitawale. Kwa kuwa haijaandikwa Tanganyika imebakia kuwa nchi isiyokuwa na mashujaa wake ukaichia shujaa mmoja Julius Kambarage Nyerere. Historia nzima ya TANU na juhudi za kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye ukoloni unazunguka kwake yeye peke yake. Kuna uvumi kuwa waliokuwa madarakani wanaogopa historia hii kwa kuwa imejaa mchango wa Waislam na wana hofu kuwa endapo mashujaa hawa Waislam wataenziwa huenda hata mustakbali wa nchi ukabadilika. Katika hofu hii nchi imebakia katika kutojitambua na kuwatambua mashujaa walioikomboa Tanganyika kutoka makucha ya Waingereza. Viongozi wakubwa na wanachama wa mwanzo katika TANU walitoka Rufiji kasha wakafuatia wanachama wa mwanzo Dar es Salaam katika mitaa ya Gerezani na Kariakoo ikafuatia.

Naikumbuka Gerezani kama vile ilikuwa jana. Kuanzia mitaaa yake hadi nyumba zilizokuwapo pale pamoja na wakazi wake ambao kwangu mimi walikuwa baba, mama, shangazi zangu na wajomba ukiachilia watoto wa rika langu tuliokua tukicheza pamoja wengi wao wameshatangulia mbele ya haki wengine katika umri mdogo sana na wengine katika utu uzima. Lakini sote tulishuhudia harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na tukauona uhuru wenyewe sisi tukiwa kizazi cha mwisho kuzaliwa ndani ya minyororo ya ukoloni. Mitaa ya Gerazani takriban yote ilikuwa ni barabara za vumbi tupu lakini mchanga kama mchanga uliopo pwani. Ingawa hadi sasa hali ni kama ile iliyokuwa miaka ile mchanga hauonekani tena na mahali pale kuna udongo wa tope mvua zikinyesha kitu ambacho hakikuwapo hapa zamani.

Kwa sisi watoto ule mchanga kwetu ilikuwa afueni maana tuliweza kucheza tukakimbizana bila ya madhara ya kuumia sana endapo mmoja wetu ataanguka. Mchezo tuliokuwa tukiupenda sana ulikuwa mpira wenyewe tukiita"chandimu" na nyakati za usiku tukicheza mchezo wa kujificha. Mtaa wetu ulikuwa unaitwa Kipata Street. Jina hili wengi hawalijui asili yake lakini ni moja ya vijiji ambavyo "mvumbuzi" David Livingstone alivipitia katika safari zake Nyasaland.

Mtaa wa mbele ya Kipata ni mtaa maarufu wa Kitchwele Street sasa unaitwa Mtaa wa Uhuru. Hakuna ajuaye hili neno "Kitchwele" nini maana yake. Lakini mtaa huu umepata heshima kubwa kwa kubadilishwa jina na kuitwa "Uhuru" Tanganyika ilipojikomboa kutoka ukoloni wa Waingereza tarehe 9 Desemba 1961. Nyuma wa Kipata Street ulikuwa mtaa wa Kirk Street sasa unaitwa Mtaa wa Lindi. Asili ya jina la Kirk ni Consular John Kirk aliyekuwa akitazama maslahi ya Waingereza Zanzibar. Sasa wazee wetu walikuwa hawawezi kulitamka jina hilo kama litakiwavyo badala yake wakawa wanasema "Kiriki" jina lililodumu hadi mtaa ulipobadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Lindi. Nakimkumbuka kibao chake cha mtaa kiliandikwa kwa wino mweupe kwenye kibao cheusi "Kirk Street." Nyuma ya Kirk Street ulikuwa mtaa wa Somali na nyuma ya Somali kulikuwa "Kiungani Street." Asili ya jina hili ni Kiungani Zanzibar ambako Universities' Mission to Central Africa (UMCA) ilijenga kanisa lake la kwanza pwani ya Afrika Mashariki katika miaka 1800.

Sasa tuingie katika mitaa ya kukatisha. New Street ndiyo ilikuwa inatengeanisha Gerezani na Uwanja wa Mnazi Mmoja, kisha inafuatia mtaa wa Livingstone, Sikukuu, Swahili, Nyamwezi, Congo na mwisho Msimbazi. Kisha kulikuwa na mitaa miwili midogo, Somali Kipande na Mbaruku. Kwa wakati ule kwa ajili ya udogo wangu ilikuwa shida sana kupambanua kuwa majina ya mitaa hiyo ya "Kipata," "Kirk," "Livingstone" na "Kiungani" ilikuwa ni kiashiria kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya ukoloni wa Waingereza. Kwa Waingereza majina hayo yalikuwa yanawakumbusha mashujaa wao akina David Livingstone, Morton Stanley na ushawishi wao katika sehemu ambazo Waingereza walituma watu wao ama kuja "kuzivumbua" au kutawala. Juu ya hayo Gerezani ilijipambanua na mitaa mingine ya Dar es Salaam kwa kuwa na wapigania uhuru wengi waliokuja kutoa mchango mkubwa katika TANU. Lakini kwa bahati mbaya sana kwa hao wazalendo wote mchango wao haujathaminiwa wala hakuna leo mtu anaewafahamu au kuwakumbuka. Sasa hebu tuanze matembezi ya nyumba kwa nyumba kuzipitia nyumba walokuwa wakiishi wazalendo wapigania uhuru wa Tanganyika ili tuwakumbuke na tueleze yale waliyofanya wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tuanze Kipata Street inapoanza Gerezani. Kipata Street inaanzia kule Msimbazi.Pale kulikuwa na nyumba ya Abdallah Salum Matimbwa akifanya kazi Relwe. Nyumba yenyewe ya asili leo haipo. Mtoto wa MZee Abdallah Salum Matimbwa, Salum Matimbwa amejenga ghorofa. TANU ilipoanzishwa Abdallah Salum Matimbwa alikuwa mmoja wa wanachama wake wa mwanzo mwanzo lakini kwa kuwa wakati ule kudai uhuru lilikuwa jambo la hatari na yeye alikuwa mwajiriwa alijiunga TANU na kuwa mwanachama kwa siri. Halikadhalika alikuwa mwanachama wa Zaramo Union chama cha kikabila kikiendeshwa na Max Mbwana. Vyama hivi vya kikabila Waingereza wakivipenda sana kwa kuwa viliwasaidia katika ile njama yao wa "wabague uwatawale" Salum Matimbwa anaingia katika historia ya ukombozi wa Tanganyika si tu kama mwanachawa wa awali waliojiunga na TANU kabla ya 1958 bali kama mmoja wa wazalendo waliochanga fedha kuanzisha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Fikrra ya kuanzisha Chuo Kikuu inasemekana ilianza na Nyerere akiwa na Dossa.

