Makaburi 1500 kuhamishwa kupisha ujenzi SGR

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,652
makaburi-pic.jpg

Mwanza. Makaburi takribani 1,500 ya Waislamu yaliyoko Mtaa wa Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza yameanza kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga na kupelekwa katika makaburi ya Nyashana kata ya Isamilo jijini humo.

Mchakato wa uhamishaji wa makabuli hayo ulianza Desemba 18, 2022 na kutarajiwa kuhitimishwa makaburi hayo yatakapoondolewa yote ambapo hadi kufikia leo Desemba 23 mwaka huu mabaki ya miili 198 ilikuwa imeshafukuliwa na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Nyashana jijini Mwanza.

Rehema Haroun ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu aliyezikwa katika makaburi hayo, ameeleza kuridhishwa na ufukuaji wa miili ya wapendwa wao huku akiziomba mamlaka kuendelea kuongeza umakini ili kuepusha mkanganyiko wa utambuzi wa miili hiyo.

Rehema ametaja changamoto iliyoibuka katika shughuli hiyo kuwa ni pamoja na watu zaidi ya watatu kudai waliwazika wapendwa wao katika eneo lenye kaburi moja.

Mmoja wa wafukuaji wa makaburi ya yaliyoko Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza akiwa amebeba jeneza lenye mabaki ya mwili wa mtu aliyezikwa katika eneo hilo. Picha na Mgongo Kaitira

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

"Kuna kaburi unakuta watu wawili wanadai mtu wao amezikwa hapo, sisi hatupingani na zoezi hili la kuwahamisha wapendwa wetu lakini tunaomba wataalamu waongeze umakini ili kutusaidia kutambua mabaki ya ndugu zetu," amesema Rehema.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Ramadhani Hamisi amesema mwili wa mdogo wake aliyefariki na kuzikwa mwaka 2018 umepatikana japo yamekutwa mabaki ya miili ya watu zaidi ya wawili katika eneo moja.

"Haya makaburi yanaonekana kuanza kitambo kidogo, ndiyo maana si ajabu kukuta katika sehemu inayoonekana kuna kaburi moja ukakuta mabaki ya miili hata miwili au zaidi, muhimu ni kutambua mwili wa mpendwa wako ulipopumzishwa," amesema.

Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa SGR Mwanza-Isaka kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Blasius Mwita amesema tathmini ya haraka iliyofanyika katika eneo hilo inakadiliwa kuna makaburi takribani 1,500.

Mhandisi Mwita amesema kila mwenye ndugu aliyezikwa hapo atalipwa Sh300,000 kama kifuta machozi baada ya shughuli ya kuyaamisha kukamilika huku akisisitiza kuwa fedha hiyo itaongezeka endapo kaburi lilikuwa limeboreshwa ikiwemo kujengewa vigae.

"Haturuhu wafiwa kufika hapa kwani itaibua kilio bali tunahitaji wawakilishi wa familia ambao watashuhudia mabaki ya wapendwa wao yakiondolewa lengo ni kuhakikisha utaratibu unafuatwa, baada ya kukamilisha kuyahamisha tutapeleka majina ya waliokutwa hapa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili kulipwa kifuta machozi," amesema mhandisi huyo

Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sophia Kiluvia amesema shughuli ya kuhamisha mabaki ya miili ya watu waliozikwa katika eneo hilo inafanyika kitaalam ili kuhakikisha hakuna mwili utakaosalia katika eneo hilo.

Pia amesema wanazingatia taratibu zote za kuanzia kuchimba kabuli, utambuzi wa miili iliyozikwa katika eneo la kabuli husika, kusafirishwa hadi makabuli ya Nyashana na kuzikwa kwa mara nyingine.

"Tupo hapa kuhakikisha taratibu zote za kiafya zinazingatiwa, wanaofukua hawapati madhara kiafya, ndugu wa marehemu wanakuwa salama hata wakazi wa eneo hili hawaathiriki na shughuli hii, tunazidi kuomba watu wenye ndugu waliozikwa hapa waendelee kujitokeza," amesema Sophia

Naye, Mwakilishi wa Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata) wilaya ya Nyamagana, Juma Malijani amesema eneo hilo lililoanza kutumiwa na Waislamu miaka 76 iliyopita, lilikuwa likitumiwa na waumini wa Kiislamu kutoka Msikiti wa Lukumani, Johari, Ghazari na Shede iliyoko katika kaya hiyo.

