Sisi tunaosema hali ya uchumi mtaani inabana nadhani tupimwe akili, pengine tutakuwa na matatizo ya akili.
Mwezi uliopita nilikwenda kuchukua mifuko ya kuhifadhia nguo hapo Kariakoo soko dogo kitu nilichokutana nacho nilibaki kinywa wazi. Ilikuwa Alhamis ya mwisho ya mwezi wa kwanza, nikakuta vile vibanda wanavyouza hiyo mifuko ikiwa ni mitupu watu wamefungua ila wamekaa wanaangaliana tu wengine wakiwa wamefunga biashara zao. Nikauliza kulikoni leo hivi!? Nikajibiwa, NEMC jana na juzi walikuja humu na maaskari wakiwa wamesheheni bunduki kwenye gari zao, umepigwa msako hapo ndani hawajawahi kuona ni kama walitaarifiwa pale pana Majambazi, wanakwenda kukabiliana nayo.
Wale wajomba walichukua stores zote za mifuko iliyokuwepo wanawaambia hiyo imezuiliwa ila ile ya Taka migumu imeruhusiwa. Kuna jamaa alichukuliwa mzigo wa mil 20 na faini juu, hizo za mil 10 zilikuwa nyingi tu, katika kutafuta suluhu na undani wa hili jambo, ikafahamika kuwa kuna muhindi katoa hongo kwa wakubwa alitawale soko yeye mwenyewe ila hatoi mifuko ya kuhifadhia nguo, yeye anatengeneza ile ya kuhifadhia mchele. Nilichoka mwili na roho, katika kudadisi haswaa naambiwa hata hii mifuko mbadala wenye viwanda vikubwa ni watoto wa mkuu mmoja hivi na yule mama.
Sisi tunaosema hali ya uchumi imekuwa ngumu tukapimwe Akili.