Makala za Mohamed Said Katika Mwananchi: Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika

Kuna watu wanafikiri haya mambo yatabaki vivyo hivyo bila uprising .. i don't think so..
Kwa hiyo hapa unatuambia kuwa uprising ni one of your options?
 
Mkuu,

Mohamed analisaidia taifa tena kwa mambo mengi

1. Analisaidia taifa kuangalia historia sahihi na ikiwezekana kuandikwa upya kwa faida ya vizazi vijavyo bila choyo na udini (ukristo)

2. Analisaidia taifa kuangalia utaratibu rasmi wa ubaguzi unaofanywa na maofisa wa serikali kuwapendelea wakristo

3. Analisaidia taifa kuangalia "church" influence kwenye goverment management mfano walipokataa nchi isijiunge na OIC ikawa, kusiwe na mahakama ya kadhi ikawa, ..why so much church influence kwenye mambo ambayo hata hayana affect kama wakristo "mahakama ya waislam maaskofu wasikilizwe it doesn't make sense.."Mfumo kristo" at work. contrary waislamu walitakiwa wasikilizwe zaidi

4. Analisaidi taifa kuangalia huu mgao wa fedha za umma kundeleza kanisa through (MoU) ni ubaguzi na uvunjwaji wa katiba ya nchi ...

Kuna watu wanafikiri haya mambo yatabaki vivyo hivyo bila uprising .. i don't think so..

Topical,

Mwenyezi Mungu akujaze kheri.

Mohamed
 
VITA, VITA, VITA.... Imetangazwa vita baina ya waislamu na wakristu hapa Tanzania???? Bila shaka, somebody is trying to plant a bad seed among us. It is better to stop him before it is too late.........

Haya sasa, wewe ndio unatangaza vita. Sisi tunasema mezani nyinyi kule, sisi huku katikati wapatanishi.
 
FF

Umeona he! wako incompetent hawawezi kujadili zaidi ya kurukia (hamaki)

Of course plus watajadili ni wakati zote ni facts, wanapendelewa, wanaiba fedha za umma kuendeleza kanisa,

Unajua mwizi anavyohamaki
 
Kuna watu wanafikiri haya mambo yatabaki vivyo hivyo bila uprising .. i don't think so..
Kwa hiyo hapa unatuambia kuwa uprising ni one of your options?

Kwanza kabisa inatakiwa Watanzania muikubali hii historia bila kujali itikadi za dini wala siasa. Mkubali kuwa hawa wazee kudhulumiwa kwa kusahauliwa hata kutajwa ni dhulma kubwa juu yao. Mkubali kuwa Masheikh wa Kiislaam kutiwa ndani au kufukuzwa nchini (karibu wote) waliokuwa kwenye harakati za kudai madaraka na usawa kuwa ni dhulma wamefanyiwa.

Kitu cha kwanza, warudishiwe hadhi yao, watambulike kitaifa waombwe na msamaha.

Kitu cha pili tunataka tujuwe uwenye "heri" na utakatifu wa Nyerere kwa jema lipi? Na kwa gharama ya nani?

Halafu tunataka kanisa lifutiwe kabisa fedha wanazopewa kila mwaka na zilengwe kwenye mashule na mazahanati ya Serikali, kwanini zipelekwe kanisani? Kwani hizo kodi ni za Wakristo tu? Suala sio na nyinyi ombeni. Suala ni kwanini ziende makanisani? Wao walipojenga mashule na mahospitali walikuwa wanajuwa au wanategemea kuwa watashindwa kuyaendesha na watayaendesha kwa fedha za Serikali? Kama ndio, kwa idhini ya nani? Huu ni ubaguzi wa hali ya juu. Na Waislaam hatukubaliani nao. Hizo fedha tuone zinakwenda mashule na hospitali za Serikali.

Tumechoka kudhulumiwa kwa miaka 50 sasa toka tupate madaraka, ya kabla ya madaraka ndio yalipelekea wazee wetu kuwa mstari wa mbele kudai madaraka na Historia inathibitisha hilo. Sasa miaka 50 baada ya madaraka tunataka haki sawa. Si lazima sisi tukatibiwe kwenye mahospitali ya Kikristo ambayo kila kitanda tunawekewa masanamu au misalaba ambayo sisi hatuiamini. Leo tukiwa na mgonjwa tutaruhusiwa tulitoe lile sanamu au msalaba na tuweke Aya zetu za Qur'an? Sidhani kama itakubalika au itakuwa busara. Tunataka fedha zetu ziende zikaboreshe mashule ya Serikali ambayo hayatafundisha watoto zetu nyimbo za kanisani.

