Maisha ni magumu utadhani nchi iko Vitani

Maisha ni magumu utadhani nchi iko Vitani

Hakuna utawala wa kuheshimu KATIBA Tanzania, bahati nzuri dunia yote inajua hivyo sasa. Dunia ilijua hilo kupitia hukumu za kesi mbali mbali kama ile ya akina CHACHA WANGWE na wenzake ya kupinga Wakurugenzi wa halmashauri, majiji na miji kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi, na badala yake "MAHAKAMA YAKO UNAYOIAMINI" IKATUPILIA MBALI HOJA ZAO.
Hujajibu swali nililouliza, na ulilojibu sijakuuliza.

Sawa, mahakama haziaminiki, dunia yote inajua.

Sasa utafanya nini kingine?

Hujajibu swali hili. Unarudi kwenye kulalama kuhusu mahakama, wakati mimi nishatoka huko.

Unaelewa hata unachotaka ni nini na utakipataje?

Kwa jibu lako hili unajionesha kama mtu anayependa kulalamika bila kufanya lilote. Inawezekana CCM ikikubali tume huru na mahakama huru ukalalamika kwamba imekuondikea sababu zote za kulalamika.

Kwa majibu kama haya sishangai CCM wanawachezea michezo kila uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nimeweka suluhisho Mkuu? Tuna OMBWE la utawala utakaoheshimu katiba ya nchi, hili tunashughukulika nalo kupitia KUPAAZA SAUTI ili watawala waachane na ukiukwaji huo. Pia VUGUVUGU la Tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu 2020, na baadaye tupate katiba mpya kupitia ile rasimu ya Mzee Warioba. Huko mahakamani hakuna chochote kwa sasa. Majaji na akina Hakimu SIMBA wanatembea na kadi za CCM muda wote.
 
Unaelewa kwamba unachekesha sana?

Ukipata katiba mpya wakati Magufuli kaziweka mahakama mfukoni kama mnavyosema, halafu mahakama zisiizingatie hiyo katiba mpya, hiyo katiba mpya itakusaidiaje?

Kama una vipengele vya katiba ya sasa vinavyokuruhusu kufanya mikutano ya kisiasa, halafu Magufuli anavivunja, na huwezi kumfanya kitu, hiyo katiba mpya itakusaidiaje?

Nauliza, kama huwezi kuitumia katiba iliyopo sasa na kupata haki zako, katiba mpya itakusaidiaje?

Watanzania tunajidanganya kwamba katiba mpya ndiyo tatizo.

Wakati hata haki za katiba ya sasa hatuzitumii.

Kuna ujinga wa kufikiri kwamba, nchi yetu ikiwa na katiba nzuri tu, kuwa na katiba nzuri kutatusaidia.

Watu ndio wanaleta mabadiliko, katiba haileti mabadiliko. Kuna mtu alikuwa anasifia uhuru wa Kenya, akasifia katiba ya Kenya imeleta mabadiliko. Nikamsahihisha, nikamwambia watu wa Kenya ndio walioleta katiba mpya na mabadiliko, katiba ya Kenya si iliyoleta mabadiliko.

Katiba mpya si suluhisho. Unaweza kupewa katiba mpya, halafu kama huna populace iliyo politically aware and active, katiba mpya ikawa maandishi yasiyo na maisha, kwenye karatasi iliyokufa.

Katiba si mabadiliko. Inaweza kusaidia mabadiliko, lakini si mabadiliko.

Watu ndio wanaleta mabadiliko.

Wakati katiba ni maandishi, kinachobadili nchi ni watu, si katiba.

Unaweza kuwa na Ferrari, gari la kwenda kasi sana, lakini kama hujui kuliendesha vizuri, mtu mwenye ki Volkswagen Beetle akakupita, kwa sababu hujui kuiendesha hiyo Ferrari iende kasi.

Kabla ya kudai katiba mpya, hii ya sasa mmeitumia vipi? Rais kavunja katiba kwa kukataza mikutano. Hatuhitaji katiba mpya kupinga uinevu huu. Mmetumiaje haki za kikatiba zilizopo sasa?

Kama mmeshindwa kutumia haki za kikatiba zilizopo sasa, katiba mpya itawafaidisha vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna pesa ya bure,fanyeni kazi
Suala si pesa ya bure.

Unaelewa kwamba maamuzi ya serikali yanaathiri uchumi?

Unajua uchumi umeanguka?

Unajua tuna nyumba zetu za ofisi hapo Dar makampuni ya kimataifa yalikuwa yanakodi kwa dola za Kimarekani 4,000 kwa mwezi, sasa yanakodi kwa dola 1,000 kwa mwezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pamoja na uchumi wako hata sio fani zetu kweli inawezekana vitabu vinakwambia ivo lakin nafikili hukurefrect zaidi katika ualisia naona umejikita kwenye theory zaidi unaposema kwamba ukiongeza mishahara wawekezaji watakimbia gharama za uendeshaji .Hivi kwa mishahara ya hapa nyumbani kwamba labda kimo cha chini iwe lki 6 kwa mwezi alafu mwekezaji ataki kuja sasa ni mwekezaji au mwekezaji uchwara ambao wengine hufika hata mtaji hawana bali ujanja janja mbona kenya watumishi angalau wanalipwa vizuri na pesa yao iko juu inamaana kenya hakuna wawekezaji
Hivi nchi zilizoendelea kama hata marekani ambapo watu wanalipwa hakuna wawekezaji ?kwa iyo wafanyakazi wetu tusiwalipe vizuri kwamba hatutapata wawekezaji .Aisee kama tunataka wawekezaji wakuja kwetu,tuwalinde,tuwape ardhi ,alafu wawalipe ndugu zetu mshahara kidogo huku wakitaka wapate faida kubwa basi nami naungana na mzee maghufuli wabaki kwao watuache na malighafi zetu mbona wakija na watu wao hua wanawalipa vizuri .mwekezaji kweli kama anajua sehemu anayowekeza output ipo ya kutosha ogopa kulipa wafanyakazi vizuri
Tofautisha malipo kwa wataalamu (professionals) na wale wasio na ujuzi, unafahamu kutwa ya Kenya KES 300 kwa siku?
 
Back
Top Bottom