Maisha mema yanapatikana kijijini

Maisha mema yanapatikana kijijini

Yupo kazini, linda kipato chako
Screenshot_20260829-170139.png
 
Tangu niamie huku kijijini, sizeeki kihasara hasara
  • Napata maji safi,
  • Hewa safi,
  • Kelele nzuri za ndege,
  • Hakuna msongo wa mawazo,
  • Napata mayai, nyama, maziwa muda wowote ninaotaka,
  • Napata vitu vingi bustanini,
  • Matumizi ya hela ni madogo sana kutokana na vitu vingi kupatikana shambani na kwenye mifugo,
  • Ngozi ya mwili inang'aa haina mabakamabaka,
  • Hakuna uchafuzi wa hewa unaosababishwa na msongamano wa watu,
  • Na mika 73 lakini naonekana kama kijana wa miaka 20,
  • Koti la suti limenikaa vizuri halijanizidi mwili kama wa huko mjini,
Kweli maisha mema, yanapatikana huku kijijini

View attachment 3659541
Weka Picha yako Mkuu.
Bila picha bado haujanishawishi kabisa.
 
Napenda sana sehemu yenye uoto asili 🥰 sehemu tulivu hakuna kelele
Bustani ya maua nyumba zisizo banana

Shida vijijini kwetu utaishia kuboreka hakuna facilities za kutosha
Upo kama mimi, napenda sehemu ambazo nyumba hazijabanana.

Napenda nikitoka nje kuwa na ukimya wa usili uliotawala.

Nimepanga hivi karibuni niende Dodoma au Morogoro kisha nipate lodge au hotel ya bei ya chini ambayo ipo sehemu zenye ukimya nikakae huko.

Uzuri wa kukaa sehemu kama hizo ni kwamba akili inatulia, unakuwa huru, unatafakari mambo ktk uzuri.
 
Bila kusahau mbeya green city, kule unapata hali ya hewa nzuri, ardhi yenye rutuba, vyakula kibaoo, maisha gharama chee na zegembe O.G zimefungashaa.. me nimejiwahi huko
Ha ha ha dah mbona unanitamanisha. Sema Mbeya ni mbali, nina watu wanaoishi Mbeya wanasema gharama za chakula zipo chini sana.
 
Upo kama mimi, napenda sehemu ambazo nyumba hazijabanana.

Napenda nikitoka nje kuwa na ukimya wa usili uliotawala.

Nimepanga hivi karibuni niende Dodoma au Morogoro kisha nipate lodge au hotel ya bei ya chini ambayo ipo sehemu zenye ukimya nikakae huko.

Uzuri wa kukaa sehemu kama hizo ni kwamba akili inatulia, unakuwa huru, unatafakari mambo ktk uzuri.
Na hakika uta enjoy sana
Nashukia makelele sana
Kelele nazoweza kuvutiwa nazo ni mziki laini tu
 
Na hakika uta enjoy sana
Nashukia makelele sana
Kelele nazoweza kuvutiwa nazo ni mziki laini tu
Miaka ya nyuma nilikuwa naendaga DODOMA, sasa kuna kipindi nikasema acha nisilale Hotelin AREA C niende sehemu ya mbali kidogo, nikapata Lodge ya elfu ishirini na ilikuwa ndo mpya mpya kule CHAMWINO. Aiseee, niliienyoj sana, kwanza ile saa mbili tu usiku purukushani huzioni, kumepoa tulii, kwa nyuma kulikuwa na Bar basi nikawa naenda naagiza maji yangu na soda na nyama fresh kabisa.

Ikifika saa au 5 kule ni kimya, ni kama saa nane au tisa ya dar. Saa moja ya kule kuna kaupepo na kabaridi kazuri sana. Ukiamka asubuhi ya saa mbili kale kajua kanachoma na upepo na ubaridi. Sasa hayo mazingira mimi ndio nayaelewa. Nimepanga mwaka mpya nikaelewa.
 
Mazingira kama hayo ni mazuri sana kwa afya ya akili
Na utulivu wa ndani
Navutiwa na maeneo kama hayo sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom