Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Habari za sasa wanachama wa Jamiiforums natumai wote ni wazima wa afya, nilikuwa na jambo lini kereketalo moyoni mwangu liitwalo “MAHARI”

Nilikuwa na tatizo na huu utamaduni ulio zoeleka hapa dunia mpaka kukomaa wa malipo ya kifedha/mali kwa mwanaume/mwanamke ili kuweza kukidhi vigezo vya kuoa au kuolewa.

Mahari ni kitendo kinacho shusha utu wa watu hapa duniani kwa wake na kwa waume hauna tofauti na biashara ya utumwa iliyo kuwa imemea hapa duniani Karne za 19 kurudi karne nyuma iliyo husisha kununua watu walio thaminishwa kwa viwango mbalimbali vya kifedha na kimali kutokana na maumbile yao na uwezo wao wa kinguvu.

Duniani mpaka sasa kwa asilimia kubwa watoto wa kike wana thaminishwa kama bidhaa sokoni kwa kigezo cha mahari kama utamaduni kitu ambacho kinavunja utu wa mtu kwa kuwa mtu hawezi kuthaminishwa kwa kiwango chochote kile cha fedha au mali.

Sasa wazazi wameshikwa na viburi vya kitamaduni za kitumwa kwa kuwa thaminisha wanao kutokana na tabia nzuri walizo nazo wanao au uzuri wa rangi/ maumbile ya wanao na kutaja viwango mbali mbali vya kifedha au mali mfano [ Mzazi anasema“ hauwezi kuoa mwanangu bila million 5-10 au bila ng'ombe 10-20]

Huu utamaduni wa mahari ulio mbaya unao vunja utu wa watu hapa dunia umekaliwa kimya sana na dunia tofauti na tamaduni nyingine kama ukeketaji, ndoa za utotoni, biashara ya utumwa wakati wa ukoloni n.k hizi ni baadhi ya tamaduni zilizo pigiwa kelele na dunia mpaka kukoma nyingine kupungua kwa kasi sana hapa duniani.

Ushauri binafsi: Kwa nini fedha/mali zinazo tumika kukamilisha biashara hii ya utumwa[ mahari ] visiwanye wazazi wa pande zote mbili wakutane kwa pamoja na kukusanya fedha au mali hizo kwa pande zote mbili na kuwa changia watoto wao fedha za kuanzia maisha yao kitu ambacho kitakuwa msaada kwao na kwa maisha yao.

Maswali:
1. Kwa nini dunia ipo kimya kuhusu kukomaa kwa biashara hii ya utumwa ya kuuza watu kwa kigezo cha tamaduni ?

2. Licha ya kuwa wanawake ndio waathirika wakuu wa biashara hii ya utumwa iitwayo mahari, kwa nini wame likalia kimya swala hili ?

3. Kwa nini wapiganiaji wakuu wa swala la usawa wa kijinsia na haki za binadamu wame likalia kimya swala hili la biashara ya utumwa linalo vunja utu wa binadamu kwa kigezo cha mahari ?

4. Je ni haki na ni sahihi mtu kuendelea kuthaminishwa kwa viwango vya kifedha au mali ?

5. Kwa nini wanawake walio wengi hawataki kuolewa bila kunuliwa ? Na hutambiana wao kwa wao kwa viwango vya kifedha au mali vilivyo tumika kuwa nunua ?

Karibuni wadau kwa michango yenu, Ila zingatieni zaidi mada husika na maswali tajwa.
 
Uzuri hailazimishwi, ukishindwa unaachana nayo.

Sina hakika sana kama mwanaume aliyetimia sawasawa akishindwa kutimiza utaratibu wa kuoa anawezaje kuwajibika kwa familia?

Kuoa sio kuwa na uwezo wa kudindisha. Kuoa ni zaidi ya majukumu ya kifamilia.

Mwenyezi Mungu akujaalie watoto wa kike uwakuze wakifika wakati wa kuolewa wagawe bure bure tu.
 
Nimesoma ila nilichokiona ni malalamiko na frustration zako na tafsiri ya kubeza mahari.

Nenda kajielimishe kuhusu maana ya mahari katika makabila mbalimbali na thamani ya mahari kwa muolewaji na muoaji na heshima inayoambatana na kukamilisha tendo hilo.

Kila kabila lina utaratibu wake wa kupanga mahari na hawatofautiani sana. Nimewahi kushiriki vikao hivyo zaidi ya makabila 10 tofauti. Mfano, ukioa kwa wasukuma mahari ni ng'ombe kati ya 14 hadi 18 na tofauti ipo kwenye thamani ya huyo ng'ombe. Uchagani ni ng'ombe 1, mbuzi hawazidi3 na pombe ya mbege madebe kadhaa kulingana na ukubwa wa ukoo unakooa. Mbeya, chunya ni vikorokoro vingiii ila hivizidi 3m.

