Unaelewa kwamba unachekesha sana?
Ukipata katiba mpya wakati Magufuli kaziweka mahakama mfukoni kama mnavyosema, halafu mahakama zisiizingatie hiyo katiba mpya, hiyo katiba mpya itakusaidiaje?
Kama una vipengele vya katiba ya sasa vinavyokuruhusu kufanya mikutano ya kisiasa, halafu Magufuli anavivunja, na huwezi kumfanya kitu, hiyo katiba mpya itakusaidiaje?
Nauliza, kama huwezi kuitumia katiba iliyopo sasa na kupata haki zako, katiba mpya itakusaidiaje?
Watanzania tunajidanganya kwamba katiba mpya ndiyo tatizo.
Wakati hata haki za katiba ya sasa hatuzitumii.
Kuna ujinga wa kufikiri kwamba, nchi yetu ikiwa na katiba nzuri tu, kuwa na katiba nzuri kutatusaidia.
Watu ndio wanaleta mabadiliko, katiba haileti mabadiliko. Kuna mtu alikuwa anasifia uhuru wa Kenya, akasifia katiba ya Kenya imeleta mabadiliko. Nikamsahihisha, nikamwambia watu wa Kenya ndio walioleta katiba mpya na mabadiliko, katiba ya Kenya si iliyoleta mabadiliko.
Katiba mpya si suluhisho. Unaweza kupewa katiba mpya, halafu kama huna populace iliyo politically aware and active, katiba mpya ikawa maandishi yasiyo na .maisha, kwenye karatasi iliyokufa.
Katiba si mabadiliko. Inaweza kusaidia mabadiliko, lakini si mabadiliko.
Watu ndio wanaleta mabadiliko.
Wakati katiba ni maandishi, kinachobadili nchi ni watu, si katiba.
Unaweza kuwa na Ferrari, gari la kwenda kasi sana, lakini kama hujui kuliendesha vizuri, mtu mwenye ki Volkswagen Beetle akakupita, kwa sababu hujui kuiendesha hiyo Ferrari iende kasi.
Kabla ya kudai katiba mpya, hii ya sasa mmeitumia vipi? Rais kavunja katiba kwa kukataza mikutano. Hatuhitaji katiba mpya kupinga uinevu huu. Mmetumiaje haki za kikatiba zilizopo sasa?
Kama mmeshindwa kutumia haki za kikatiba zilizopo sasa, katiba mpya itawafaidisha vipi?
Sent using
Jamii Forums mobile app