Makabila yenye mafanikio (kasoro wachaga), sehemu walizotokea hazina maendeleo kwasababu wanaogopa kurogwa wakitaka kurudi kufanya maendeleo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Mchaga ana mambo yake meusi lakini hata yakiwekwa hayo mambo kumi, bado uchawi hauingii kwenye orodha, hata kwa watu tuliowahi kuishi nao Moshi na Arusha tunawajua upande wao mweusi ni utapeli, wizi (hapa wapo hadi majambazi sugu), visasi, ulevi uliopindukia, n.k. lakini maswala ya ushirikina hawa jamaa ni weupe kama mtu alietoka bush kwenda Dar, hata kama watauhitaji ni ule wa kununua maana hata kumkuta sangoma huko kwao ni sawa na kutafuta bikra hodi ya wazazi.

Makabila mengi yenye watu walofanikiwa, maendeleo yao huwa yanaonekana wakiwa mjini ama nje ya wilaya walizotokea, huku mijini watajiachia sana kwenye nyumba nzuri, gari za kifahari, kuishi kitajiri, n.k. lakini breki zote zinafungwa ukiyapima maendeleo yao kulingana na sehemu walizotokea.

Kiukweli wala huwa sio kosa lao kuto endeleza sehemu walizotokea, hii yote huwa ni kwasababu ya hofu ya kupigwa vipapai, mfano kuna sehemu huko makambako nyumba hazina bati, watu wana uwezo wa kuweka bati lakini wanaogopa kuweka bati kwa hofu ya vipapai.

Hali hii huwa inapelekea hata watu wasirudi sehemu zao walizotokea hasa habari zikisambaa kijijini kwamba wametoboa mjini.

Wakinga wanafanya mapinduzi makubwa ya kutisha kwenye biashara kiasi kwamba Kariakoo wao ndio wameikamata lakini wanahofia kurudi kwao kuendeleza kwasababu ya kuogopa vipapai.

Wapo wasukuma migodini, wenye kazi nzuri, n.k. wametokea Geita, shinyanga, Simyu, lakini wanahofia kurudi kwao kupaendeleza kwasababu ya kuogopa vipapai.

Kuna maprofesa wengi sana wametokea Ukerewe lakini wanahofia kurudi kwao kuendeleza kwasababu ya kuogopa vipapai.

Kuna wahaya wengi wameelimika na wana kazi nzuri wametokea bukoba lakini wanahofia kurudi kwao kuendeleza kwasababu ya kuogopa vipapai.

Makabila ya koa wa Mara yamerundikana Jeshini huko wapo wenye vyeo vikubwa lakini wanahofia kurudi kwao kuendeleza kwasababu ya kuogopa vipapai.

HITIMISHO
Ushirikina ni adui wa maendeleo.
 
Mada yako haina ukeli wowote. Umeungaunga habari kufikia unakotaka.

Watu wanawekeza mahali ambako uwekezaji wao utapata thamani sahihi.

Uende ukajenge ghorofa Makete, utasema kuwa hilo ghorofa ni asset au liability?

Ukajenge nyumba nzuri sana kijijini wakati huishi huko, unaenda kwa mwaka mara moja, inasaidia nini? Labda kuwaonesha tu wanakijiji kuwa una uwezo. Wengi huko vijijini, tunajenga nyumba nzuri za kawaida, nzuri zaidi ni pale unapoishi.
 
Na hayo makabila ndo yamejazana kwenye miji mikubwa mbalimbali ya Tz, namaanisha wamepeleka maendeleo kwenye mikoa isiyowahusu.

Hapa nasisitiza kwenye makabila matatu, Wakurya, Wasukuma na Wahaya.
 
Mada yako haina ukeli wowote. Umeungaunga habari kufikia unakotaka.

Watu wanawekeza mahali ambako uwekezaji wao utapata thamani sahihi...
Huko unakoona ni sahihi mtu kujenga ghorofa kwasasa, je palianza na maghorofa miaka?? Au umekuja Dar juzi?
Kwanini hio mikoa aliyoitaja mleta mada isianze kujengeka na kuwa n kama ilivyojengeka dar, kiasi kwamba unaona mtu hapaswi kujenga ghorofa au nyumba nzuri??

Mleta mada anaweza kuwa sawa kwa asilimia fulani lakini sio kusema amekosa mashiko moja kwa moja kama usemavyo.
 
Mada yako haina ukeli wowote. Umeungaunga habari kufikia unakotaka.

Watu wanawekeza mahali ambako uwekezaji wao utapata thamani sahih...
Kwenye mizizi yako ulikotokea huwa hakunaga cha asset wala liability,

Hivi kweli seemu uliyotokea nyumba imechoka, utaacha kujenga nyumba ya kisasa kwasababu ni liability ?

Haya ndio matokeo ya kupatwa na aibu misiba ikitokea huko kwenu, mtu umezoea kulala nyumba kali mjini ila kijijini kwenu unaenda kulala na mifugo chumba kimoja.
 
Kwenye ukoo wenu. Usi generalize mambo. Mimi mchagga pia ila kwetu uchawi haupo.

Na kama upo labda uchawi wa kimaendeleo
Kuna wachawi kama wamarangu? Sehemu gani hiyo isiyokuwa na uchawi Tz hii, halafu mbona huwa mnapenda kujiengua sana kwenye kila linaloonekana baya??

Yani mtu mzima unadiriki kabisa kusema Uchaggani hakuna uchawi??😄

Basi makabila yote hayana uchawi (maana hata nikikwambia uthibitishe uwepo wa uchawi kwa macho huwezi)
 
katika koo zote za kichaga huwezi kosa mtu zaidi ya mmoja ni wendawazimu/vichaa!
 
Kuna wachawi kama wamarangu? Sehemu gani hiyo isiyokuwa na uchawi Tz hii, halafu mbona huwa mnapenda kujiengua sana kwenye kila linaloonekana baya??

Yani mtu mzima unadiriki kabisa kusema Uchaggani hakuna uchawi??😄

Basi makabila yote hayana uchawi (maana hata nikikwambia uthibitishe uwepo wa uchawi kwa macho huwezi)
Em sema ulilogwa lini na mchagga?
 
Back
Top Bottom