Ilkuwa kawaida ya Dossa baada ya mikutano ya TANU pale Mnazi Mmoja kumchukua Nyerere na gari lake kumrudisha Pugu. Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita hapo kilipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Sasa ilikuwa kiza kimeingia na walitaka kutoka nje ya gari kuangalia mandhari ya Dar es Salaam maana kutokea pale mji ulikuwa unapendeza sana kwa taa zilizokuwa zikiwaka barabarani. Nyerere alimwambia Dossa, "Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge Chuo Kikuu." Hili wazo lilifanyiwa kazi na wananchi wakahamasishwa kuchangia ujenzi wa Chuo hicho. Fedha zilichangwa na Chuo kikajengwa pale New Street kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kuwapa TANU. Hapo ndipo kilipoanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. (Chuo hiki sasa ni Chuo Cha Watu Wazima).Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo y ash. 50.00 stakabadhi ambayo ina saini ya Joseph Nyerere. Wazee hawa walikuwa wazalendo wa kweli kabisa. Baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 na zilipokuwa zikianzishwa harakati za ushirika Abdallah Salum Matimbwa alitoa lori lake Commer Fargo DSY 435 kama mtaji kuingiza katika Coast Region Transport Company (CORETCO). Pamojanae katika kuanzisha CORETCO walikuwa wazee wengine kama Sharia Bofu na nduguye Ibrahim Bofu, Salum Kambi, Juma Mzee na wengineo.

Unateremka sasa Kipata unaelekea Mnazi Mmoja. Kipata kona na Congo kulikuwa na nyumba ya Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association mwaka 1929. Huyu alikuwa Mnubi kutoka Darfur. Baba yake alikuwa askari wa Kinubi walokuja Tanganyika na Kamanda wa Kijerumani Harmine von Wissman kuja kuwasaidia Wajerumani katika vita yao dhidi ya wazalendo wa Tanganyika akina Bushiri bin Harith wa Pangani na Chifu Mkwawa kutoka Kalenga. Ibrahim Hamisi akifanya kazi Government Press kama "composer." Wajerumani walikuwa wajanja na wepesi katika kulipa fadhila. Waliwasomesha vizuri sana watoto wa askari wao waliowaleta Tanganyika kuja kuwasaidia kutawala. Kwa njia hii waliweza kujenga tabaka la wageni lililokuwa juu kupita wenyeji wa Dar es Salaam, Wazaramo, Wamashomvi nk. Hali hii kwa kiasi Fulani ilileta migogoro baina Wamanyema, Wazulu na Wanubi kwa upande mmoja ambao walionekana kama "watu wa kuja" na wenyeji wazawa wa Dar es Salaam kwa upande mwingine.

Kwa wakati ule kazi ya "composer" ilikuwa kazi yenye hadhi kwa Mwafrika na ilihitaji mtu aliyesoma. Ibrahim Hamisi alikuwa mmoja wa waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika chama cha Waislam kilichoanzishwa mwaka 1933 na kikajenga shule Al Jamiatul School New Street kona na Stanley Street ambayo jengo lake lipo hadi leo Mtaa wa Lumumba na Max Mbwana. Uongozi wa Al Jamiatul Islamiyya ndani yake mlikuwa na Waarabu, Wanubi, Wazulu, Wamanyema, Wazaramo na makabila mengine ya pwani na mara nyingi Wazulu na Wanubi ndiyo wakishika uongozi. Na hii ilipata kujaleta mgogoro mkubwa mwaka 1940 kiasi cha kufunga shule kwa muda hadi Gavana akaingia kati kusuluhisha. Hii Ilikuwa katika Ali Aljamiatul Islamiyya lakini hata katika African Association mambo yalikuwa hivyo hivyo. Mwaka wa 1933 kulitokea ugomvi uliosababisha secretary Kleist Sykes ajiweke pembeni katika chama hadi alipoombwa na Mzee bin Sudi aliyekuwa president ndipo aliporejea tena katika chama. Mzee Bin Sudi alikuwa Mmanyema. Hizi ndizo zililiwa siasa za wakati ule.

Mbele ya Kipata Street ukishapita Swahili Street unafika nyumba ya Hassan Machakaomo. Kizazi kingine cha wageni kutoka nje ya mipaka ya Tanganyika. Hassan Machakaomo ni mtoto wa Machakaomo Mzulu askari mamluki kama walivyokuwa Wanubi. Wazee wake waliletwa Tanganyika na lile jeshi mamluki la Harmine von Wissman. Hassan Machakaomo alijulikana zaidi kama kiongozi wa Young Africans Football Club katika miaka ya 1950 na harakati za kudai uhuru zilipoanza mwaka 1954 Young Africans, "Yanga" kama ilivyokuwa inajulikana ilijinasibisha moja kwa moja na bila ya kificho na TANU. Si mbali na nyumba hiyo kwa mkono wa kulia Kipata kona na Sikukuu ilikuwa nyumba ya Clement Mohamed Mtamila ambaye katika miaka ya mwisho ya 1940 ndiye alikuwa katibu wa TAA baada ya African Association kubadilisha jina na kuitwa TAA. Hapa itabidi tusimame kidogo.


Itaendelea...


