NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
A. MAENDELEO (Kujenga kwao)
Mtu ana mafanikio makubwa huku mjini ana nyumba ya kisasa, gari nzuri, kipato cha uhakika, n.k lakini huko kwao hali ni mbaya, Nyumba imekaa kimasikini mpaka aibu, bati lina kutu,ndani vitanda vimechoka, jikoni sufuria ni za kale, n.k… Huu ni uungwana kweli ? kuna makabila unakuta profesa kasimamisha mjengo kijijini humo ndani lakini ukiangalia hali za mjirani zinatia huruma.
Hakunaga kitu kinaleta baraka kama kusaidia kwenu kwa kupelekea maendeleo, na ndio maana mkoa wakilimanjaro si ajabu ni namba 2 kwa kiwango cha chini cha umasikini,,,, wachaga huwa hawasahau kwao, yani ukifika huko vijijini watu wamejenga,
KURUDI KUSALIMIA NA KUKUTANA
Kwenda kusalimia kijijini wengine mwaka mzima unapita hawajarudi ila nauli ipo, hata kwa wale wanaorudi kila moja anaenda kivyake vyake awajumuiki kwa pamoja,,, mwezi huu mjomba, mwezi unaofata, shangazi, mwezi mwengine ba mdogo, mwisho wa mwaka ni kaka, n.k.
wachaga wana utamaduni mzuri, ikifika mwezi wa 12 wachaga wanarudi kwao "KWA PAMOJA", hata waliopo New York, Dubai, London hufanya jitihada kurudi, kukutana ndugu wote ama wengi kwa wakati mmoja kuna umuhimu zaidi kuliko kila mtu akienda kivyake vyake,, Ondoa shaka, si ndugu tu utawakuta bali hata majirani na marafiki