Pia, amewataka watu wenye ndugu waliozikwa katika eneo hilo kitotumia shughuli hiyo kama kitega uchumi na kusema hakuna fedha inayoweza kuthaminishwa na binadamu hivyo akawataka kujitokeza kwa wingi.

"Natambua kuwa wapo watu ambao wanasita kuja kushuhudia mabakinya ndugu zao yakiondolewa wakishinikiza kuongezewa hela, niseme tu hii siyo fidia bali ni kifuta machozi kwani hakuna pesa inayoweza kuthaminishwa na binadamu, tujitokeze kuwapumzisha ndugu zetu," amesema Malijani ambaye pia ni Shehe.

Mwananchi
 
Yaaani hapo kwenye pesa ndio macho yote yapo hapo,
Mwingne hata kwenge mazishi hajaja ila pesa lazima aifuatilie, sasa pesa haitoshi kivipi?
Na kwa waislamu ni tofauti na wakristo kuna msalaba wenye jina, hii kweli itakua kazi kutambua.

Hapo mtu anang'ngania maiti hata haijui ili tuu 300k
 
Makaburi takribani 1,500 ya Waislamu yaliyoko Mtaa wa Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza yameanza kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga na kupelekwa katika makaburi ya Nyashana kata ya Isamilo jijini humo.

Mchakato wa uhamishaji wa makabuli hayo ulianza Desemba 18, 2022 na kutarajiwa kuhitimishwa makaburi hayo yatakapoondolewa yote ambapo hadi kufikia leo Desemba 23 mwaka huu mabaki ya miili 198 ilikuwa imeshafukuliwa na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Nyashana jijini Mwanza.

Rehema Haroun ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu aliyezikwa katika makaburi hayo, ameeleza kuridhishwa na ufukuaji wa miili ya wapendwa wao huku akiziomba mamlaka kuendelea kuongeza umakini ili kuepusha mkanganyiko wa utambuzi wa miili hiyo.

Rehema ametaja changamoto iliyoibuka katika shughuli hiyo kuwa ni pamoja na watu zaidi ya watatu kudai waliwazika wapendwa wao katika eneo lenye kaburi moja.

Mmoja wa wafukuaji wa makaburi ya yaliyoko Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza akiwa amebeba jeneza lenye mabaki ya mwili wa mtu aliyezikwa katika eneo hilo. Picha na Mgongo Kaitira
"Kuna kaburi unakuta watu wawili wanadai mtu wao amezikwa hapo, sisi hatupingani na zoezi hili la kuwahamisha wapendwa wetu lakini tunaomba wataalamu waongeze umakini ili kutusaidia kutambua mabaki ya ndugu zetu," amesema Rehema.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Ramadhani Hamisi amesema mwili wa mdogo wake aliyefariki na kuzikwa mwaka 2018 umepatikana japo yamekutwa mabaki ya miili ya watu zaidi ya wawili katika eneo moja.

"Haya makaburi yanaonekana kuanza kitambo kidogo, ndiyo maana si ajabu kukuta katika sehemu inayoonekana kuna kaburi moja ukakuta mabaki ya miili hata miwili au zaidi, muhimu ni kutambua mwili wa mpendwa wako ulipopumzishwa," amesema.

Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa SGR Mwanza-Isaka kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Blasius Mwita amesema tathmini ya haraka iliyofanyika katika eneo hilo inakadiliwa kuna makaburi takribani 1,500.

Mhandisi Mwita amesema kila mwenye ndugu aliyezikwa hapo atalipwa Sh300,000 kama kifuta machozi baada ya shughuli ya kuyaamisha kukamilika huku akisisitiza kuwa fedha hiyo itaongezeka endapo kaburi lilikuwa limeboreshwa ikiwemo kujengewa vigae.

