Maisha ya mtu mzima na urafiki unaobadilika polepole

Maisha ya mtu mzima na urafiki unaobadilika polepole

Palina

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2021
Posts
3,754
Reaction score
10,031
Mtu anatoka kazini, anarudi nyumbani.

Anafanya shughuli zake. Labda aende dukani.Akiwa njiani, salamu kwa majirani—hakuna mazungumzo marefu.Ni maisha ya kawaida, ya utulivu.

Ule urafiki wa “buda niko base, pita” umeisha.

Sasa ni “tupange weekend” lakini weekend ikifika kila mtu ana shughuli.
Sio kwa ubaya. Ni maisha tu yanavyojipanga.

Ile energy ya kukutana kila siku, kukaa hadi usiku, kuzungumza mambo yote ya dunia—imepungua.
Sio kwamba watu hawapendani tena. Ni kwamba priorities zimebadilika.

Ule bestie wa kila siku, sasa mnachat maybe mara moja kwa wiki.

Mkiambiwa mkutane, ni plan ya siku mbili kabla—na bado inaweza ikaghairika. Lakini bado, ukimuona, mnacheka kama zamani.

Connection haijapotea, imebadilika tu.

Na hiyo nayo ni aina fulani ya grace—mazingira yakibadilika lakini moyo ukiendelea kupenda.

upo phase ipi?
 
Umependa au upo phrase ipi?

Umri hasa unachangia Sana kuna age girls or women wakifika , they prefer kuwa karibu na mahusiano yanayo involve win win situation.
 
The older i becomes, the fewer friends i have
The verb "becomes" should be "become" to match the subject "I." Everything else is structured well!

Ndiyo ukubwa na pia mtu unavyozidi kukua na ndiyo u-muhimu wako unazidi kupungua kwa baadhi ya watu wanaona kama unaelekea kuzeeka zama zako zimepita hasa ukiwa huna hela ndo tatizo zaidi...
 
Haya ndio maisha ya kisasa ya kimjini hasa. Ni mihemko tu Wazungu wana msemo "dog chasing its tail" yaani kama mbwa anavyo ukimbilia mkia wake ni mzunguko tu na mateso.
Furaha katika maisha imepungua japo tuna vitu vingi vya kusaidia maisha.
 
Hakika, umeandika uhalisia kabisa. Cycle inapungua sana, unabaki na watu wachache kwa ajili ya mambo muhumu. Kukutana kila mara ni kama kunakufa, ni umri, ni majukumu, ni kubadilika hobbies, ni kufocus na mahusiano na familia.
 
njoo uwanjani ukutane na wenzako, ni furaha tu,, uyu anavuta sigara , yule anapga energy drink, alafu pembeni wajuba wanapuliza😄,, si lazima ucheze mpira, njoo unione navosakata kabumbu,,

au kacheze draft ukutane na kila aina ya vituko,, utasikia "Hili nakuua kabisa hutoki kenge wewe"
 
Back
Top Bottom