Tunataka, Nyerere ahukumiwe kwa kulitumikia kanisa badala ya nchi. Kaachia madaraka nchi hohehahe lakini kanisa limenawiri.
 
Kwanza kabisa inatakiwa Watanzania muikubali hii historia bila kujali itikadi za dini wala siasa. Mkubali kuwa hawa wazee kudhulumiwa kwa kusahauliwa hata kutajwa ni dhulma kubwa juu yao. Mkubali kuwa Masheikh wa Kiislaam kutiwa ndani au kufukuzwa nchini (karibu wote) waliokuwa kwenye harakati za kudai madaraka na usawa kuwa ni dhulma wamefanyiwa.

Kitu cha kwanza, warudishiwe hadhi yao, watambulike kitaifa waombwe na msamaha.

Kitu cha pili tunataka tujuwe uwenye "heri" na utakatifu wa Nyerere kwa jema lipi? Na kwa gharama ya nani?

Halafu tunataka kanisa lifutiwe kabisa fedha wanazopewa kila mwaka na zilengwe kwenye mashule na mazahanati ya Serikali, kwanini zipelekwe kanisani? Kwani hizo kodi ni za Wakristo tu? Suala sio na nyinyi ombeni. Sual ni kwanini ziende makanisani? Wao walipojenga mashule na mahospitali walikuwa wanajuwa au wanategemea kuwa watashindwa kuyaendesha na watayaendesha kwa fedha za Serikali? Kam ndio kwa idhini ya nai? Huu ni ubaguzi wa hali ya juu. Na Waislaam hatukubaliani nao. Hizo fedha tuone zinakwenda mashule na hospitali za Serikali.

Tumechoka kudhulumiwa kwa miaka 50 sasa toka tupate madaraka, ya kabla ya madaraka ndio yapelekea wazee wetu kuwa mstari wa mbele kudai madaraka na Historia inathibitisha hilo. Sasa miaka 50 baada ya madaraka tunataka haki sawa. Si lazima sisi tukatibiwe kwenye mahospital ya Kikristo ambayo kila kitanda tunawekewa masanamu au misalaba ambayo sisi hatuiamini. Leo tukiwa na mgonjwa tutaruhusiwa tulitoe lile sanamu au msalba na tuweke Aya zetu za Qur'an? Sidhani kama itakubalika au itakuwa busara. Tunataka fedha zetu ziende zikaboreshe mashule ya Serikali ambayo hayatafundisha watoto zetu nyimbo za kanisani.

Tunataka, Nyerere ahukumiwe kwa kulitumikia kanisa badala ya nchi. Kaachia madaraka nchi hohehahe lakini kanisa limenawiri.
Utakubalije historia iliyoandikwa upande upande? Ni kama vile umepanda gari lenye magurudumu mawili tu. Na hizo dhana za dhuluma ni dhana tu. Mmepewa mifano hapa katika shule nne tulizojengewa na Castro, waislamu wa mwambao hawakuzichangamkia, sasa mnabaki kulalamika tu dhuluma dhuluma. Sasa Nyerere mnataka afufuke ili mmhukumu? Mbona unachekesha hapo. The only way mnaweza kumhukumu Nyerere ni kuhakikisha tuna viongozi ambao watafanya better than he did. Hilo la kufutiwa misaada ya hospitali ya kanisa kazungumzeni na Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kufanya hivyo.
 
Utakubalije historia iliyoandikwa upande upande? Ni kama vile umepanda gari lenye magurudumu mawili tu. Na hizo dhana za dhuluma ni dhana tu. Mmepewa mifano hapa katika shule nne tulizojengewa na Castro, waislamu wa mwambao hawakuzichangamkia, sasa mnabaki kulalamika tu dhuluma dhuluma. Sasa Nyerere mnataka afufuke ili mmhukumu? Mbona unachekesha hapo. The only way mnaweza kumhukumu Nyerere ni kuhakikisha tuna viongozi ambao watafanya better than he did. Hilo la kufutiwa misaada ya hospitali ya kanisa kazungumzeni na Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Jasusi nikuulize,

Historia lazima muikubali nyie ndio iwe historia???? Kwani msikubali tu kuwa mmekosea na hivyo historia iandikwe kwa pande zote hata kama nyie hamuikubali??
 
