"Raha" ya nyumba za kupanga ni pale nyumba inapokuwa na familia zaidi ya sita lakini choo na bafu ni kimoja!
Choo na bafu vikiwa ni kimoja ni mtihani.
Niliwahi kupanga nyumba ya aina hiyo maeneo ya Kinondoni miaka ya mwishoni ya 80 mwanzoni ya 90.
Ila kutokana na kazi zangu nyingi kumaliza baada ya saa 1 jioni nilikuwa napenda kupita kwanza mgahawani ili kupata chakula cha jioni maana kupika kila siku nayo ilikuwa mtihani.
Sasa nikirudi ni saa 4 au 5 na nakuta wengi wa wapangaji wameishalala.
Kumbe kuna dada mmoja ambae alikuwa akitatizwa sana na kutokuwepo kwangu mimi mapema pale nyumbani.
Basi kumbe mimi bila kufahamu hilo akawa ananingojea na kila nikirudi tunajikuta twaongea wee hadi saa 7! Khasa ikiwa ni ijumaa.
Akaja kusema kwamba anapenda nikiwepo mapema maana anakuwa assured na ulinzi wa mahala pale, nikaelewa jambo hili.
Ila siku moja nilichelewa sana na niliporudi nilipitiliza hadi chooni na kabla sijaiingia nikamwona yule dada anatoka huko bafuni akiwa na khanga moja tu, lakini akarudi haraka chumbani kwake huku akiwa ameficha uso akinisalimia kwa aibu.
Ni pale nilipojifunza kwamba bahati zingine huja kwa namna tofauti, maana huyu bibie kumbe ni wa kwenye kaya kabisa Tanga Line.
Nilimuuliza kwa utani kama alikuwa akifanya safari za kule Handeni ama vipi, akasema la na alikuwa yupo OK na mimi.
Na baada ya muda kidogo tukaanza kuzoeana na baadae akaja kuwa ndo bi mkubwa wangu na mama watoto tokea wakti ule hadi leo.
😀