"Haturuhu wafiwa kufika hapa kwani itaibua kilio bali tunahitaji wawakilishi wa familia ambao watashuhudia mabaki ya wapendwa wao yakiondolewa lengo ni kuhakikisha utaratibu unafuatwa, baada ya kukamilisha kuyahamisha tutapeleka majina ya waliokutwa hapa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili kulipwa kifuta machozi," amesema mhandisi huyo

Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sophia Kiluvia amesema shughuli ya kuhamisha mabaki ya miili ya watu waliozikwa katika eneo hilo inafanyika kitaalam ili kuhakikisha hakuna mwili utakaosalia katika eneo hilo.

Pia amesema wanazingatia taratibu zote za kuanzia kuchimba kabuli, utambuzi wa miili iliyozikwa katika eneo la kabuli husika, kusafirishwa hadi makabuli ya Nyashana na kuzikwa kwa mara nyingine.

"Tupo hapa kuhakikisha taratibu zote za kiafya zinazingatiwa, wanaofukua hawapati madhara kiafya, ndugu wa marehemu wanakuwa salama hata wakazi wa eneo hili hawaathiriki na shughuli hii, tunazidi kuomba watu wenye ndugu waliozikwa hapa waendelee kujitokeza," amesema Sophia

Naye, Mwakilishi wa Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata) wilaya ya Nyamagana, Juma Malijani amesema eneo hilo lililoanza kutumiwa na Waislamu miaka 76 iliyopita, lilikuwa likitumiwa na waumini wa Kiislamu kutoka Msikiti wa Lukumani, Johari, Ghazari na Shede iliyoko katika kaya hiyo.

Pia, amewataka watu wenye ndugu waliozikwa katika eneo hilo kitotumia shughuli hiyo kama kitega uchumi na kusema hakuna fedha inayoweza kuthaminishwa na binadamu hivyo akawataka kujitokeza kwa wingi.

"Natambua kuwa wapo watu ambao wanasita kuja kushuhudia mabakinya ndugu zao yakiondolewa wakishinikiza kuongezewa hela, niseme tu hii siyo fidia bali ni kifuta machozi kwani hakuna pesa inayoweza kuthaminishwa na binadamu, tujitokeze kuwapumzisha ndugu zetu," amesema Malijani ambaye pia ni Shehe.
View attachment 2455956
makaburi-pic2.jpg
 
Mwanza. Makaburi takribani 1,500 ya Waislamu yaliyoko Mtaa wa Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza yameanza kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga na kupelekwa katika makaburi ya Nyashana kata ya Isamilo jijini humo.
Haina taabu maana waliokuwamo kwenye hayo makaburi wako peponi wanakula kuku kwa mirija na thawabu zao mbalimbali, wengine wakiwa wamezungukwa na watoto wazuri waliopewa walipofika huko!
 
View attachment 2455812

Pale Nyashana si patajaa
Mungu awalaze pema marehem wote.
 
Wakati mwingine viongozi ni kama hawafikilii, gharama zote hizo na usumbufu wa kufukua maiti si bora reli ingepita pembeni
 
Yaaani hapo kwenye pesa ndio macho yote yapo hapo,
Mwingne hata kwenge mazishi hajaja ila pesa lazima aifuatilie, sasa pesa haitoshi kivipi?
Na kwa waislamu ni tofauti na wakristo kuna msalaba wenye jina, hii kweli itakua kazi kutambua.

Hapo mtu anang'ngania maiti hata haijui ili tuu 300k

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna watu wamejibanza sehemu kusikilizia makaburi yasiyotambulika ili wao wajitokeze na kusema ni ya ndugu yao....hatari sana
 
Wakati mwingine viongozi ni kama hawafikilii, gharama zote hizo na usumbufu wa kufukua maiti si bora reli ingepita pembeni
Reli sio kama barabara inakunjwa kienyeji.

Kona yake inatakiwa ianzie kilomita nyingi nyuma.
 
Hivi katika hao Marehem 1500+ hakuna aliyegoma Kufukuliwa?! Maana hizo shughul za ufukuaj zina changamoto
 
Reli sio kama barabara inakunjwa kienyeji.

Kona yake inatakiwa ianzie kilomita nyingi nyuma.
Mkuu una japo picha ya kona ya reli iliyoanzia kilometers nyingi nyuma uweke hapa ? Sijawahi kuona kitu kama hicho dunia hii
 
Back
Top Bottom