Utakubalije historia iliyoandikwa upande upande? Ni kama vile umepanda gari lenye magurudumu mawili tu. Na hizo dhana za dhuluma ni dhana tu. Mmepewa mifano hapa katika shule nne tulizojengewa na Castro, waislamu wa mwambao hawakuzichangamkia, sasa mnabaki kulalamika tu dhuluma dhuluma. Sasa Nyerere mnataka afufuke ili mmhukumu? Mbona unachekesha hapo. The only way mnaweza kumhukumu Nyerere ni kuhakikisha tuna viongozi ambao watafanya better than he did. Hilo la kufutiwa misaada ya hospitali ya kanisa kazungumzeni na Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Dhulma siyo dhana kama unavyofikiri....

1. MoU ipo na fedha za umma zinatoka siyo dhana ni facts

2. Mohamed kaandika na evidence (hakuna aliye dispute siyo serikali siyo nani) ambavyo wazee wa kiislam wamedhulumiwa kwasababu ya udini wa nyerere

3. Hiyo ya kuzungumza na JK ni one option ...

Kubwa zaidi iko siku hizo fedha umma na historia sahihi itajulikana kwa hekima au kwa nguvu
 
Jasusi nikuulize,

Historia lazima muikubali nyie ndio iwe historia???? Kwani msikubali tu kuwa mmekosea na hivyo historia iandikwe kwa pande zote hata kama nyie hamuikubali??
Hapana. Sijasema hivyo. Tunachosema ni kwamba historia kama anavyoiandika Mohamed Said ni historia ya ajenda. Mohamed hakuandika historia hii kwa ajili tu ya kumbukumbu ya wazee wake kama anavyosema, lakini pia ameiandika kwa ajili ya kuwaamsha Waislamu ambao anasema wamedhulumiwa na kuonewa licha ya kwamba walishiriki katika harakati za uhuru. Haya, Mohamed kishaandika upande wake, sasa mbona hamjaridhika? Vitabu vyake vinasomwa kama njugu, kama anavyosema mwenyewe, anaitwa kutoa mihadhara/minakasha ulimwenguni kote hata katika nchi zisizo za Kiislamu na bado mnaona kuna tatizo. Hapo ndipo tunapotufautiana. Lakini twende sote taratibu, tutafika tu.
 
Hapana. Sijasema hivyo. Tunachosema ni kwamba historia kama anavyoiandika Mohamed Said ni historia ya ajenda. Mohamed hakuandika historia hii kwa ajili tu ya kumbukumbu ya wazee wake kama anavyosema, lakini pia ameiandika kwa ajili ya kuwaamsha Waislamu ambao anasema wamedhulumiwa na kuonewa licha ya kwamba walishiriki katika harakati za uhuru. Haya, Mohamed kishaandika upande wake, sasa mbona hamjaridhika? Vitabu vyake vinasomwa kama njugu, kama anavyosema mwenyewe, anaitwa kutoa mihadhara/minakasha ulimwenguni kote hata katika nchi zisizo za Kiislamu na bado mnaona kuna tatizo. Hapo ndipo tunapotufautiana. Lakini twende sote taratibu, tutafika tu.

Sasa ulitaka waislam wasiamshwe walale milele muendelee kunyonya na kubagua watu kwa ajili ya dini yao? duh
 
If that is the case then bring it on!


Jasusi,

Unahamaki achana na hawa dot.com sisi humu ukumbini ndiyo watu wazima.
Tuuongoze huu mnakasha hadi tuuhitimishe salama.

Katu hatutoweza kumlipa JF kwa hii hisani anotufanyia kutukutanisha hapa jamvni na tukafanya mnakasha.
Nuksani isiwe ndiyo jaza yake.

Ihsani malipo yake ni ihsani.
Tumlipe wema JF kwa wema anotufanyia na hakuna wema utakaompendeza kama kuona mijadala ya kisomi inashamiri.

Mohamed
 
Mohamed Said;2697795] Catholics form Most areas which are underdeveloped in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma,Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselvesand are gradually turning into local factions of radical Muslim politicsreminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s. This could be asource of civil unrest in the very near future
Mohamed Said;2717867]Mwanakijiji, serikali haijakubali kuwa tuna tatizo. Hadi watakapokiri na kutaka ushauri kipi kifanyike hapo ndipo tutazungumza . Kwa sasa tujikite katika kuisihi serikali iamke tuiepushe nchi yetu na vurugu
Mohamed Said;2725399]MM,Wako wanaokimbia humu ukumbini lakini mimi sijapata na Insha Allah Mungu asinijalie kukimbia vita,Hilo ni moja katika makosa makubwa sana katika Uislam[
]Mohamed Said;2697795Ndugu zangu haya yote yaliyo humu ukumbini kuhusu dhulma dhidi ya Waislamu siku moja yatakuwa ndiyo ushahidi wetu ama tuko African Union (AU) au United Nations (UN)endapo kama baadhi ya watu wanavypenda kusema, tutakuwa "ignored" maana yake sisi hatuwezi kukubali hali hii iendelee daima. Serikali zote duniani zinajua hatari yake.Subirini zitakuja nchi hii kamisheni kuja kuchunguza ukweli. Siku hizi hawasubiri mpaka vita ianze kama Rwanda ndiyo waje. Kuwa leo tunamkabili dhalim waziwazi kwetu ni ushindi mkubwa sana.Mohamed
Mwita Maranya;2730674]sheikh mohamed pamoja nanyi wafuasi wake mmekuwa mkitoa vitisho kama mnavyojaribu kuwabrand wengineKama ni sifa, hizo ulizotaja aidha ni nzuri ama ni mbaya, hata ninyi mnazo kwahiyo hakuna hoja hapo
Mkandara;2730774]Mdondoaji, unajua hata wao wanaweza kusema vivyo hivyo. Tatizo ni kwamba mnashindwa kujitazama nyie wenyewe kuwa you are incompetent na mabandiko mengi yaliyomo humu ni vitisho vitupu toka pande zote. Mnazungumzia vita inakuja, sijui waislaam wameona mwanga sasa hawatakubali tena kuonewa wakati chombo kilichosimamisha bendera ni serikali na nyie wenyewe ndio wanachama wa chama tawala
Mwita na Mkandara, ahsanteni sana kwa busara zenu!
Chanzo cha nukuu zangu ilikuwa kujibu hoja ya Mohamed kuhamasisha vita na kukana hajasema hilo neno. Nimeonyesha kuwa amesema na kwenda mbali kuonyesha nia aliyo nayo. Hivi mtu anaposema Subirini zitakuja kamisheni kuchunguza, anaposema utakuwa ushahidi UN au AU watakapokuja,anaposema 'mpaka vita ianze' na anaposema waislam ni kosa kukimbia vita akinasibisha na neno na ukatoliki na serikali ana maana gani.

Narudia Mohamed ametoa kauli za vitisho akizihusisha na vita. Nimewekea ushahidi hapo juu. Kutangaza vita na kuhamasisha vita ni vitu viwili tofauti na mimi nasema anachagiza vita. Anayekana hayo si maneno ya Mohamed aseme ili nipakue mzigo uliobaki!

Nimefunga mjadala wa hili kwasababu lipo wazi na wenye akili zao wanaliona kwa uwazi.
Turudi katika uchambuzi wa makala zake kwa mitazamo mbali mbali yenye tija kwa taifa na wasomaji
 
Mkandara,

Heshima mbele mkuu mie nawaelewa ndugu zetu ila vile vile naelewa elimu ya majadiliano. Technic inayotumika na baadhi yetu kutafuta mapungufu ina walakini kwasababu haujengi mjadala badala yake unauharibu. Mie nishamueleza mfano Mwanakijiji kuwa ukiwa ndani ya box kujua yaliyo nje ya box ni vigumu na tabu. Why asivae viatu vya waislamu akatembea navyo akajua nini kinaendelea. Mie nilikosa nafasi ya kuendelea kusoma serikalini kwasababu ya jina langu. Faiza foxy pia alikosa nafasi ya kusoma serikalini kwakuwa jina lilikuwa tatizo. Wazee wangu wengine walilazimika kubadilisha majina ili wasome. Wengine walisoma hadi mafundisho kanisani ili mradi wapate elimu. Hivyo suala la mistreatment against muslims lipo na Mwanakijiji hawezi kulipinga. Hata hivyo mapungufu ya waislamu nayo yapo na yamechangiwa zaidi na grievance ambayo waislamu wanayo dhidi ya Bakwata. Mfano shule ya Kinondoni imekuwa ikifelisha na wanafunzi hawafanyi vizuri kwasababu hakuna mwislamu anataka kujiweka upande wa Bakwata. Bakwata imebakia baraza la maulidi, mwandamo wa mwezi na matamko tu. Shule ya Ubungo Islamic, Mzizima, Feza, Al-Muntazir zimekuwa zinafanya vizuri sana katika matokeo ya wanafunzi wake kwakuwa zimekuwa zikisimamiwa na waislamu wenyewe bila ya mikono ya Bakwata. Hivyo utaona kuna tatizo katika vitu vinavyosimamiwa na Bakwata na sio taasisi zengine.