Ukichunguza mahari yana mgawanyo mpana; baba, mama, bibi, babu, wajomba, mashangazi, kaka,dada nk
Ila furaha yake na heshima yake ni kubwa kwenye jamii zetu.

USHAURI:
Kama uwezo umepungua ongea na msichana aongee na wazazi wake ila usionyeshe kudharau... hata baadhi ya makanisa hayafungishi ndoa bila idhini ya maandishi ya wazazi wa mwanamke kuwa taratibu zote zimefuatwa.

KUMBUKA:
MKE MTU HUPEWA NA WAZAZI WA MWANAMKE. WAKIRIDHIA UNA MKE. VINGINEVYO HUYO NI KIMADA TU.
 
Usirekebishe mipaka iliyoachwa na babu wa babu zako.... Angalia marekebisho mengi yameleta Mambo gani katika jamii.
Nafkiri hakuna haja ya kukwepa gharama hizo.
Ndugu kwani ndoa za utotoni na ukeketaji haukuwa utamaduni wa mababu na mababu wa huko kale, je leo hii karne ya 21 havija pigwa vita hivyo vitu ?
 
Uzuri hailazimishwi, ukishindwa unaachana nayo.

Sina hakika sana kama mwanaume aliyetimia sawasawa akishindwa kutimiza utaratibu wa kuoa anawezaje kuwajibika kwa familia?

Kuoa sio kuwa na uwezo wa kudindisha. Kuoa ni zaidi ya majukumu ya kifamilia.

Mwenyezi Mungu akujaalie watoto wa kike uwakuze wakifika wakati wa kuolewa wagawe bure bure tu.
Kulikuwa hakuna ulazima ndugu wa kutumia lugha chafu katika huu mjadala, lugha chafu inapoteza maana na nguvu ya hoja zako. Jitahidi kutumia lugha nzuri ndugu utaeleweka tu ujumbe wako.

Karibu tena kwa hoja zako ndugu
 
Nimesoma ila nilichokiona ni malalamiko na frustration zako na tafsiri ya kubeza mahari.
Nenda kajielimishe kuhusu maana ya mahari katika makabila mbalimbali na thamani ya mahari kwa muolewaji na muoaji na heshima inayoambatana na kukamilisha tendo hilo.
Kila kabila lina utaratibu wake wa kupanga mahari na hawatofautiani sana. Nimewahi kushiriki vikao hivyo zaidi ya makabila 10 tofauti.Mfano, ukioa kwa wasukuma mahari ni ng'ombe kati ya 14 hadi 18 na tofauti ipo kwenye thamani ya huyo ng'ombe. Uchagani ni ng'ombe 1, mbuzi hawazidi3 na pombe ya mbege madebe kadhaa kulingana na ukubwa wa ukoo unakooa. Mbeya, chunya ni vikorokoro vingiii ila hivizidi 3m.
Ukichunguza mahari yana mgawanyo mpana; baba, mama, bibi, babu, wajomba, mashangazi, kaka,dada nk
Ila furaha yake na heshma yake ni kubwa kwenye jamii zetu.
USHAURI:
Kama uwezo umepungua ongea na msichana aongee na wazazi wake ila usionyeshe kudharau...hata baadhi ya makanisa hayafungishi ndoa bila idhini ya maandishi ya wazazi wa mwanamke kuwa taratibu zote zimefuatwa.
KUMBUKA:
MKE MTU HUPEWA NA WAZAZI WA MWANAMKE. WAKIRIDHIA UNA MKE. VINGINEVYO HUYO NI KIMADA TU.


Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo ndugu wazungu na waarabu walikuwa sawa kushirikana na machifu kuuza mababu zetu kwa kuwa thaminisha kwa viwango vya kifedha/mali kutokana na maumbile yao na nguvu walizo kuwa nazo ?
 
Kipindi mama yangu anaolewa, babu yangu alikataa mahari kata kata, ikabidi baba atoe jogoo asiwe ameondoka mikono mitupu.

Lakini baba yangu alimjengea pia alimuuguza babu pesa inayozidi mahari mara dufu.

Wakipendana waende wakaishi, kama Mungu akiwabariki watawakumbuka.
Wewe ni miongoni mwa wana jamii wachache wanao weza kutafsiri hili swala kiupana zaidi, wana jamii wengi hudhani wote wanaopiga vita mahari ni hawana uwezo wa kutoa mahari la hasha hio sio tafsiri sahihi.
 
Mahari ipo mpaka kwa biblia tangu Yakobo alichunga kwa miaka saba kama malipo ya kuchukua mke, malezi ya mtoto wa kike sio kazi ndogo
 
umaskini ni mbaya sana,ndoa ina heshima yake aliyeolewa kwa mahari usilinganishe na aliyechukuliwa bure
Je mababu zetu na mabibi zetu watumwa walio nunuliwa na waarabu na wazungu wali heshimishwa kwa kunuliwa kwa vipande vya fedha/mali na hao wazungu na waarabu ?
 
Back
Top Bottom