Mtu anatoka kazini, anarudi nyumbani.
Anafanya shughuli zake. Labda aende dukani.Akiwa njiani, salamu kwa majirani—hakuna mazungumzo marefu.Ni maisha ya kawaida, ya utulivu.
Ule urafiki wa “buda niko base, pita” umeisha.
Sasa ni “tupange weekend” lakini weekend ikifika kila mtu ana shughuli.
Sio kwa ubaya. Ni maisha tu yanavyojipanga.
Ile energy ya kukutana kila siku, kukaa hadi usiku, kuzungumza mambo yote ya dunia—imepungua.
Sio kwamba watu hawapendani tena. Ni kwamba priorities zimebadilika.
Ule bestie wa kila siku, sasa mnachat maybe mara moja kwa wiki.
Mkiambiwa mkutane, ni plan ya siku mbili kabla—na bado inaweza ikaghairika. Lakini bado, ukimuona, mnacheka kama zamani.
Connection haijapotea, imebadilika tu.
Na hiyo nayo ni aina fulani ya grace—mazingira yakibadilika lakini moyo ukiendelea kupenda.
upo phase ipi?