========================
UPDATE 05/10/ 2011
========================
Baada ya vita ya pili ya dunia vijana askari waliokuwa katika King's Africa Rifles (KAR) 6[SUP]th[/SUP] Batallion waliopigana Burma katika wengi wao wakiwa Dar es Salaam walianza kuwachachafya viongozi wazee waliokuwa wakiongoza TAA. Rais wa TAA wakati ule alikuwa Mwalimu Thomas Plantan mtoto wa Afande Plantan mkubwa wa askari mamluki wa Kizulu aliokuja Tanganyika na Harmine von Wissman. Afendi Plantan alikuwa ndiye kiongozi wa askari wa Kizulu na mkubwa wa Wazulu wote pale mjini. Afendi Plantan hakutoroka na Harmine von Wissman kurudi kwao Mozambique baada ya Vita ya Kwanza kumalizika na jeshi la Wajerumani kushindwa wakaoroka kukimbilia Mozambique kupata hifadhi. Afande Plantan alibaki Dar es Salaam na kuweka makazi yake Mtaa wa Masasi Mission Quarter Mtoto wa Affendi Plantan Thomas, akijulikana kwa jina lingine la Sauti alipata elimu nzuri katika shule ya Kijerumani akawa mwalimu wa shule. Thomas Plantan alistawi hadi kufikia kushika uongozi wa African Association. Sababu ya uongozi huu wa wazee kuchachafwa ni kuwa vijana walikuwa wakiona chama hakina malengo ya kudai uhuru wa Tanganyika. Kwa hakika chama kilikuwa kimezorota sana. Mikutano ilikuwa haiitishwi na chama kilikuwa hakina fedha za kuweza kujiendesha. Hapa ndipo tunakutana na kijana Abdulwahid Sykes, mtoto wa Kleist Sykes, (Mzulu mwingine) yeye na kundi la vijana wenzake, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando, Dr Vedasto Kyaruzi na wengineo wakawa wanatafuta njia za kuingia katika uongozi wa TAA ili wadai uhuru wa Tanganyika. Tatizo lililowakabili ikawa wazee hawataki kuachia hatamu za uongozi wala kuitisha mkutano wa uchaguzi.
Thomas Plantan alikuwa muwindaji na alitumia muda wake mwingi porini kuwinda, hakuwa na muda na siasa za mjini. Hata miaka mingi baada ya kifo chake, bado kuta za nyumba yake Masasi Street, Mission Quarter zilipambwa na vichwa vya pofu na mbogo aliowaua porini. Hata hivyo walikuwapo wazee ambao ingawa walikuwa watu wazima lakini walikuwa wanataka kuona mabadiliko katika TAA. Mmoja wa wazee hawa alikuwa Schneider Plantan, mdogo wake Thomas Plantan. Katika mkutano ulipoitishwa Arnautoglo Hall mwaka 1950, Schneider alifanya vurugu mbele ya maofisa wa kikoloni kiasi ilibidi wazee wakubali kuitisha mkutano wa uchaguzi, lakini kabla ya uchaguzi kufanyika Abdulwahid Sykes na Hamza Mwapachu walivamia ofisi za TAA pale New Street na kuchukua uongozi kwa nguvu wakaitisha mkutano wa uchaguzi na Dr Vedasto Kyaruzi akachaguliwa President na Abdulwahid Sykes Secretary. Hii ilikuwa mwaka 1950.
Inasemekana harakati za kupanga mipango ya kufanya mapinduzi katika TAA ilikuwa ikipangwa Ilala Welfare Centre ambako Hamza Mwapachu alikuwa akifanya kazi kama Welfare Officer, mahali pengine ilikuwa Kariakoo Market ambako Abdulwaihd alikuwa Market Master. Tuachie hapa, tutakuja kuyazungumza haya huko mbele. Turudi kwenye nyumba ya Mzee Mtamila turudi kwa Nyerere. Nyerere aliambiwa na mwajiri wake achague moja siasa au kazi. Nyerere alilileta tatizo hilo kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee. Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu. Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya Nyerere kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi. Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu.
Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid Kariakoo Market. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba Mtaa wa Stanley na Abbas Sykes ndiye aliyeambiwa na kaka yake atoke chumbani kwake ampishe Nyerere. Abbas wakati ule alikuwa kijana mdogo. Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma. Mtamila. Nyumba hii leo haipo, ilipokuwa nyumba ya Mzee Mtamila kuna gorofa na si watu wengi wanofahamu historia iliyopata kubebwa na nyumba ile. Leo hakuna anaewajua watu hawa wala historia haiwataji lakini walifanya kazi kubwa sana. Clement Mtamila hatajwi, Tatu Biti Mzee hatajwi wala Iddi Faizi Mafongo ndiye aliyefanikisha ukusanyaji wa fedha za TANU ziliotumiwa kumpeleka Nyerere Umoja wa Mataifa, New York. Watu wachache sana wanajua kuwa Sheikh Iddi Faizi Mafongo alichota fedha katika hazina ya Aljamitul Islamiyya kutunisha mfuko wa TANU ili Nyerere aende Umoja wa Mataifa kudai uhuru wa Tangnayika. Hili la kuchota fedha za Al Jamiatul Islamiyya halikuwa na shida yoyote kwani katibu wake alikuwa Ali Mwinyi Tambwe mmoja wa watu wa mwanzo kujiunga na TANU. Licha ya hilo Abdulwahid na Ally walikuwa na sauti katika jumuia hiyo kwa kuwa ilianzishwa na baba yao na walisoma Al Jamiatul Islamiyya Muslim School. Akina Tatu bint Mzee, Bi Asha Ngoma, Bi Hawa Maftah, Bi Titi Mohamed, Mwalimu Sakina Arab na wanawake wengine wa mjini ndiyo waliotia nyimbo za Lelemama katika kwaya ya TANU nyimbo ambazo zilihamasisha watu kupita maelezo. Kuna nyimbo moja ilikuwa inaimbwa hivi:
"Muheshiwa nakumpenda sana,
Wallahi sina mwinginewe,
Insha Allah Mungu yupo,
Tanganyika tutajitawala"
Hii ndiyo ilikuwa nyimbo ya mwanzo ya lelemama kutiwa katika harakati za kudai uhuru na baada ya hapo zikaja nyingine nyingi lakini maarufu na inayofahamiza zaidi ni "Hongera Mwanangu." Mzee Mtamila ameacha hazina kubwa sana ya picha za siku za mwanzo za harakati za kudai uhuru zikionyesha wana TANU katika mikutano ya mwanzo Mnazi Mmoja. Picha hizi zilipigwa na Mzee Shebe Mohamed Awadh ambae studio yake ilikuwa Livingstone Street si mbali na nyumbani kwa Mzee Mtamila. Baadhi ya picha zikimuonyesha Mzee Mtamila, Bibi Titi Mohamed, John Rupia wakiwa wamekaa katika jukwaa huku Mwalimu Nyerere akihutubia wananchi. Studio ya Shebe ilikuwa Livingstone Street kona na Kipata unaelekea Kiungani mkono wa kushoto kulikuwa na nyumba ambamo kulikuwa studio ya Mzee Shebe. Mzee Shebe ndiye alikuwa mpiga picha wa mwanzo wa TANU na Nyerere na ameacha hazina kubwa ya historia ya TANU na Nyerere katika picha. Ukitaka kuijua historia ya TANU na matokeo yote kuanzia 1954 hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1961 pitia picha za Mzee Shebe ambazo hivi sasa hazina hii imehifadhiwa na watoto wake mjini Dar es Salaam.
Ukivuka Kipata mbele unakutana na Livingstone Street, ukitazama mkono wa kulia kabla ya kufika New Street labda nyumba tatu kabla pale ndipo ilipokuwa nyumba ya Kleist Sykes, Mtoto wa Sykes Mbuwane, askari wa Kizulu aliyekufamaji Mto Ruaha akiwa anarudi vitani baada ya kumshinda Mkwawa. Hii ilikuwa mwaka wa 1898. Kuna kisa kitatokea miaka 56 baadae kati ya kizazi cha Mtwa Mkwawa na Sykes Mbuwane. Wajukuu wao watakuwa wamoja katika TANU kupambana na ukoloni. Nitakieleza kisa hicho kwa ufupi. Mwaka 1954 fuvu la Mkwawa liliporudishwa Kalenga Adam Sapi Mkwawa mjukuu wa Mtwa Mkwawa aliwaalika Abdulwahid Sykes mjukuu wa Sykes Mbuwane, adui wa babu yake na Dossa Aziz kuja katika sherehe ya kupokea fuvu lile. Ilikuwa pale Kalenga ndipo Abdulwahid alipomuingiza Adam Sapi katika TANU kwa siri na kumfanya awe mmoja wa machifu wa mwanzo kabisa kuiunga mkono TANU. Wakati Chifu Adam Sapi anajiunga na TANU chama kilikuwa hakijamaliza hata mwezi moja katika uhai wake. Tutazieleza habari za Abdulwahid Sykes na ushawishi mkubwa aliokuwa nao katika TAA na baadae TANUna katika wanasiasa wa wakati ule pamoja na machifu tutakapofika kusanifu makazi yake pale Stanley Street kona na Sikukuu Street. (Baada ya uhuru mtaa huu ulikuja ulibadilishwa jina na kuitwa Aggrey) Ila ieleweke tu kuwa kwa wakati ule wa siku za mwanzo za harakati kuanzia enzi za TAA baadhi ya machifu hawakuitazama TAA na baadae TANU kwa jicho zuri sana. Hofu kuu na ndiyo hofu aliyokuwanayo mshirika wao Muingereza katika ule mfumo "indirect rule" wa Lord Lugard ni kuwa TANU imekuja kuwanyang'anya madaraka yao.
Sasa turejee kwenye nyumba ya Kleist Sykes hapo Kipata. Kwa hakika Kleist alikuwa mtu wa mipango na mjengaji wa mikakati si tu katika maisha yake binafsi bali hata katika kupeleka mbele maslahi ya Waafrika katika Tanganyika. Kleist alizaliwa Pangani mwaka 1894. Akiwa na umri mdogo wa miaka 25 alikuwa keshaasisi African Association mwaka 1929 na kufikia mwaka 1933 aliasisi Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika, hicho ni Kiarabu (maana yake kwa Kiswahili ni "Umoja wa Waislam wa Tanganyika"). Mwaka wa 1924 Dr Aggrey alikuja Tanganyika kama mjumbe katika kamisheni moja ya elimu kuchunguza hali ya elimu kwa Waafrika wa Tanganyika. Kwa wakati ule Dr Aggrey alikuwa mfano wa Mwafrika aliyeelimika sana. Alipokuwa Dar es Salaam Dr Aggrey alikutana na Kleist na katika mazungumzo Dr Aggrey alimshauri Kleist kuwa endapo Waafrika wanataka kupiga hatua ni lazima waunde umoja wao. Ilimchukua Kleist miaka mitano hadi kuja kufanikisha ushauri ule na kuunda African Association akiwa katibu muasisi.
African Association na Al JAmitul Islamiyya ndivyo vilivyokuja kuwa chimbuko la kuundwa kwa TANU kwa kutoa viongozi kama Abdulwahid na Ally Sykes, Ally Mwinyi Tambwe, Iddi Faizi Mafongo, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Abdalla Iddi Chaurembo, Sheikh Suleiman Takadir na wengineo na wanachama wake wa mwanzo. Kleist alilelewa nyumba moja na Thomas, Schneider na Mashado Plantan baada ya kifo cha baba yake. Hapa ningependa kidogo kuwaeleza wasomaji asili ya majina haya ya Kikristo na yenye asili ya Kijerumani. Hawa watoto baba zao walikuwa askari katika jeshi la Wajerumani. Wajerumani baada ya kuituliza Tanganyika kwa mtutu wakaliita lile jeshi lao la mamluki wa Kinubi na Wazulu "Germany Constabulary." Mkubwa wa jeshi hili alikuwa Afendi Plantan, baba yao Thomas, Schneider na Mashado.


Itaendelea...


=========================
Update: 10/10/2011
=========================
Tumkumbuke Marehemu Mzee Kiyate Mshume
  • Dalali wa Samaki Kariakoo na Mfadhili wa TANU na Nyerere


Mohamed Said

Napenda nieleze kisa hiki cha kusisimua cha marehemu Mshume Kiyate kama nilivyoelezwa na mzee wangu Ahmed Rashad Ali, kisa ambacho yeye alihadithiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa kinywa chake mwenyewe. Ahmed Rashad anasema siku aliyosikia kisa hiki yeye alikuwa pamoja na Dossa Aziz na Lucy Lameck. Ilikuwa mwaka wa 1965 siku ile mlowezi Ian Smith alipojitangazia uhuru kutoka kwa Waingereza. Ahmed Rashad wakati ule alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi Idara ya Habari na alikwenda nyumbani kwa Mwalimu Msasani ili apate kauli ya Mwalimu Nyerere na msimamo wa serikali kuhusu mgogoro wa Rhodesia. Walimkuta Mwalimu Nyerere nyumbani kwake katika maktaba yake anaandika. Ahmed Rashad anasema Nyerere aliwaeleza kuwa katika kutafakari mambo yaliyokuwa yakiendelea Rhodesia, Uingereza haitofanya lolote dhidi ya Ian Smith kwa kujitangazia uhuru wa maguvu. Ahmed Rashad alinieleza kuwa Mwalimu Nyerere alisema, "Hawa ni mtu na mjomba wake," akikusudia kuwa Waingereza na walowezi wa Rhodesia walikuwa ndugu wa damu kwa hiyo Waingereza hawatatia jeshi pale kuwang'oa walowezi.

Baada ya Mwalimu Nyerere kumaliza kutoa msimamo wake wakawa sasa wamekaa wanapiga gumzo huku wakinywa vinywaji na Mwalimu alikuwa mtu hodari sana wa kustawisha baraza. Waliokuwa karibu na Nyerere wanamjua kwa sifa hii. Mwalimu Nyerere alianza kuhadithia kisa chake na Mshume Kiyate. Haifahamiki hasa ni lini Nyerere alijuana na Mzee Mshume lakini huenda ilikuwa hata kabla ya kuaisiswa kwa TANU siku zile za TAA Nyerere alipokuwa nakwenda ofisini kwa Abdulwahid Sykes pale Kariakoo sokoni ambako Abdulwahid alikuwa Market Master. Mzee Mshume alikuwa ndiye dalali wa samaki soko la Kariakoo na alikuwa mzee aliyeheshimika sana mjini Dar es Salaam na baadae alikuja kuwa mmoja wa wazee katika Baraza la Wazee wa TANU. Nyerere alianza kukihadithia kisa chake na Mzee Mshume kwa kusema kuwa siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita kwa miguu kuelekea Kariakoo ili kupata mahitaji yake lakini katika safari hiyo mfukoni mwake alikuwa hana hata senti moja. Akiwa njiani karibu na sehemu inayoitwa Mwembe Togwa (hapa kwa leo ni pale Fire makutano na Morogoro Road na Barabara ya Umoja wa Mataifa)Mwalimu alikutana na Mzee Mshume Kiyate. Mwalimu Julius Nyerere akamfahamisha Mzee Mshume kuwa alikuwa anakwenda sokoni Kariakoo lakini hana fedha za kununulia mahitaji yake. Mzee Mshume Kiyate aliingiza mkono katika koti lake akatoa shilingi mia mbili na kumpa Nyerere. Ukitaka kujua thamani ya fedha hiyo kwa wakati ule, naitoshe kujua kwamba ilimgharimu mtu shilingi mia tano tu kujenga nyumba ya vyumba sita katika eneo la Kariakoo.