Kauli za vitisho hakuna mtu ametoa kauli za vitisho. Watu wamechukua maneno yao na kuyafanya maneno ya Mohamed Said. Mohamed hakusema kunakuja vita bali amesema hali hii ikiendelea inaweza kusababisha vurugu kwa mujibu wa maono yake na utafiti alioufanya. Je amesema kitisho gani hapo zaidi ya kusema ukweli. Kumbukeni ndugu zanguni kuwa an unjust society is a society of lawlessness. Wananchi wakiona sheria ziko kuwafavor watu wa aina fulani resistance huchipukia hapo hapo. Je kuendelea huku kwa waislamu kufanywa second class citizen hauoni kunapelekea kuwepo kwa fukuto la moyo miongoni mwa waislamu?

Halafu kuna mambo yanachangia pia kuleta kupotea kwa hali ya uaminifu. Mfano MoU ya Kanisa na Serikali. Serikali inawalipa Kanisa Bilioni 91 kila mwaka kutoka katika kodi za waislamu na wakristo. Je waislamu wanagaiwa ngapi? Kuna mtu anaweza kutuambia MoU ya Serikali na Aga Khan serikali ilikuwa INATOA KIASI KWA TAASISI ZA AGA KHAN KILA MWAKA???? Huu ni ufisadi na unapelekea waislamu nao waulize mustakabali wa kodi zao vp?????
Shukran sana kwa mjadala wenye maana na ndio sababu napenda sana kujadiliana na wewe kwa sababu unatafuta suluhu ya tatizo unaloliona na sii kutafuta mchawi kumtangaza hali anaendelea na uchawi...

Ningependa sana kuelewa wewe ulikosa vipi elimu na umeweza vipi kuipata maanake tupo waislaam wengi sana tulosoma enzi ya mwalimu na tumefaidika na mabadiliko aliyoyafanya. pengine elimu yako umeikosa wakati wa Mwinyi au Mkapa na hi sintoshangaa isipokuwa kwa uhakika nimekufahamisha huko nyuma matatizo ya kielimu aliyopambana nayo mwalimu. Na kati ya wazee wako wlaiopata taabu nimesema mimini mmoja wapo na hakika nimefaidika na kutaifishwa kwa shule, lakini nimetukanwa kwa sababu nilikuwa nilitumia jina la Kikristu kuweza kusoma ktk shule za kikatoliki..Sikujibu nimekaa kimya kwa sababu mtukanaji hakutaka kujadili isipokuwa matusi yamemkaa kinywani na hana haya...

Mkuu wangu, ni vigumu sana kuchukua kati ya wananfunzi wote asilimia 5 kuendelea na masomo ya form 1 kutokana na uchache wa shule na walimu halafu ni gumu zaidi kuchukua wananfunzi asilimia 1 kuendelea ma masomo ya vyuo vikuu bila shaka kwa mtu yeyote unaweza kusema lolote lile. Binafsi naelewa mfduko kristu ulikuwepo kabla ya Uhuru na hakuuanzisha mwalimu isipokuwa mwalimu aliupiga vita na ndio maana tukataifisha mashule yote ya taasisi za kidini.. Kwa hilo wengi waliliona kosa kwa sababu elimu zao zinawafundisha kwamba ubepari ni pamoja na kuweka elimu mikononi mwa watu na sio serikali... Hii sio kweli na haijawa ubepari isipokuwa ni upotoshaji kuifanya elimu sii haki ya mwananchi isipokuwa ni previlege..

Sasa unapoondoa serikali ktk mamlaka ya kusimamia elimu na uendeshaji wake ukaviweka mikononi mwa serikali kwa mtazamo ule ue wa biashara ina maana hata elimu haihitaji regulations zinazowabana waendesha biashara. Na huwezi kumlazimisha mtoa elimu a target watu gani isipokuwa yeye anatazama biashara yake itauzika wapi zaidi na ktk standard iliyowekwa..Na matokeo ya mfumo huu utawapa nafasi zaidi wale wenye kipato kupata elimu bora zaidi ya wale wasiokuwa na kipato.

Na kwa bahati mbaya waislaam ndio wengi maskini kuliko wakristu ktk mikoa ya Pwani lakini kwa ujumla mimi nadhani Wakristu maskini ni wengio zaidi ya Waislaam kwa sababu wengi takwimu zinaonesha wazi kwamba umaskini upo zaidi vijijini ambako kuna asilimia kubwa ya wananchi na mara nyingi waislaam hawaishi vijijini.. Hivyo, tunapozungumzia umaskini nadhani swala hili siii la waislaam pekee isipokuwa Taifa zima wote tunanyimwa elimu bora kwa kutokana na hizo shule za kata ambazo hazina walimu na vifaa vya kufundishia. Unjust society sii ya waislaam pekee ni kwa wananchi wote kutokana na hivyo unapata lawless society...

Sheria zipo kuwa favor wenye kipato, haijalishi wewe mkristu au Muislaam kwa sababu leo hii huwezi kusoma na mtoto wa JK, Lowassa, Mwinyi au Mkapa, Rostam na wengineo wakubwa ndani ya chama CCM, hawa wote wanapewa special treaties hata hospital zao ni nje ya nchi tofauti na wewe au mMwanakijiji.. Kwa hiyo unapotumia lugha ya Udini na advantage wanazopewa Wakristu wakati Mwanakijiji au Jasusi wanaelewa kwamba they struggle hard to get education wakati ni wakristu ndio maana hawawezi kukubaliana na mawazo yako. Kama wao wangekuwa mfanoi wa madai yetu ingeweza kabisa kuobnekana lakini sote tunasota!.. inakuwaje Mkristu aliyependelewa na serikali ya Nyerere leo hii awe na maisha duni sana na yako wakati yeye anaona wazi kabisa kwamba watoto wa viongozi wa CCM wote waislaam kwa Wakristu wakila bata..


Na ndio maana nikasema Unjust ipo ktk uongozi wa serikali ya CCM na nakubaliana sana na mawazo yako isipokuwa unayatazama kwa viatu ulovaa wewe muislaam bila wewe pia kuvaa viatu vya mkristu ambaye hana refa CCM. Na maadam sisi sote tumeishi na tunaendelea kuishi tanzania kwa nini hatutaki kukubali kwamba CCM ndiye mgonvi wetu, kwa nini tunataka sana kulaumiana sisi ambao wote ni victim wa mfuko huo huo Kristu ambao hakika unawapendelea ndugu na watoto wa viongozi wetu kiasi kwamba leo hii wamepangana kupokezana madaraka ndani ya chama hicho. Na pengine hata hiyo mikataba ya MoU na AghaKhan ni kwa sababu ya watoto wao wapate elimu bora ama walichukua asilimia 10 kuwezeshwa..
 

Jasusi nani mdini?

Aliyeshika madaraka 83% au huyu wa 17%.
Mbona unawajibia waliotuhumiwa si tumeeleza dhulma zote hadharani mbona hawathubutu kufungua mdomo kukanusha?

Kama Waislam ndiyo wadini wanamdhulumu nani na kwa njia zipi?

Au kusema kuwa Waislam wanadhulumiwa ndiyo udini wenyewe?

Tafadhali usilijibie Kanisa litie hima wajibu tuhuma za Waislam.

Huo ndiyo uungwana.


Mohamed

kanisa halina muda wa kujibu upuuzi huu wapo serious kuleta maendeleo ya nchi na kumwondolea mtanzania lundo la umaskini
 
CCM inahusu nini hapa? angalia wengine hawa, hata pakutokea hawapajui. Usitupeleke huko. Unanchekesha.

FF
Wala usipate shida,wenzio wametumwa na chama cha kanisa,ndio maana wanataka kuharibu mad kwa porojo zao za siasa.Waanzishe mada nyingine ya siasa hizo tutachangia!
 
Na miye niweke 50 cents zangu.

Alichoandika Bw. Said kwenye simulizi la kila ambacho anakiita "historia" kwa kweli siyo historia kwa maana ambayo inakubalika. Ndio maana toka mwanzo wa mnakasha huu nimekuwa nikiuliza maswali ambayo yanahusiana na ukusanyaji wa taarifa mbalimbali. Napenda zaidi maana ya neno "history" inavyotolewa kwenye wikipedia - History (from Greek ἱστορία - historia, meaning "inquiry, knowledge acquired by investigation"[SUP][2][/SUP]) is the discovery, collection, organization, and presentation of information about past events. History can also mean the period of time after writing was invented.

