Nakupa uzoefu na facts muhimu sana. Mimi sina historia ya kukaa nyumba ya kupanga ambayo ni ya kushare wapangaji wengi. Niliwahi kukaa kwa miezi 5 tuu kipindi naanza kazi kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo nikapata kazi nyingine nzuri zaidi nikahama mkoa kabisa, huko nikapata nyumba nzima tunashea watu wawili tuu. mwenzangu alikuwa anakaa mwenyewe familia yake ilikuwa mkoa mwingine. so nilienjoy utulivu mkubwa sana, hadi nilipohamia kwangu.
Sasa buana, nisikuchoshe. nimepata safari mkoani, ambayo nitakaa miezi 3 kwa ajili ya mradi fulani. Nikachanga karata zangu na wenyeji wa hapo ninapoenda, nikasema nitakuwa bwege nikikaa lodge kwa miezi 3. Mwenyeji wangu akaingia kusaka vyumba, nikapata chumba kimekaa design kama hostel, but so advanced kama apartment hivi. Kucheki, bei kitonga maana ni za taasisi flani. Jamaa alinikaribisha, kweli kuna vyumba vingi pale. Nilipoingia jamaa akanielekeza masuala ya maji ni bure, umeme ndo kila mtu anajinunulia wa kwake ukiisha. Kwa kuwa nilikuta umeme upo sikuhangaika, ila alinipa angalizo kuwa nikiona umeme umekatika kwangu na vyumba vingine unawaka, basi nijue wa kwangu umeisha ninunue. Maana wameweka sub-meters kila chumba. Nilikaa kama wiki 3, usiku saa 7 nikaona umeme umekatika kwingine unawaka. Nikaona hakuna haja kumsumua jamaa. Asubuhi ndo nikamcheki akanipa mwongozo nikajinunulia. nilinunua umeme wa 5000, nikapata 12.3 units. Matumizi yangu ni taa tuu usiku, feni mara chache, kuchaji simu na laptop, na kupiga pasi nguo. Leo ni siku ya 7 tangu nimeweka umeme, nimeshangaa nimekuta nimetumia unit 1.5 kwa wiki nzima. Kwa hiyo kwa muda wa wiki 4 nitakuwa nimetumia units 6 za umeme. kwa lugha nyingine, kwa Sh. 5000, napata umeme wa kutumia miezi miwili.
Sasa jiulizeni nyie mnaokaa vyumba vya kupanga, mpo wapangaji 6 wengine hadi 10. Mwenye nyumba anawaramba kila mmoja 10,000/- au 15,000/-kila mwezi umeme. wewe bachelor ndani hakuna unachotumia zaidi ya taa. kupiga pasi nguo yako moja kila siku, na kuchaji simu na laptop. Mnapigwa hela za bure au mnazidiana nyie wapangaji wengine wanatumia vitu vingi vinavyotumia umeme mwingi ila wewe usiye na vingi unawahudumia wengine. Nimependa sana huu utaratibu wa hawa jamaa kwa kweli laiti wapangaji wangejitambua nchi nzima mngewangembana wamiliki waweke submeters kila mtu anunue umeme anaoutumia. Haya mambo ya kuchangiana ni wizi mkubwa aisee.