Mzee Mshume alifadhaishwa sana na hali ile ya Nyerere kuwa anahangaika na kuikimu familia yake na huku wamemtwisha mzigo wa kuendesha TANU. Kutokana na hali hii Mzee Mshume aliona itakuwa ni kumtaabisha Nyerere bila sababu ikiwa atakuwa anashughulika na kuwatafutia wanawe chakula na wakati huohuo akiwa na jukumu la kufanya kazi za TANU. Hapo ndipo Mzee Mshume alipojitolea kuihudumia nyumba ya Mwalimu Julius Nyerere. Kila asubuhi Landrover ya TANU inapiga breki Karikaoo sokoni pale na Mzee Mshume ananunua mahitaji yote ya siku anamkabidhi dreva wa TANU jina lake Said lakini watu wakampachika jina wakimwita TANU. Said TANU anachukua vitu vile anapeleka vile Magomeni Majumba Sita kwa Mama Maria. Mzee Mshume alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana. Baada ya uhuru Mwalimu Nyerere sasa akiwa Waziri Mkuu alimwomba Mzee Mshume aache kumnunulia chakula lakini Mze Mshume alikataa na badala yake akamtafadhalisha Mwalimu Nyerere aendelee kupokea chakula chake na kile ambacho kinatolewa na serikali kwake yeye, kama mkuu wa nchi alimuomba Mwalimu awakirimu wageni wake. Mwalimu Julius Nyerere alikiita kisa hiki ‘the TANU spirit' – yaani moyo wa TANU – akieleza mapenzi na moyo waliokuwanao wana TANU wakati ule wa kudai uhuru.

Kisa hiki kwa mara ya kwanza kabisa kilihadithiwa hadharani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa wakati ule marehemu Ditopile Mzuzuri Mkiwaona kada wa Chama Cha Mapinduzi. Ditopile alikieleza kisa hiki kama alivyokieleza Mwalimu Nyerere kwa Ahmed Rashad na Lucy Lameck kwa nia ya kuonyesha moyo wa TANU na mchango wa wazalendo katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Kisa hiki kwa Dossa hakikuwa kipya. Dossa akimjua Nyerere nje ndani. Kwa bahati mbaya waandishi wa magazeti wakapotosha kisa kizima. Badala ya kutoa umuhimu kwa moyo wa ukarimu wa Mzee Mshume na kumueleza kama mzalendo aliyejitolea katika kupigania uhuru, magazeti yakageuza maneno ya Ditopile kuwa masimango dhidi ya Mwalimu Nyerere. Kwa ajili hii nafasi ambayo ingeliweza kutumiwa ili kueleza umuhimu wa Mzee Mshume na historia ya TANU ikapotezwa.

Tuendelee na Mzee Mshume na Mwalimu Nyerere. Tarehe 20 Januari 1964 wanajeshi waliasi ikabidi Nyerere aombe msaada kwa Waingereza waje kuwanyang'nya silaha askari. Baada ya uasi ule kuzimwa na jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam. Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Nyerere kilemba kama ishara ya kumuunga mkono. Hakuna picha alioyopiga Nyerere kati ya mwaka 1955 na 1961 ambayo Mzee Mshume asiweko ndani yake. Mzee Mshume alikuwa mstari wa mbele katika harakati za uhuru na kumuunga mkono Nyerere kwa kila jambo kwa hali mali. Picha ya Mzee Mshume akimvisha Nyerere kilemba ilichapishwa katika magazeti mengi. Halikadhalika picha nyingine mashuhuri ya Mzee Mshume na Mwalimu Nyerere ni ile iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu.Picha hiyo inamuonyesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti, kanzu na kofia na huku amemshika Mwalimu Nyerere mkono akimsindikiza kupiga kura. Magazeti ya Chama na Serikali – Uhuru na Daily News yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu kupiga kura na kumchagua Mwalimu Julius Nyerere. Kwa bahati mbaya picha ile siku zote hutoka bila maelezo na kwa hiyo wengi hawafahamu yule mzee aliyefuatana na Mwalimu Julius Nyerere ni nani. Kadhalika si wengi wanaoufahamu mchango wa Mzee Mshume Kiyate katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwa sababu Mwaka 1995 Jiji lilipoamua kubadilisha jina la mtaa aliokuwa akiishi Mshume Kiyate – yaani Mtaa wa Tandamti ili uitwe Mtaa wa Mshume Kiyate kama ishara ya kumuenzi na kuthamini mchango wake katika kupinga ukoloni, baadhi ya magazeti yalipinga kitendo hicho na hadi leo mtaa ule haujawekewa kibao kilicho na jina la Mshume Kiyate.

Hofu iliyotanda katika vyombo vya habari na kwa wengi wasiojua historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa mbona majina ya mitaa yote yanapewa majina ya Waislamu? Lakini kubwa zaidi la kushangaza sana ni kuwa hata pale magazeti yalipokuwa yameingia katika malumbano ya kupinga majina yale mapya ya wazalendo katika mitaa kama vile Kleist Sykes, Max Mbwana, Mshume Kiyate, Tatu Bint Mzee, Omari Londo nk. Mwalimu Nyerere ambaye yeye ndiye akiwajua vyema mashujaa hawa alikuwa kimya. Katika mahojiano aliyofanyiwa Meya wa Dar es Salaam, Kitwana Selemani Kondo na Serah Dumba wa Radio Tanzania kuhusu mabadiliko ya majina ya mitaa, Mzee Kondo alisema hao wanaosema hawawajui hao walioenziwa kwa kupewa majina yao kupewa mitaa waulize watu hao walikuwa nani wataelezwa.

Mzee Mshume amekufa pweke Hospitali ya Muhimbili na katika maziko yake hawakuonekana wale waliokuja faidi matunda ya uhuru. Akiwa kitandani mgonjwa pale hospitali alisikika mara kadhaa akimwambia mwanae akiitwa Kiyate, "Kiyate umewapa taarifa wenzangu (anawataja majina) kuwa mimi nimelazwa?" Mazishi ya Mzee Mshume yalifanyika mtaa wa Matumbi kwenye nyumba ya Sheikh Maguno aliyekuwa ndugu yake. Sheikh maguno ndiye alikuwa muadhini wa msikiti wa Shadhly kwa miaka 35. Mazishi ya Mshume Kiyate yalikuwa ya kawaida sana na wala hapakuwa na hotuba wala rambirambi. Kwa miaka mingi Mzee Mshume alipumzika kaburini kwake kwa amani hadi pale alipoenziwa na Kitwana Kondo kwa jina lake kupewa mtaa.
3 Oktoba 2011


Itaendelea....


=====================
UPDATE 13/ 10/ 2011
=====================
Mohamed Said

Sasa inasemekana wakizaliwa watoto Wajerumani ndiyo walikuwa wakitoa majina kwa watoto hao na majina waliyowapa ni ya Kijerumani ndiyo kukawa na Kleist, Thomas, Schneider, Mashado na mengineyo. Lakini wakiondoka tu palepale baba zao wakawa wanatoa majina ya Kiislam kwa kuwa wao walikuwa Waislam hawakupenda sana watoto wao wajulikane kwa majina ya Kikristo. Kwa mfano Kleist jina lake ni Abdallah, Shneider jina lake ni Abdillah na Mashado jina lake ni Ramadhani. Hadi leo kwenye kaburi la Kleist pale Makaburi ya Kisutu jina lake limeandikwa: "Kleist Abdallah Sykes." Haieleweki kwa nini yeye hakupenda kujinasibu na jina lake la asili "Mbuwane" au "Abdallah" na kwa nini watoto wa Plantan kwa jina lao la asili la "Mohosh" ambae huko kwao Kwalikunyi Mozambique alikuwa chifu wa Kizulu. Sasa zaidi ya miaka mia moja ukoo wa Sykes umevuma na kujulikana katika siasa na biashara kwa jina hilo la Kijerumani na hadi leo ukoo wa Plantan ambao uko Mission Quarter, Mtaa wa Masasi ni katika koo maarufu sana Dar es Salaam nao wanajulikana kama akina Plantan.

