Serikali imeanza kutekeleza hoja ya CAG ya kulipa fidia wakazi wa Kipunguni kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege JNIA

Chikuvi2021

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
459
517
CAG kwenye ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha 2020/2021 miongoni mwa mambo mengine, alitoa hoja ya ukaguzi wizara ya Ujenzi na Uchukuzi -Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania ya kulipa fidia kwa wakazi wa Kipunguni A,Kipawa na Kigilagila waliofanyiwa uhakiki na tathamini miaka ya 1994-1997 -Lakini wakazi wa kipawa na kigilagila walipewa fidia mwaka 2011 kwa tathamini ya nyuma.

Serikali tayari imeshajenga terminal 3.Wananchi wa kipawa na kigilagila walipunjwa, lakini kwa uzalendo wao,,walipisha ujenzi wa terminal 3.

-, Serikali iliwazuia wananchi wa Kipunguni A kuendeleza au kufanyia matengenezo nyumba zao. -Kwenye hoja zake za Ukaguzi kwa mwaka 2020/2021 1. CAG kichere alipendekeza Serikali ilipe fidia kwa wakazi wa Kipunguni A kupisha upanuzi wa JNIA 2.CAG alipendekeza Serikali ilipe fidia (nyongeza ya 6%kwa kila) kwa wakazi wa kipawa na kigilagila ambao wamehamishiwa Kigogo Fresh,Zavala,Kinyamwezi na Nyeburu, lakini wengi wao wameshindwa kumalizia kujenga nyumba zao.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG madai hayo yaliongezeka kwa asilimia 301 (kipindi cha ukaguzi wake). 3. CAG aliagiza Serikali kupitia Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania wakae na Mthamini Mkuu wa Serikali kupitia upya madai ya wananchi wa kipawa, kigilagila na Kipunguni A,na walipe fidia stahili, kuepusha kuongezeka kwa gharama.

Serikali ya awamu ya sita ya mama Samia,imefanya tathamini kwa nyumba za wakazi wa Kipunguni A na juzi ijumaa tarehe 6July 2023 Waziri wa fedha Dr Mwigulu Nchemba, Naibu Spika Na Mbunge wa Ilala Mh Mussa Hassan Zungu, Mh Bona Kamori Mbunge wa Segerea na viongozi wengine wa chama na Serikali walihudhuria kwenye mkutano wa Kipunguni A kutangaza kuwa zoezi la uhakiki na tathamini kwa wakazi wa Kipunguni A limekamilika na jumla ya bilioni 140 zitalipwa kwa wakazi wa Kipunguni A kuanzia Mwezi August 2023.

Serikali ya awamu ya sita ipewe maua, Lakini wananchi wa kipawa na kigilagila kigilagila ambao nyumba zao zilivunjwa kupisha ujenzi wa terminal 3 na wao walipwe asilimia 6 kama alivyo shauri CAG ili kufunga hoja ya ukaguzi. Ninawasilisha
 
Mama yupo vizuri tu Ila kwenye bandari ndo ametukosea
Ni uelewa tu unatusumbua wala mama hajakosea nenda Israel mwaka jana wao wameiuza kabisa bandari yao Haifa port kwa Adani group kwa bilioni 1.2 USD .unataka kuniambia waisraeli hawawezi kuijenga nchi yao?
Screenshot_20230709_211457_Google.jpg
 
Mama kanyaga twende tumechelewa sana
Mama yupo vizuri sana.Lakini awe mwangalifu na wasaidizi wake. Kwa mujibu wa hoja ya Ukuguzi wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2020/2021 CAG alisema wananchi wa Kipawa, Kigilagila na Kipunguni A walipwe fidia zao kwa maana kwa kipindi cha miaka 23 ya uchelewashaji wa kufanya malipo stahiki deni limeongezeka kwa shs22.35 bilioni na kufika shs29.78 bilioni . Wasaidizi. wa Rais, baada ya kufanya uhakiki na uthamini kwa nyumba za Kipunguni A,wamekuja na deni la shs 140billioni? Ni Jambo jema kwa wananchi kupata fidia stahiki. Lakini, isije ikawa malipo halali yatakayolipwa wananchi ni pungufu ya hayo mabilioni(sehemu kubwa ikawa malipo hewa).
 
Hadi sasa tuaingia mwezi wa 9 hakuna malipo,kuna mchezo unachezwa na Wizara ya Fedha au TAA. iko kazi nchi hii. wanamwangusha mama kwa kila mbinu.
 
Back
Top Bottom