TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,718
- 10,214
Dar es Salaam. Makaburi zaidi ya 600 yaliyopo katika kata ya Kipunguni yanatarajiwa kuhamishwa ili kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).
Mchakato wa kuhamisha makaburi hayo unafuatia mpango wa ulipaji fidia kwa wakazi 1,865 wa eneo hilo wanaotakiwa kuhama kupisha upanuzi wa uwanja huo.
Akizungumzia mchakato huo, Ofisa Afya Mkuu Jiji la Dar es Salaam, Salim Musya alisema serikali inaendelea na utaratibu wa kulipa fidia kwa wakazi hao mpango unaosimamiwa na Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA).
"Katika eneo hili ambalo wakazi hawa wanatakiwa kupisha kuna sehemu nane za makaburi ya familia na makaburi ya jumuiya zikiwa sehemu mbili," amesema.
Mwinjuma Seke ambaye ni Mwenyekiti Mtaa wa Kipunguni amesema ili kufanikisha zoezi hilo wametoa miezi mitatu kwa ndugu kujiandikisha.
"Zoezi hili litakamilika rasmi Desemba 1, 2023," amesema Seke.
Ramadhani Kinyaiya ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanagati sehemu ambako makaburi hayo yatahamishiwa amesema tayari wameshaanza kufanya usafi kwa ajili kuandaa eneo la kuzikia watu hao.
Hii inakuwa ni mara ya pili Mwanagati kupokea makaburi yanayohamishwa ikiwa ni baada ya kupokea makaburi mengine 378 kutoka Vingunguti.
Akizungumzia suala hilo, Mohammed Abdallah ambaye ni moja ya watu waliozika ndugu katika makaburi ya Kipunguni Mashariki amesema wamepokea suala hilo kwa mikono miwili.
Daud Peter ambaye ni Mkazi wa Kipunguni pia amesema anasikitishwa na hatua hiyo lakini ni hatua nzuri.
"Mchakato hatujaukataa tumeupokea kiroho safi,"
Eneo hilo 1995 lilitangaza kufanyiwa tathmini ya kwanza ili wananchi walipwe fidia lakini haikufanikiwa hadi tathmini nyingine ilipofanyika mwaka huu.
Mshana Jr kuna chochote tunaweza kubeba cha kutufaa?
Mchakato wa kuhamisha makaburi hayo unafuatia mpango wa ulipaji fidia kwa wakazi 1,865 wa eneo hilo wanaotakiwa kuhama kupisha upanuzi wa uwanja huo.
Akizungumzia mchakato huo, Ofisa Afya Mkuu Jiji la Dar es Salaam, Salim Musya alisema serikali inaendelea na utaratibu wa kulipa fidia kwa wakazi hao mpango unaosimamiwa na Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA).
----"Katika eneo hili ambalo wakazi hawa wanatakiwa kupisha kuna sehemu nane za makaburi ya familia na makaburi ya jumuiya zikiwa sehemu mbili," amesema.