Kleist alisoma shule ya Kijerumani na shule yenyewe ndiyo hii sasa Ocean Road Hospital. Alisoma hadi darasa la sita na alipomaliza shule hapo alikuwa anasema Kijerumani, anajua short hand (hati mkato) na kupiga taipu. Huu ulikuwa ujuzi mkubwa sana kwa Mwafrika kuwa nao wakati ule. Lakini alipomaliza shule Wajerumani hawakumwacha afanye kazi ofisini walimtia katika jeshi na Vita Vya Kwanza vilipoanza mwaka 1914 Kleist na ndugu yake Scheneider Plantan walijikuta wakielekea Tanga kupambana na majeshi ya Kiingereza. Mkuu wa majeshi ya Kijerumani alikuwa Von Lettow Voberk na Kleist ndiye alikuwa Aide De Camp wake. Cheo kizito sana wakati ule kwa Mwafrika kukibeba. Baada ya vita na kushindwa kwa Wajerumani baadhi ya askari wa Kizulu walikimbia na kamanda wao Vorbeck na kuingia Mozambique. Wazulu waliobaki Tanganyika walikuwa wamepwelewa.

Kleist alikuwa mateka wa vita na alipoachiwa alianza kujifunza Kiingereza na hakutaka tena kujiunga na jeshi. Habari za Kleist ni nyingi sana na mengi katika maisha yake aliandika kwa mkono wake mwenyewe. Mwaka 1969 mjukuu wake, Daisy Sykes Buruku kwa msaada wa msaada wa baba yake, Abdulwahid Sykes na akiwa chini ya Profesa John Illife wa Chuo Kikuu Cha Cambridge wakati ule, Iliffe akisomesha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Disy akiwa mwanafunzi wake alikujakuandika upya maisha ya babu yake "Kleist Sykes The Townsman" katika kitabu "Modern Tanzanians" kilichohaririwa na John Illife. Katika kitabu hicho Kleist anatoka kama mwanasiasa makini na muasisi wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Kleist alifanya mengi Dar es Salaam, alijenga shule Al JAmiatul Muslim School, jengo la TAA ambamo TANU ilikuja asisiwa mwaka 1954, alikuwa katika baraza la Munispal Council, memba wa Dar es Salaam Maulid Committee, alikuwa kiongozi wa chama cha Wafanyakazi wa Relwe, alikuwa mfanya biashara mkubwa na mwanachama wa Chamber of Commerce Mwafrika pekee katika chamber.

Kleist aliwanunulia vyombo vya muziki wanae wakati huo vijana wadogo baada ya Abdulwahid na Ally kurudi vitani Burma mwaka 1945 walipokwenda kupigana kama askari katika KAR. Wanae pamoja na vijana wenzao wa mjini kama Matesa, Said Kastiko, Msikinya (huyu alikuwa ametokea Afrika ya Kusini), Dome Okochi Budohi na nduguye akiitwa Martin (hawa walikuwa wanatoka Kenya) wote hawa wakaanzisha bendi iliyojulikana kama "Skylarks." Baadae walibadili jina na kujiita "The Blackbirds" Kleist mwenyewe akiwa patron wa bendi na akihudhuria maonyesho ya bendi hiyo. Kulikuwa na bendi kama hiyo siku zile Johannesburg ikiitwa "Skylarks." Hili ni kundi ambalo Miriam Makeba wakati huo msichana mdogo alikuwa akiimba. Bendi hii ikaja tena baadae kubadili jina na kuitwa "Merry Makers." Bendi hii ilipendwa sana na vijana wa mjini wa wakati ule hasa kwa kuwa wao walipiga ile mitindo ya Ulaya kama Waltz, Foxtrot, Quick Step nk. Bendi hii ikipiga nyimbo zilizokuwa maarufu wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia na maiaka ya 1950 mwanzoni si Tanganyika tu bali hata Ulaya na Marekani kama "More," "Chacanuga Chouchou," "Siboney," "Siboney," "Fly Me to The Moon," "Perfidia" na nyinginezo, nyimbo ambazo zilipewa umaarufu na wanamuziki wakubwa wa Amerika na Uingereza kama Glenn Miller, Louis Armstrong, Charlie Parker, Benny Goodman, Andrew Sisters na wengineo.

Vijana hawa walikuwa wakipendwa sana hata Zanzibar ambako wakipiga Victoria Garden na kule mashabiki wao walikuwa akina Ahmed Rashad Ali (huyu alikujakuwa mtangazaji maarufu sana na mwanapropaganda mahiri katika Radio Afrika Huru kutoka Cairo wakati wa kupigania uhuru) nduguye Prince Sudi, Abdillah Masud maarufu kwa jina la "Smuts," (huyu alikuwa vitani Burma pamoja na akina Sykes), Mkubwa Mohamed Mashangama maarufu kama "Bwana Mkubwa Shoto" (jina hili la "Shoto" alilipata kwa kuwa alikua mcheza mpira maarufu na akipiga mashuti makali kwa mguu wake wa kushoto), na jamaa wengi. Kleist alipenda kukaa meza ya pembeni pale Arnatuoglo Hall nadhifu katika suti yake akitingisha mguu sawa na midundo iliyokuwa ikiporomoshwa na watoto wake na rafiki zao, picha ya King George ikiwa inamkodolea macho kwa juu ilipokuwa imetundikwa katika ukumbi ule. Baada ya kifo cha King George, ikatundikwa picha ya Queen Elizabeth ambayo hata sisi tuliikuta pale Arnautoglo katika miaka ya 1950 mwishoni. Hebu tusimame kidogo hapa.

Vijana hawa walipotoka utotoni na kuwa watu wazima na wakaanza siasa misingi hii waiyoijenga katika urafiki wao wa utotoni uliwasaidia sana katika harakati. Aman Thani mmoja wa viogozi wa Hizbu au (Zanzibar Nationalist Party) anasema ilikuwa Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz ndiyo walikuja na Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume. Historia bado haijaweka wazi mchango wa hawa watu watatu katika kuundwa kwa Afro-Shirazi Party lakini Issa Nassoro Ismaily amepata kusema kuwa Abdulwahid alipata kumweleza masikitiko yake kwa yale yalipotokea Zanzibar baada ya mapinduzi na akasema kuwa hapendi yeye kuzungumza suala lile kwa kuwa anahisi litavunja udugu baina yao. Halikadhalika Ali Mwinyi Tambwe hakupenda kabisa anasibishwe na mapinduzi yaliyotokea Zanzibar lau kama yeye alikuwa mmoja wa watu wa ndani katika kupanga mipango ile. Tuendelee.