Kamuni ya "The Pocket Webster School & Office Dictionary" inasema kuwa "history" ni a. A narration or description of facts and events arranged chronologically with their causes and effects. b. A knowledge of facts c. all of the known past and d. A scientific study of the past.

Kumbe historia siyo simulizi kama hadithi. La hasha! Historia ni somo linaloongowa na kanuni za kisayansi na kanuni ya kwanza kabisa ni kuwa objective. Manake nini? Maana yake ni kwamba unapoenda kuangalia matukio ya nyuma unakuwa huru kutoka katika biases zako, stereotypes zako na kwa hakika kabisa kuzigundua hivyo vikwazo vya kuwa objective. Hapa ndipo tunapokutana na kosa kuu kabisa la mzee wetu.

Bw. Said hakuisogelea historia katika mwanga wa mtu ambaye ni objective. Alisimuliwa maneno na wazazi wake, aliyaona mambo kadha wa kadha akiwa na umri mdogo, na kwa bahati mbaya sana alikulia na kufundishwa chini ya wale ambao waliamini kabisa kuwa Nyerere alikuwa ni mdini toka siku ya kwanza anaingia Dar. Hivyo anapokua na kupata Ilimu tayari ameshajengewa hisia hii kutokana na masimulizi mbalimbali. Mara kwa mara hurudia kutuambia jinsi alivyosimuliwa na "wazee" wake. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.


Kosa lake la pili mzee wetu ni kuwa alipoanza kufanya utafiti hakuwa anafanya utafiti ili kuwathibitisha wazee wake au kuwakanusha. Hakuwa anafanya utafiti ili kujua ukweli wote kabla ya kujenga maoni yake. Badala yake yeye alienda kuangalia historia ili kuthibitisha kile ambacho alishaaminishwa tangu akiwa kijana mdogo hadi leo hii. Hivyo, chochote ambacho angekutana nacho kinyume na kile alichosimuliwa alikiweka pembeni. Na matokeo yake ni kuwa simulizi zima halihusiani na historia hata kidogo linahusiana na MAJINA YA WAISLAMU.

Umenisoma vizuri.

Bw. Said kwa kweli hajali kabisa kama hao wanaoitwa "waislamu" wa wakati ule walikuwa kweli wanashika dini au wanaitwa tu kwa majina. Hilo kwake si hoja hata kidogo. Alipofanya utafiti alipoona jina la Kiislamu alihitimisha ni "MUislamu" na hivyo hata kama watu hao kihistoria walikuwa hawashiki dini au hata kufuata imani ilivyo yeye kwake haikuwa hoja alimradi tu wale walijiita "Waislamu" sasa hiki ukiangalia ni kigezo kidogo sana kukifikia. Nguruvi ameonesha mahali fulani hapa - kwamba Bw. Said anatumia majina ya Waislamu kuwapa watu "Uislamu" lakini ikija kwenye BAKWATA au mtu mwingine yeyote anayempinga ambaye anajina la Kiislamu kipimo chake hicho hukitupa mbali. Anaingiza kipimo kingine kabisa nacho ni "kukubaliana nasi". Yaani, Muislamu ambaye anaampinga si Muislamu ila yule wanayekubaliana naye. Matokeo yake kwake BAKWATA haiwezi kuwakilisha maslahi ya Waislamu kwa sababu hata kama wote waliomo mle wanaamini katika Uislamu; wanamuamini Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na Mshirika na wanaamini kuwa ni Mtume Mohammed (SAW) ni mjumbe wake.

Hili linashangaza. Hakuna kipimo chochote kingine cha Muislamu zaidi ya imani yake katika mambo haya mawili ya msingi na mengine yanayotokana na hayo. Hakuna siasa, hakuna rangi, hakuna uanachama wa chama fulani n.k

Hata hivyo kosa la tatu ambalo linavunja kabisa hii dhana kuwa anachosimulia ni historia ni kuwa haandiki ili kuwaleta watu pamoja kuweza kufahamu ukweli . Nina bahati kuwa nimesoma maandishi yake mengi sana na katika yote yeye anazungumzia ugomvi kati ya Waislamu na Wakristu au kati ya Uislamu na Kanisa. Na katika hili kwa kweli amefanikiwa sana. Siyo kuwaamsha Waislamu bali kuwapotosha watu kuamini kuwa adui yao ni Kanisa! Hazungumzii umaskini, magonjwa na ujinga uliokithiri kati ya watu wetu - Waislamu, Wakristu na Wapagani; hazungumzii matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zinatokana na kodi za walio BAKWATA NA wale walio nje ya BAKWATA; hazungumzii haja ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yatawaleta wananchi wetu pamoja kuubomoa na kuuvunjilia mbali mfumo wa utawala wa kifisadi. Anachofanya yeye ni kuwafanya baadhi ya Waislamu - na inasikitisha wapo ambao wanamini -kuwa adui yao ni Kanisa!

Matokeo yake ni kweli wapo watu wanalichukia kanisa katoliki; wapo watu ambao wanachukia hata Wakristu kwa sababu ya mafundisho ya Bw. Mohammed. Ndio nikaonesha juzi kwamba anachofanya ni kinyume hata na mafundisho ya Qurani. Analeta faraka siyo tu kati ya Waislamu na Waislamu (wale wa BAKWATA NA WALE NJE YAKE) bali pia faraka kati ya wanadamu tulioumbwa na Mwenyezi Mungu ili "tujuane" siyo tuchikiane, tuogopane au hata tudhulumiane. Angekuwa kweli kabisa lengo lake ni kutafuta umoja na ukweli asingedai kuwa ameandika kwa ajili ya "kuwatuhumu" watu fulani.

Na hata kama angetaka kutuhumu watu basi tungeona kweli kabisa angejiunga na wengine na kuleta mashtaka Mahakamani.

Bw. SAid na wale wanaoamini kuna mfumo Kristu wangeweza kabisa kuleta hata kesi mahakamani. Kushtaki Baraza la Maaskofu Katoliki kwa kuwa wanafanya ubaguzi. Wangeweza kufungua mashtaka dhidi ya Wizara ya Elimu ili kuonesha kuwa inafanya kazi kibaguzi. Hadi leo hii hakuna kesi hata moja iliyowahi kufunguliwa dhidi ya kanisa au serikali au hata mtu yeyote mwingine kudai kuwa kuna watu wanabaguliwa. Nilimuambia mtu mmoja juzi humu humu ambaye alidai kuwa kuna ubaguzi wa kidini NSSF - nikasema kama yeye ni mwathirika leteni mashtaka.

Sitaraji kama kuna mtu yeyote upande wa Bw. Said ambaye anaweza kuleta mshtaka nchini ya kudai kuwa Waislamu wanadhulumiwa. Hakuna ushahidi unaoweza kusimama mahakamani wa jambo hilo. NONE. Wapo ambao wanapenda uwepo ushahidi ili waweze kusema "tuliwaambia" lakini kwamba kuna ushahidi unaoweza kuoneshwa wa mfumo rasmi wa kibaguzi wenye kupendelewa Wakristu (mfumo kristu) haupo.

Kwa hiyo, kwa ufupi mjadala huu unatuonesha tu hatari tuliyonayo kama taifa. Hasa uwepo wa watu ambao wanaamini yanayodaiwa bila kuuliza. Mwanahistoria wa Kiarabu aliyeishi 1337 Ibn Khaldun - ambaye anatajwa kama Baba wa Sayansi ya Historia na mmoja wanafalsafa wa hali ya juu toka katika Ulimwengu wa Kiislamu - aliandika kuhusu makosa saba ambayo waandishi wa historia wanayafanya. Lakini kwa sehemu hii itoshe kunukuu maneno yake ni kukosoa kile aliachokiita "idle superstition and uncritical acceptance of historical data" kama mojawapo ya makosa ya wanahistoria.

Tumeona humu wapo watu ambao hawataki kuuliza maswali sahihi kwa sababu majibu yake yanavunja hoja zao. Matokeo yake ni kuwa watu wanakubali bila kupatiwa uhakika na hasa vijana ambao huenda kumsikiliza nawaonea huruma kwa sababu wengi wanajikuta wanaamini kile lisemwalo kwa sababu aliyelisema anatumia authority ya kuwa amezungumza sehemu nyingi duniani, anakubalika na majarida mbalimballi duniani. For untrained minds hii ni authority tosha. It is sad that some people among "great thinkers" wako hivyo hivyo. Wanakubali kitu wanachoambiwa bila kukihoji kwa sababu tayari wanakiamini.

Kwa hiyo, tafuteni kazi za Bw. Said mzisome lakini mkae mkijua hamsomi historia bali masimulizi ya kijana kuhusu wazazi na wazee wake. Mtu anayesoma akiamini anasoma historia hatuna jinsi ya kumsaidia bali kumuonea huruma.
 
Back
Top Bottom