Leo hii ukiangalia picha za wakati ule za bendi hii jinsi walivyokuwa wamevaa suti zao na "bow - tie" na ukiangalia zile ala za muziki pamoja na piano unaweza ukakosea ukadhani hiyo ni bendi ya Count Bessy, Louis Armstrong au Charlie Parker wa Marekani. (Kipindi hiki kiliibua vipaji, Hamza Aziz, mtoto wa Aziz Ally mmoja wa matajiri wakubwa Waafrika Dar es Salaam na rafiki wa Kleist alikuwa akiimba nyimbo za Nat King Cole na yeye mwenyewe alikuwa akijiita Nat Nat King Cole). Harakati za kudai uhuru zilipoanza mwaka 1954 Hamza Aziz alikuwa katika jeshi la polisi la kikoloni na kaka yake Dossa Aziz alikuwa mstari wa mbele na Nyerere katika TANU. Inasemekana TANU wakimtumia sana Hamza kupata siri za wakoloni. Sasa njoo angalia picha za mama zetu na mitindo ya nywele na magauni waliyovaa na mikanda mipana mithili ya wanawake wa Kizungu. Hapo wapo Arnatouglo Hall wakicheza mziki wa The Skylarks. Mama zetu waliokuwa ehe kidogo walikuwa wanavaa na glovu nyeupe kama wanawake waKizungu.

Nikiwa mtoto mdogo sana nina kumbukumbu ya party moja nyumbani kwetu Kipata Street na nyimbo ambazo zikipendwa sana wakati ule zilikuwa za Septet Habanero kutoka Cuba. Katika waliohudhuria party ile nina kumbukumbu ya Dome Okochi Budohi aliyekuja kuwa mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU na mtu aliyekuwa inasemekana kiungo kati ya TAA na KAU ya Jomo Kenyatta. Okochi Budohi kadi yake ya tano ni nambari sita. Budohi na mwanachama mwingine wa TANU Patrick Aoko walikamatwa mara tu hali ya hatari ilipotangazwa Kenya baada ya mapambano kati ya Wakikuyu na Waingereza kupamba moto. Msako huu na kamata kamata ilokwenda pamojanayo ilipewa jina "Operation Anvil" na Waingereza. Kundi zima la viongozi wa Kenya kama Kenyatta, Bildad Kaggia, Paul Ngei, Kungu Karumba na wengine waliwekwa kizuizini sehemu moja Kenya ijulikanayo kama Manyati. Wakenya hawa wanachama wa TANU walitiwa mbaroni na kurudishwa Kenya chini ya ulinzi mkali wakiwa wamefungwa minyororo. Leo hii hakuna anaejua kuwa TANU ilikuwa na wanachama na viongozi Wakenya ndani yake toka enzi za TAA. Dome Budohi licha ya kuwa alikuwa mmoja katika vijana wa Skylarks vilevile alicheza senema na Kawawa iitwayo "Mgeni Mwema."

Turejee kwa Kleist. Hapakuwa na mfano wa Kleist katika mji wa Dar es Salaam. Kleist alikuwa na kinyozi wake tena Muhindi akija mnyoa ndevu na nywele nyumbani. Kleist alikuwa anakwenda kazini kwa baskeli kitu nadra katika miaka ile na aliwanunulia wanae baskeli ndogo za kupanda kitu ambacho Mwafrika wa kawaida hakumudu. Kleist akiwashangaza wengi kwani alikuwa akila juu ya meza na wanae. Utamaduni wa wakati ule ulikuwa watu kula chini juu ya mkeka au jamvi. Wenzake wakimuona Kleist akiishi kama Mzungu. Vilevile wakati wote yeye alikuwa kavaa suti, hata anapokwenda msikiti kwake kusali pale Kipata. Msikiti huu upo hadi leo. Nyumba aliyoacha Kleist sasa haipo na mtoto wake, Ally Sykes amejenga nyumba ya gorofa tano pale. Nyumba hii ndimo alimozaliwa Ally na Abbas na ina historia kubwa kabisa kama ilivyokuwa historia za maisha ya wanae katika historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Hatuwezi kuelezana yote hapa.

iTAENDELEA...


 
Uhuru gani unayouzungumzia Mkuu?, Sisi uhuru wetu wa kumtoa Kibanga Mwizi CCM bado haujatimia siku utakapo timia ndio tutakapokuwa na furaha. Naichukia sisiem mpaka inatia kinyaa. Mambo walioyafanya hwa Mijangili sisiem yanatosha. Tumeibiwa sana na sasa tunasema tumechoka Huyo Uhuru wenu nendeni mkasheherekeeni hukohuko na wajinga wenzenu.
 
Wanaukumbi,

Kuanzia leo Jumatano, 28 Septemba
Mwananchi limeanza "series" zangu na
za waandishi wengine kuhusu Miaka
50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Tusomeni kwa furaha.

Mohamed Said

Uhuru wa Taifa ambalo halipo kwenye ramani ya dunia?
Viongozi wetu wanatumia pesa nyingi kuandaa sherehe
wakati wananchi wanaishi kwenye lindi la umasikini!
Hata hivyo, tunategemea kusoma changamoto nyingi
badala ya kuongozwa na fikra za udini au uchama...

keep it up...
 
Uhuru gani unayouzungumzia Mkuu?, Sisi uhuru wetu wa kumtoa Kibanga Mwizi CCM bado haujatimia siku utakapo timia ndio tutakapokuwa na furaha. Naichukia sisiem mpaka inatia kinyaa. Mambo walioyafanya hwa Mijangili sisiem yanatosha. Tumeibiwa sana na sasa tunasema tumechoka Huyo Uhuru wenu nendeni mkasheherekeeni hukohuko na wajinga wenzenu.

Tutamtoa katika nchi gani, Tanzania au tutarudisha Tanganyika?
 
Suala la kusheherekea uhuru awapelekee watu wenye kufaidika na nchi!! Sisi bado hatujajitawala!!! Utasemaje tunajitawala wakati;
  • kundi moja la majangiri limejipa license to rule milele
  • hata tukijitahidi tutumie sanduku la kura, zinachakachuliwa
  • ukisema basi ujitahidi tu basi utafute maisha yako, hujafanya kitu kwani jamii iliyokuzunguka bado iko mikononi mwa majangiri,
Watu wanaopaswa kufurahia ni kama juzi meeting ya DICOTA, watu wakala wakaserebuka, wenye kulobby wakafanikiwa, wenye kutengeneza mazingira ya kutua kwenye maziwa na asali wakafanikiwa, ali muradi kila mtu alifanikiwa kivyake. Uzuri wao wakitoka hapo wanendelea na maisha yenye amani. Umeme bwerere, maji ndo duh, energy kama kawaida, wakifanya kazi kwa bidii matunda wanayaona.......to name few!!!

Wewe jiangalie hapa, usipoiba huendi popote!!! Na wakikukamata wewe ndo unakuwa mfano wao kuonyesha justice system ilivyokuwa imara...
Uhuru washeherekee wenyewe!! Toka miaka hiyo iliyopita sijawahi kusheherekea iweje leo!!! Ukisema lol, ngoja basi hata nijikumbushe historia yetu...unakuta imepindishwaaaa weeeeee ku-suite matakwa yao, ya nini sasa si basi niendelee tu na utaratibu wa kusubiri kesho, inayokuwaga bora ya jana........
 
msikimbilie kumhukumu mtu kabla hamjasoma makala zake,
kama itatokea zina mlengo wa udini hamlazimishwi kuzisoma...
Una mfahamu Mohammed Said au una msikia tu?
Jamaa anatetea msimamo wake wa kidini kama nini vile.
Utabishana naye page na page kwa vile kwake uhuru ni uhuru wa uislamu dhidi ya dini nyingine na si vinginevyo.
Kama humjui mPM.
 
Mohamed Said ana uhuru wa kuandika makala na kutoa maoni yake kama mtu mwingine yoyote yule

Sidhani kama GREAT THINKERS mtatishwa sana na mawazo na maoni yake. Ame mdini au asiwe mdini

Mwanakijiji alileta series zake hapa za 50 years ya uhuru na the same applies to Mohd Said
 
Mohamed Said ana uhuru wa kuandika makala na kutoa maoni yake kama mtu mwingine yoyote yule

Sidhani kama GREAT THINKERS mtatishwa sana na mawazo na maoni yake. Ame mdini au asiwe mdini

Mwanakijiji alileta series zake hapa za 50 years ya uhuru na the same applies to Mohd Said
Mkuu Great Thinking entails an open mind and not an opinionated inclination of views.
Huyo bwana hautafika mbali sana na yeye kwani yeye si campaighner wa historia tu bali wa historia ya uislamu na uhuru wa Tanganyika.
Nimeliona gazeti alitajalo na sioni kama kuna mtazamo tofauti na yale ayasemayo hapa jamvini ie uhuru wa Tanganyika uliletwa na waislamu.
Period.
 
I am looking forward reading your article as it provides me with the other side of our history hidden by our utopian first leader Nyerere. Just a small advise Sheikh Mohammed Said will you be kind enough to provide us with your way of solving this problem (of religious bias in our society) as it may be useful in the future to provide a foundation of reconciliation structure and way forward to unite our country.
 
Una mfahamu Mohammed Said au una msikia tu?
Jamaa anatetea msimamo wake wa kidini kama nini vile.
Utabishana naye page na page kwa vile kwake uhuru ni uhuru wa uislamu dhidi ya dini nyingine na si vinginevyo.
Kama humjui mPM.

In all his writings, Mohamed Said has maintained that the Muslims were shortchanged by Mwalimu Nyerere after the country gained its flag independence and that now is the time for Muslims to rise up and claim what they believe was their right since 1961!! Jamaa ni mdini zaidi ya DAU wa NSSF!!
 
I am looking forward reading your article as it provides me with the other side of our history hidden by our utopian first leader Nyerere. Just a small advise Sheikh Mohammed Said will you be kind enough to provide us with your way of solving this problem (of religious bias in our society) as it may be useful in the future to provide a foundation of reconciliation structure and way forward to unite our country.


Mdondoaji.
Ahsante kwa mchango wako.

Niandikie: mohamedsaid54@gmail.com Insha Allah nitakuletea fikra zangu kupitia "paper" na mihadhara niliyotoa.

Mohamed
 
In all his writings, Mohamed Said has maintained that the Muslims were shortchanged by Mwalimu Nyerere after the country gained its flag independence and that now is the time for Muslims to rise up and claim what they believe was their right since 1961!! Jamaa ni mdini zaidi ya DAU wa NSSF!!
[1] Catholics form 76% of all members of Parliament the remaining 24% seatsare divided between Christians of other dominations and Muslims. Muslimscontrol a mere 6% of the seats. Most areas which are underdeveloped in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma,Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselvesand are gradually turning into local factions of radical Muslim politicsreminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s. This could be asource of civil unrest in the very near future. Signs of this have begun toshow in the recurrent violent conflicts between Muslims and the government.Tanzania has experienced the Buzuruga Muslim-Sungusungu Conflict (1983), Pork Riots (1993) and MwembechaiUpheaval (1998). For more information See Hamza Mustafa Njozi, Mwembechai Killings and Political Future ofTanzania, Globalink Communications Ottawa, 2000. (The book is banned by thegovernment). In all these conflicts, Muslim blood has been shed. In betweenthese conflicts Muslims have sent several petitions to the governmentrequesting it to look into these problems but all of them have been ignored. Asa result of this Muslims from all regions of Tanzania met in Dar es Salaam atMasjid Tungi in 1990 and issued the Tungi Declaration which among other thingsstated that Muslim should prepare to defend their rights by all means even ifit means by force of arms.

(Nukuu hii inatoka kwenye mswada wangu "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania Mainland." Jamiiforums waliiweka asubuhi na wakaiondoa jioni.)
 
Mkuu Great Thinking entails an open mind and not an opinionated inclination of views.
Huyo bwana hautafika mbali sana na yeye kwani yeye si campaighner wa historia tu bali wa historia ya uislamu na uhuru wa Tanganyika.
Nimeliona gazeti alitajalo na sioni kama kuna mtazamo tofauti na yale ayasemayo hapa jamvini ie uhuru wa Tanganyika uliletwa na waislamu.
Period.

Ahsante kwa mchango wako.

Katika gazeti la Mwananchi la leo kuna makala zangu mbili
na kila moja nimeandika kwa staili yake.

Moja nimezungumzia Tanganyika chini ya Udhamini wa Umoja
wa Mataifa.

Makala ya pili nimejieleza mimi mwenyewe kama mtoto mdogo
wakati wa kupigani uhuru.

Nimeanza kwa kuhadithia nyumba kwa nyumba mitaa ya Gerezani
nilikozaliwa na kukulia nikieleza historia za wazee wangu walivyochangia
katika kupigania uhuru.

Sijui hili la Uislam liko sehemu gani. Tafadhali nifahamishe wapi umeliona.
Nimepitia upya makala hizo sikuona popote neno Uislam.

Mohamed
 
...... Most areas which are underdeveloped in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma,Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselvesand are gradually turning into local factions of radical Muslim politicsreminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s..............

Who are radical muslim Mr Said ?I think dar esalaaam was supposed to be in the list if the author was to be trusted on his view and analysis abut areas with radical muslim.

Otherwise it just show how Mr Saidi is using some statistics without detailed analysis to promote the same radicalism agenda.

 
<br><br>

Thubutu! Huyu ndo muasisi wa udini Zanzibar

Nitashukuru endapo utanifafanulia zaidi ili nipate kukupa jibu ukipenda.

Ila nitakufungulia kwa ufupi ili uongozeke.

Mimi ni Mmanyema wa Dar es Salaam sina uhusiano wowote na Unguja.

Mohamed
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom