Kwanini kijana hutakiwi kutoa mahari kwa karne hii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nafahamu mada hii ni ngumu, na haitakuwa nzuri sana kwa sababu ya mazoea na desturi za jamii zetu nyingi ambazo kimsingi bado zipo gizani. Lakini hiyo haitazuia kuijadili na hapa tutajadiliana kwa hoja. Wale wenye hisia na mihemko ya kimbuzimbuzi tayari nilishawafikiria hivyo najua nitadili nao vipi.

Elewa kuwa Mahari ni utaratibu wa zamani ambao ulihusisha kumtoa binti kwenda/kuhamia familia au ukoo mwingine. Yaani Mwanamke kumilikiwa na familia au ukoo mwingine. Unapozungumzia umiliki unazungumzia vitu, wazo au wanyama au rasilimali zingine isipokuwa Watu.

Kiasili, kisheria, Kihaki, na kiukweli, na kiakili Mtu HAMILIKIWI. Hakuna sheria popote pale ya kummiliki MTU.

Hata Mungu muumbaji hakumiliki na hana hatimiliki yako wewe kama Mtu. Hii ni kwa sababu ya utu ulio ndani ya mtu mwenyewe. UTASHI ndio kitu kipekee ambacho kinamfanya Mtu asimilikiwe na yeyote yule hata yule aliyemuumba.

Mtu anahaki ya kuchagua chochote atakacho, kumchagua yoyote amtakaye na ikiwezekana kumuacha wakati wowote autakao bila kuzuiwa na yeyote. Mtu amepewa uwezo wa kumchagua au kumkataa hata muumba wake. Hii ni kwa sababu ndani ya mtu kuna Uungu ndani yake, huo Uungu ndio unaitwa UTU.

Zamani, wanawake na baadhi ya makundi ya binadamu hawakuchukuliwa kama Watu. Hata juzijuzi tuu hapa kulikuwa na biashara ya utumwa. Watumwa hawachukuliwi kama Watu na ndio maana huuzwa, na kutumikishwa pasipo haki yoyote ya kujiamulia (UTASHI).

Zamani ili umiliki mwanamke (sio mtu) ni lazima umnunue. Ili awe kwenye ukoo au familia yenu.
Mwanamke kwa vile hakuwa mtu, aliweza kuuzwa hata pasipo kushirikishwa kuwa anauzwa kwa nani bila kujali anampenda mtu huyo au laa. Ulikuwa ni ukatili wa kuogofya. Binti yangu kamwe sitokufanyia jambo hili.

Katika kuuza Mwanamke ambaye baadaye ataitwa mke(kumbe sio kweli isipokuwa mtumwa fulani) kinachofuata ni kumfanya yule mke mtumwa na kijakazi lakini pia Inakuwa kama mashine ya ngono na kuzalisha watoto.

Wanawake hawakuzingatiwa kihisia, kiakili, kiroho wala kimwili. Sio ajabu Mwanamke asipozaa mtoto kwa zama zile ilikuwa Kimbembe. Sio ajabu pia kukuta wanawake wameolewa kimafungu kwa makumi kwa kile kiitwacho ndoa za Mitala.

Hii itategemea na uwezo wa Mwanamke kununua Wanawake kama ng'ombe. Ukiweza kununua wanawake ishirini zamani ungewanunua na kuwaweka sehemu moja na wasifanye kitu kwa sababu hawakuwa Watu bali waliathiriwa na mifumo ya kijinga na kuwageuza kuwa wanyama. Ndio maana walinunuliwa.

Mwanamke hakuweza kurithi chochote kwa sababu alinunuliwa tuu, na anaweza kuuzwa muda wowote. Ilikuwa ni bidhaa. Kwa kweli Taikon ingawaje sieleweki na wengi lakini naandika mambo haya kwa huzuni.

Haya, Mwanamke kwa vile sio mtu na alinunuliwa basi hana haki na watoto aliowabeba yeye mwenyewe katika tumbo lake kwa miezi tisa, kwa taabu. Akizaa inakuwa tena shida kama amezaa mtoto aliyekinyume na matarajio ya mumewe au ukoo alionunuliwa. Mwanamke hakuwa na haki ya watoto na wakati mwingine mpaka jina lake huweza kubadilishwa kwa sababu alinunuliwa, sio Mtu.

Ni kama wazungu walivyokuja Afrika, walibadisha majina ya wale wote waliotaka kuwa na uhusiano nao(wazungu).

Kimsingi mimi kama Mtibeli halisi nilishasema kuwa sitotoa mahari na kamwe sitofanya jambo hilo kwa sababu ninajua ni ujinga, kosa na kinyume na haki, upendo, akili na Ukweli.

Sasa Kwa nini kijana wa sasa hutakiwi kutoa Mahari? Sababu zifuatazo zinahusika;

1. Mwanamke ni mtu kama wewe, huwezi kumnunua/kummiliki
Unaweza ukajidanganya umemnunua lakini kimsingi hujafanya hivyo zaidi ya kuwa umemdhalilisha na atakuzalilisha tuu. Sio ajabu baada ya kumnunua bado atataka kwenda kwao jambo ambalo kwa zamani ukishamnunua Mwanamke hana uwezo wa kufikiri jambo kama hilo.

Huwezi kumnunua/kummiliki kwa sababu siku yoyote akitaka kukuacha atakuacha tuu na hakuna chochote utafanya na huna pakulalamika hata kwa Mungu muumbaji. Kwa sababu hata Mungu mwenyewe hawezi kummiliki/kumnunua mtu.

2. Haki sawa
Wewe na Mwanamke mnahaki sawa kwa sababu nyote ni Watu ila wewe mwanaume kwa upeo wako mdogo au ubinafsi ndio ulitaka kumgeuza mwenzako kama Bidhaa au kifaa fulani hivi. Sio ajabu sikú mkiachana licha ya kuwa ulimnunua (tolea mahari) hautalipwa chochote zaidi ya kugawana mali ikiwezekana na watoto kwenda na mama yao.

Wakati zamani ukitoa Mahari (ukinunua Mwanamke) unammiliki (kwa sababu sio mtu) na hamuwezi kuwa na haki sawa. Hata akizingua hana popote pakwenda na hata akiondoka bado hataondoka na chochote hata watoto aliowazaa na hakuna wa kumsikiliza kwa sababu yeye sio mtu na alinunuliwa. Ni kama ng'ombe tuu.

3. Huna mamlaka naye licha ya kumnunua
Zamani ukimnunua Mwanamke unakuwa na Mamlaka naye na kumuamulia chochote.
Lakini siku hizi kwa vile wanawake wameshajitambua na kuwa Watu, huwezi kuwa na Mamlaka nao ingawaje watakulaghai au utalaghaiwa na familia au jamii kuwa ni mkeo na unamamlaka naye lakini huo ni uongo tuu.

Labda ni kwa sababu siku hizi Mahari au biashara ya kuuza wanawake siku hizi sio kwa jumla jumla bali unakodishiwa tuu.

Elewa kuwa licha ya kuwa utamuoa binti wa Watu kwa kumnunua lakini bado Mamlaka itakuwa juu yake mwenyewe na wazazi wake au ukoo wake. Hivyo hukuwa na sababu ya kumnunua wakati ungeweza kumchukua kwa hiyari ili Muishi maisha ya Hiyari pasipo Unafiki.

4. Mwanamke anahaki ya kuondoka na watoto na usifanye chochote
Zamani jambo hili lisingewezekana kwa sababu tayari ulishamnunua na kumtolea mahari. Nina kesi nyingi za wanaume wanaonipigia simu wakiomba ushauri wa namna ya kuwachukua watoto waliochukuliwa na Mama zao licha ya kuwa walifuata taratibu zote za kimila ikiwemo utaratibu wa kumnunua huyo Mwanamke.

5. Mtoto anahaki ya kumchagua mama yake na kukukataa wewe hata kama ulimnunua mama yake
Zamani hilo lisingewezekana, mtoto hana uwezo wa kumchagua mama yake hata angekua mkubwa kwani mfumo tayari ulikuwa unatambua biashara ya kuuza binadamu ikiwemo kuuza Wanawake.

Yaani unamnunua Mwanamke kwa kile kiitwacho mahari, unamzalisha, unalea watoto kwa nguvu zako alafu mwisho wa siku Mwanamke anaomba talaka, kisha huyo na watoto wanamchagua yeye wewe unabaki huna lolote zaidi ya kulialia kama lijinga na kusema wanawake ni mashetani. Wewe ndio shetani ambaye ulifanyika biashara ya kununua binadamu.

Hutafanya chochote hata uende mahakamani hakuna utakachokipata kwa sababu Mahakama zinatambua Mkeo na watoto wako ni Watu na wana uhuru wa kuchagua. Usije ukaleta upuuzi wako kuwa sijui ulimnunua (ulitoa mahari), sijui uliwalea hiyo haitahesabika chochote.

6. Unaweza kutoa Mahari na ukamfumania mkeo na mwanaume mwingine na mkeo akawa upande wa huyo mwanaume uliyemfumania naye na hutafanya chochote zaidi ya uhalifu kama ulivyomnunua.

Hakunga kesi mahakamani ya kuibiwa Mke. Mke haibiwi kijana. Mke ni mtu anahiyari na uhuru wa kutumia mawazo yake, mwili wake atakavyo na yeyote ilimradi wamepatana.

Kama wewe unavyoweza kuwa na Mwanamke yeyote ndio vivyohivyo.

Sasa wanaume wengi tukiona wake zetu wanatumia uhuru wao katika miili yao roho zinatutoka na hii ni kutokana na ile kasumba mbaya ya kujua tunamiliki wake zetu na zaidi tumewanunua na kugharamika kwa mengi. Acheni uzwazwa vijana. Mtakufa siku sio zenu. Huwezi miliki mtu yeyote dunia hii hata mtoto uliyemzaa huwezi kummiliki. Mbuzi Wewe.

Taikon Master ninakushauri, Usitoe mahari(usimnunue Mwanamke), Kama umempenda Mwanamke au kama wewe ni binti unakijana anakupenda.

Kwa heshima tuu, zungumzeni, wekeni mambo yenu Sawa. Nendeni kwa Wazazi wenu pande Mbili.
Kama wanataka mahari waambieni hatuna mahari ya kutoa au binti sema sitaki kutolewa mahari.

Sio ajabu mtu akishatoa mahari hataki tena ukaribu na Familia ya Mwanamke. Pia familia ya Mwanamke haina uhuru wa kwenda kwa binti yao kusalimia. Huo ni ubinafsi. Lakini kwa upande mwingine ni haki kwa sababu binti yenu nilishamnunua, nilimalizana na nyie kwa nini kunifuatafuata.

Watibeli hatutoa mahari wala binti zetu hawatolewi Mahari. Familia zinaunganishwa kwa upendo na sio biashara za kijinga. Wazazi wa mwanamke ni wazazi wetu na wazazi wa mwanaume ni wazazi wa Wake zetu.

Mama mkwe au baba mkwe wangu anahaki ya kunichukulia kama kijana wake na mimi namchukulia kama mzazi wangu kwa sababu tumeunganishwa na upendo. Sikununua binti yao na wao hawakuniuzia binti yao. Wanahaki ya kunionya kama kijana wao.

Lakini mniuzie binti yenu tena kwa kushusha shusha bei kama nguo za karume. Ati ku-bargain kutoka milioni saba mpaka tatu alafu leo mjifanye kuniita mtoto wenu. Pumbavu labda sio Mimi Mtibeli na wala sio Watibeli. Watibeli hatunaga unafiki.

Au ati umeshachukua mahari ya watu, umemuuza binti yako hivi kuna upendo tena hapo. Ndio ile hata kwenda kumsalimia binti yako mpaka ujiulizeulize, unaona aibu kama jinga fulani.

Sio ajabu ndoa inaonekana ngumu kwa sababu kuna mambo mengi ya kijinga ambayo Watu wanayaona kabisa lakini wanashindwa nini chakufanya wakati uwezo wanao. Waliochukizwa Poleni

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Naunga mkono hoja na ndo chanzo cha kuzalisha masingo mama na masingo baba usipotoa mahari hicho ndo chanzo cha laana Kabisa na kingine vijana wa skuizi hawasikii Kabisa ni wabishi sana
 
Mmmmmmhmn .Okay nimesoma kwa umakini hadi mwisho. Ila pamoja na uandishi wako mzuri wa kulenga hoja nadhani unatakiwa kuielewa jamii ya mwafrika na tamaduni zake kwa mtazamo wa kiafrika (afrocentric perspective) na sio kwa mtazamo wa kimagharibi au ulaya (Eurocentric perspective).

Haya ndio mojawapo ya madhara ya elimu ya magharibi ambayo tumepewa kutokea vidudu hadi chuo ambayo inatutoa katika uhalisia na uasili wetu na kutengeneza mgogoro wa nafsi katika kukubaliana na asili yetu tukiamini sisi ni watu tofauti na ancestors wetu sababu hatukupitia mafunzo ya tamaduni zetu kwa kupitia channels zetu za asili bali tumejulishwa kuhusu tamaduni zetu kupitia mfumo wa elimu tunaoita rasmi ambao umeundwa na tamaduni za kimagharibi ndani yake na hivyo kuleta conflict na asili yetu.

Ila kwa kifupi ni vema ukafahamu kuwa mahari haikuwahi na wala haitawahi kuwa ishara ya manunuzi ya binadamu kama namna umeiweka hapa. Mahari inazungumziwa kwa mitazamo ya mataifa ya kimagharibi ambayo hii si sehemu ya tamaduni zao.

Kama ilivyo kawaida ya mataifa ya magharibi moja wapo ya athari ya muingiliano wao na mataifa mengine ni kulazimisha maoni yao yakubalike na watatumia kila aina ya maneno ili wao waonekane wanatamaduni bora juu ya wengine. Si unaona hata ushoga wanalazimisha na kuna wapumbavu tupo nao hapa afrika wameshaanza kukubaliana nao na kupractice, si juzi tu hapa umesikia papa amepenyeza idea ya kubariki ndoa za jinsia moja hivi bado tu haustuki ajenda za haya mataifa ya magharibi ni ipi?

Haya mataifa ya magharibi yamekwenda uarabuni na kukuta waarabu wana tamaduni zao, wao wakaziharamisha na kuita za kishenzi, imani zao wamezigeuza kuwa za kigaidi na kufanya muarabu popote anapoonekana aonekane ni msababisha milipuko ya mabomu a.k.a terrorist. Hivi haushtuki?

Ukikataa asili yako wewe unatambulika kwa identity gani?

Naomba unambie ni mzazi gani au ni wapi ambapo ulishawahi kuona imeandikwa na watu wa jadi kuwa mahari ni bei na dau la kumuuza binti regardless ya maneno unayoyasikia hewani au kwa watu wasiojua asili ya mwafrika na tamaduni zake?

Brother, napenda sana maandiko yako ambayo huwa yamejaa maarifa ndani yake ila kwenye hili fanya kama umekosea darasa na haujaeleweka, hebu nenda kaitembelee tena tamaduni ya mwafrika au niseme basi TAMADUNI ZA WATU WEUSI. Naomba ukajifunze na kuielewa vema ndani yake kwa maana ya Values, practices, symbols, heritage, history, routines, participants, languages, na kadhalika. Ukielewa jambo vema kwa asili yake itakuwa ngumu sana kupotoshwa.

Naomba nimalizie kwa kusema, hili andiko ni batili na halijazingatia uhalisia wa jamii yetu ya kiafrika na mbaya zaidi halijautambua utamaduni wa mwafrika kwasababu huwezi kujiita na kujitambua kama mwafrika huku kwa kauli zako ukikataa mila na desturi za asili ya mwafrika ambazo kwa bahati mbaya unaonekana kutozifahamu kabisa especially eneo hili la Posa na mahari badala yake umechota fikra za magharibi na kuziamini zaidi kuliko fikra za asili yetu kama waafrika.

Ni mitazamo hii ambayo hupelekea mabinti leo kuzalishwa hovyo na vijana ambao hawana ridhaa ya wazazi wa binti kwa kigezo cha kukwepa process ya kuposa na mahari. Huwezi kuwa kijana wa kiafrika mwenye akili timamu halafu uende kwenye familia ya mtu useme kirahisi rahisi nataka ridhaa ya kuishi na binti yenu bila kufuata mila na desturi za familia ya binti hiyo ni dharau kubwa sana na kukosa baraka za familia kwenye maisha utakayoishi na binti.

Mahari sio mauziano ya binadamu, mahari na posa ni sehemu ya mila na desturi za tamaduni zetu za kiafrika ambayo inalenga kujinga misingi ya mahusiano mapya halali, inajenga utambuzi wa kimamlaka ya kuwa kijana umepewa fimbo ya uongozi na baba wa familia umchukue binti yake ukaishi nae na kumuongoza kama vile mwanao, jinsia ya kike na mtu anayejifunza kwako zaidi.

Mahari na posa ni ishara ya kupevuka kiakili na utayari wa kuanza maisha ya mahusiano halali kinyume na sasa vijana unachukua binti wa watu, mara ghafla mimba, mara maisha yamewashinda, ukifuatilia kiundani unakuta mlichukuana kimya kimya na kuanza maisha bila ridhaa ya wazazi wa binti kisha unakwenda mikono nyuma baada ya kugundulika na pengine umeshazaa nae halafu unataka wale wazazi wawape baraka zao?Ndio maana wengi huwa hata mkienda mahusiano yanakumbwa na nuksi za kila aina na yanafeli sababu wazazi walipa maigizo ya baraka ila ndani walikuwa na fedhea ya kuona kijana asiye na maadili kachukua binti yao bila ridhaa yao na anakuja kuwatusi kuwa ameshalala naye sana ndio kaja kujulikana.

Ulizeni wenzenu ambao wamelipa mahari kwa adabu zote kisha wakaoa wakwambie namna wanajiskia huru kimahusiano na mambo yanakwenda vema.

Tujifunze, tusikurupuke.
 
Mahari haina uhusiano wa moja kwa moja na pesa, kutoa mahari haihusiani na kumnunua mtu, mahari inaweza kuwa kitu chochote, mwanamke ni mtu anaeheshimiwa, kusikilizwa na aliepewa upendeleo wa hali ya juu sana hii ni kutokana na mafundisho ya Kiislamu. Mahari ni sehemu ya somo kabisa katika dini na ukilielewa vizuri hauta lipinga hilo.

NB, Mtibeli najua unapenda kujifunza bila kubagua imani, tamaduni wala itikadi hivyo chukua mda wako kusoma tena kuhusu Mahari ni nini, kwanini iliwekwa taratibu ya mahari, sheria zake na kwanini tunapaswa kutoa mahari kulingana na Uislamu ulivyoelezea hayo yotee.
 
Mahari inayopaswa kuzungumziwa hapa si mahari ya kiarabu maana wale wana mila na desturi zao kwenye utamaduni wa kiarabu, turejee kwenye utamaduni wetu wa kiafrika.

Mahari zetu hupangwa kulingana na mila na desturi za tamaduni za makabila yetu ya kiafrika.

Naomba tusipotoshane hapo
 
Unajua hata hao wazungu walikuwa na mahari?

Identity ya muafrika ipo lakini sio kufuata mila potofu.
Unajua hata ukeketaji ni mila na desturi?
Unajua ukabila ni mila na desturi?
Unajua waganga wa Jadi na matambiko ni mil na desturi?
Unajua kuoa wake wengi na Mwanamke kutokusoma na kutokurithi mali ni mila na desturi?
Unajua kumrithi mke wa kaka au mdogo wako ni mila na desturi?
Unajua uongozi wa kichifu, kitemi na kifalme ni mil na desturi? Hizi demokrasia sio mila zetu.

Unajua binti kuchaguliwa mum3 ni mila na desturi?
Unajua kuolewa na kaburi ni mila na desturi?

Kufuata mila sio tatizo, ishu inakuja kwenye ni mila na desturi ipi sasa.

Zipo mila nyingi mno ambazo ni mbaya ambazo baadhi zimeondolewa na wakati zinaondolewa walikuwepo wapingaji kama hivi leo.
Desturi ya kutoa mahari ni sehemu ya mila potofu inayolenga kuutoa utu wa Mwanamke.

Ndio maana nikakuambia sababu kubwa ya mahari mpaka leo wengi hawajui na wanashindwa kusema ukweli kuwa ni biashara ya kumnunua Mwanamke.
 
Uislamu hauna uhusiano na tamaduni za kiarabu bali ni muongozo na taratibu zakumuwezesha binadamu kuishi kulingana na makusudio ya mungu. Hata waarabu wenyewe wanatamaduni zao nje na Uislamu ambazo zilikuwepo kabla hata ya Uislamu.
 
Mahari haina uhusiano wa moja kwa moja na pesa, kutoa mahari haihusiani na kumnunua mtu, mahari inaweza kuwa kitu chochote, mwanamke ni mtu anaeheshimiwa, kusikilizwa na aliepewa upendeleo wa hali ya juu sana hii ni kutokana na mafundisho ya Kiislamu. Mahari ni sehemu ya somo kabisa katika dini na ukilielewa vizuri hauta lipinga hilo.

NB, Mtibeli najua unapenda kujifunza bila kubagua imani, tamaduni wala itikadi hivyo chukua mda wako kusoma tena kuhusu Mahari ni nini, kwanini iliwekwa taratibu ya mahari, sheria zake na kwanini tunapaswa kutoa mahari kulingana na Uislamu ulivyoelezea hayo yotee.

Nimezungumzia Mahari katika mfumo wetu wa kiafrika.

Mahari ya kiislamu haina shida kwa sababu anayetamka ni Mwanamke mwenyewe. Sasa itategemea Mwanamke anampenda mumewe kiasi gani. Na ninaimani kuwa Mwanamke akiambiwa ataje mahari yake lazima azíngatie moyo wake kwa hiyo Mumewe mtarajiwa.

Lakini akitaja mahari mtu mwingine lazima atazingatia maslahi yake hasa nini alikifanya kwa mtoto(uwekezaji) na hapo ndio biashara inapoingia ya kuuza Watu.
Mbali na aliwekeza kiasi gani atathaminisha muonekano wa binti yake. Sio ajabu huko Usukumani binti mweupe na mrembo bei yake ya kuuzwa ni kubwa mno tofauti na wanawake wengine. Hii pekee inatosha kueleza kuwa ni unyanyasaji wa hali ya juu.

Au unaambiwa Mwanamke ukimzalisha soko lake linashuka (hauziki kwa bei nzuri) au ukilala na Mwanamke unaweza kulipishwa pesa kwa kuharibu bidhaa ya Watu kwani itaathiri siku ya Kuuzwa.

Sasa bado utasema hapo Watu hawauzi wanawake. Labda kama Watu wameamua kuwa wanafiki.

Mtu akienda kununua Mwanamke utasikia akisema, kwanza binti amezalishwa, kwanza hana Bikra, binti yenu mwenyewe si mnamuona.
Hivi hiyo kweli ni Akili au Haki?
 
Mimi binafsi Nina mke mwaka wa 7 sjawahi kutoa mahali na sjawahi kuombwa hata SKU moja ,bila shurti ya yeyote niliamua Sehemu ambayo ningepeleka mahali aitumie kupata ujuzi kwenye vyuo vya ufundi na huu ndo mwaka wa tatu amamalizia ,
 
Mimi nitaunga mkono suala la kufuta mahari endapo wanaume watakubali kwamba wote wanaume na wanawake tuna haki sawa na hakuna mwenye mamlaka ya kumtawala mwingine, na hata watoto wanaozaliwa waruhusiwe kutumia majina ya ukoo ya upande wa mwanaume na mwanamke na yote yaandikwe kwenye vyeti vyao vya kuzaliwa, kwanza hili lilipaswa lianze kutekelezwa hata kabla ya kufuta mahari maana siku hizi hadi mwanamke naye anatafuta pesa na kuhudumia watoto kama mwanaume wakati hilo halikutakiwa kuwa jukumu lake
 
Mtoto anaweza kuitwa au kujiita jina lolote tuu hata asipotumia jina la mzazi au wazazi wake.

Jina ni utambulisho wa mtu.

Kutawaliwa kunatokana na wanawake kutokuwa Watu.
Biblia inaposema Mwanaume atamtawala Mwanamke inarejelea kuwa Mwanaume ni mtu na Mwanamke sio.

Ndani ya familia yenye Watu kuna Uongozi.
Kiongozi anaweza kuwa yeyote tuu iwe mwanaume au mwanamke ilimradi kuna sheria za familia za kufuata.

Mtawala lazima awe zaidi ya kiongozi kwani atatawala binadamu kwa kudhibiti utu wao
 
Mimi binafsi Nina mke mwaka wa 7 sjawahi kutoa mahali na sjawahi kuombwa hata SKU moja ,bila shurti ya yeyote niliamua Sehemu ambayo ningepeleka mahali aitumie kupata ujuzi kwenye vyuo vya ufundi na huu ndo mwaka wa tatu amamalizia ,

Sasa usijemkamtesa baadaye kwa kisingizio cha kumsomesha ujuzi huo
 
Mtibeli hoja yake ipo sahihi kabisa

Zamani mume akifa Moja Kati ya Mali zake alizoacha ni pamoja na mke au wake, utasikia marehem ameacha mashamba matano na wake wawili.

Ndugu wa marehem walikua wanarithi hizo Mali akiwemo mke au wake. Yaani mwanamke alikua ni kama bidhaa au Mali inayomilikiwa na kurithiwa

Sasa hivi mambo mengi yamebadilika kama kurithiwa, limebaki hili la mahari.

Mnaosema mahari ni kama ahsante kwa wazazi wa Binti kwa malezi mazuri ya binti yao mnataka kusema mtoto wa kiume halelewi vizuri? Kwanini hakuna ahsante kwa wazazi wa mtoto wa kiume?
 
Unajua hata hao wazungu walikuwa na mahari?

Identity ya muafrika ipo lakini sio kufuata mila potofu.
Unajua hata ukeketaji ni mila na desturi?
Unajua ukabila ni mila na desturi?
Unajua waganga wa Jadi na matambiko ni mil na desturi?
Unajua kuoa wake wengi na Mwanamke kutokusoma na kutokurithi mali ni mila na desturi?
Unajua kumrithi mke wa kaka au mdogo wako ni mila na desturi?
Unajua uongozi wa kichifu, kitemi na kifalme ni mil na desturi? Hizi demokrasia sio mila zetu.

Unajua binti kuchaguliwa mum3 ni mila na desturi?
Unajua kuolewa na kaburi ni mila na desturi?

Kufuata mila sio tatizo, ishu inakuja kwenye ni mila na desturi ipi sasa.

Zipo mila nyingi mno ambazo ni mbaya ambazo baadhi zimeondolewa na wakati zinaondolewa walikuwepo wapingaji kama hivi leo.
Desturi ya kutoa mahari ni sehemu ya mila potofu inayolenga kuutoa utu wa Mwanamke.

Ndio maana nikakuambia sababu kubwa ya mahari mpaka leo wengi hawajui na wanashindwa kusema ukweli kuwa ni biashara ya kumnunua Mwanamke.
Unaona sasa, unarudia kule kule nilipotoka. Kama utakumbuka nilisema kwamba unatumia standards za mitazamo ya kimagharibi kuhalalisha mambo ya tamaduni za mwafrika. Ona sasa kauli yako kuwa "hata hao wazungu walikuwa na mahari" ni kauli ambayo inaashuria kujilinganisha au kuoanisha utaratibu wa maisha ya mzungu na ya mwafrika kitu ambacho ni kosa muda mwingine.

Hebu tuanze na huo upotoshaji, kusema mila hii ni POTOFU ni kwa kutumia kipimo gani ambacho kimepitishwa na baraza la wanajamii wa kiafrika ambao wanakiri hili jambo kwetu linatudhuru. Hivi unajua kuna mambo mengi sana waafrika wameyapotosha na hawajui hata sababu ya kupotosha ni ipi wao wanachojua hii kitu ni potofu ila wasijue inawadhuru eneo gani. Na hata ukifanya tafiti unagundua hata hao walioambiwa jambo fulani linawadhuru kwa asilimia 90% hawajui ni eneo gani wanadhurika.

Hivi unajua wazungu wana kitu kinaitwa propaganda na hapo wameweka pesa nyingi sana na wameweka watu vichwa sana (propagandists) kwaajiri ya hiyo kazi, unalijua hilo?

Leo unaona wazungu wanaforce kutuaminisha kuwa ndoa ya wake wengi ni haramu sasa kaa nao chini wakuonyeshe hayo madhara utaona makaratasi ya report za kinafiki yatakavyomiminwa hapo ila nenda uraiani ukaone uhalisia kitu ambacho miaka yote kimekuwapo mababu na mababu leo kije kuwa haramu kizazi hiki cha watibetiani?

Halafu mzungu huyo huyo anakuambia mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzake njia ya haja kubwa haina shida na ni jambo la kutetewa kitaifa, umeona huu umalaya wa kitamaduni unavyoweza kuleta madhara. Na kama haujui tu ni kufahamishe hiyo ndio ajenda yao namba moja kwasasa kwenye mataifa mengine especially africa. Wewe unakazania hapa eti ndoa za wake wengi ni haramu, unaweza nipa uharamu wa mwanaume m'moja kuishi na wake 12 katika mji wake?

Umeongelea kukeketa, unajua kukeketa inafanywa na jamii ngapi hapa tanzania yaani umeongea as if ipo kwenye kila kabila la Tanzania. Mimi hata sijui kukeketwa huwa inafanywaje ila najua tu ina involved kukata na kutia majeraha maumbile ya kike so obvious hiyo si salama na inakosa mashiko ndio maana ni jamii chache sana wanafanya tena kwa usiri mkubwa.

So ndugu, naomba tu nikwambie kuijua na kuielewa vema tamaduni yako haikufanyi kuwa mshamba bali itakupa fursa ya kujua namna gani utaivaa nyakati hizi ambazo tuna kizazi hakijui mila na desturi zao ila kuishi kama wazungu ndio ujanja. Matokeo yake leo watoto wa kiume hawajui nafasi yao na wakike hawajui nafasi yao.

Ukisema ukabila hapo sio swala la afrika tu hilo ni swala la nature ambalo utalikuta hata kwa wanyama maana lazima waform classes ili waweze kugawana majukumu. Popote pale unapokwenda kuna kitu kinaitwa makundi (makabila) so hata ukiondoka afrika ukienda ulaya , china, india utakutana na hicho kitu so usikitumie kutaint utamaduni wa mwafrika.

Ukizungumzia uganga wa jadi na matambiko hapo lazima ufahamu sekta zilizomo usichanganye. Afrika hata asia wana wale traditional herbalists au dawa zitokanazo na mimea ya asili ambao wanafanya kazi kama ya pharmacist, halafu kuna wale wazee wa kutumia hisia kutatua matatizo a.k.a wazee wa ramli, usiwachanganye hawa watu katika kundi moja.

Usitumie matapeli waliokuwa wanafanya ramli chonganishi, uongo, kutumia rituals za utapeli kurubuni watu kufanya uhalifu ukasema hawa ni sehemu inayotambulisha tamamudi ya mwafrika hapo utachemka eneo hilo. Zungumzia utajiri wa tiba za asili zisizo na madhara kwenye mwili wa binadamu kama hizi dawa za magharibi, zungumzia group therapy na wazee wenye hekima ambazo gharama yake ni pombe ya kienyeji na nyama kidogo, zungumzia Cupping therapy ambayo sisi tuliifanya kwa pembe la ng'ombe na vifuu, unajua haya mambo wazungu wamekopi kwetu na kujifunza kisha wamekwenda nayo kwao?

Kama watakatifu wetu wakiitwa mizimu inakutisha mbona hauogopi kusali kwa kutumia majina ya watakatifu wa wenzako huko sababu wako unawaharamisha. Yaani babu yako mzaa babu yako, babu mzaa baba, bibi nyanya, hawa leo wanakuwa ni mashetani baada ya kufa ila mtakatifu maria imakulata ambaye hajawahi hata kukupakata ni msafi na malaika?

Kwahiyo kuoa wake wengi ni haramu ila kuwa na mke m'moja na kubadilisha wanawake malaya kila wiki ni sahihi na haina madhara yoyote, yaani mzungu anakupa idea ya kutengeneza mfumo ambao utahalalisha mwanamke kulalwa na wanaume tofauti tofauti hadi achakae mwili kisha tulaumiwe wanaume wote kuwa tunaharibu na kuchezea wanawake ila kuharamisha mfumo ambao mwanamke atakuwa chini ya amri ya mwanaume m'moja, ataishi kwa kuelekezwa na kulindwa na atakuwa na back up na support ya kutosha ya kiuchumi, kijamii, na kiafya. Hebu jitafakari vema hapa.

Kuhusu elimu kwa mwanamke na kurithi mali, hivi nikuulize mzee, hadi sasa haujaona madhara ya wanawake kupelekwa shule, kupewa kazi za mishahara mizuri, kupewa fursa za kumiliki mali, haujaona madhara yake tu bado? Hivi hizi nyuzi zinazofunguliwa hapa JF kola siku wanaume wakihadhithia matukio ya wake zao kuanza ukaidi, viburi na dharau baada ya kupata kazi, au kuhamishwa mkoa kikazi, au kujenga nyumba kwa siri , bado tu haujaona madhara yake boss au unajizima fyuzi?

Hebu zunguka uone wanawake wenye pesa ila wapo chini ya himaya ya wanaume zao uone tofauti yao na hawa wenye pesa na wapo huru kulala na yoyote wanaetaka utamaduni ambao upo sana mataifa ya magharibi.

Mwanamke kutorithi mali kunasababu zake, inaweza kuwa ni ubabe wa ndugu za mume jambo ambalo sheria zipo za kutetea hapo, ila pia inawezekana ikawa familia ya mume wameona tatizo kwa mwanamke pengine alisababisha kifo cha mume ili kurithi mali ili akatapanye na mpenzi wake wa Siri, au pengine shida ni mwanamke hana uwezo wa kusimamia hizi mali ambazo zinasaidia yeye, watoto na ukoo, umeona mfano kesi ya mengi, wewe demu mdangaji kama K lyn ndio wa kumuachia empire kubwa kama ya Mzee mengi aiendeshe kwa kichwa gani alichonacho yule mdangaji?

Kurithi mke wa kaka au mdogo wako haimaanishi ulale nae kimapenzi. Sidhani kama unajua huu utamaduni wa vema maana haupo tu afrika bali hata kwa walatino huko. Kurithi mke wa kaka au mdogo wako maana yake ni kutake over majukumu ya kaka yako katika kuitazama familia yake na huwa ni mwanamke anachagua maana inajulikana mjane huwa ni ngumu sana kusimamia kila kitu mara tu mume wake anapofariki ghafla. Haya mambo yapo hata huku mjini mbona, mtu anapofariki lazima ateuliwe mtu maalumu atakaesimama na mke wa marehemu ili kumlinda na chochote katika kuishi maisha yake bila mume wake.
Kuna wanaume matapeli wanaweza mrubuni wamtapeli mali, kuna yeye kurubuniwa na ndugu zake akajikuta amefilisika na watoto wakaanza kuteseka, kuna pia yeye kuwa na mahusiano ya hovyo nje kama ameshindwa kujizia kwasababu za upweke uliopitiliza. Nadhani ni vema kuelewa jambo kwa faida zake na madhumuni yake na sio uzushi.

Uongozi wa kichifu, kitemi ni hatua za kwanza kabisa za maendeleo ya kisiasa katika jamii yoyote. Hakuna jamii inakaa na mfumo m'moja wa uongozi miaka 1000, eventually tungeweza kuevolve na kuja na aina yetu mpya ya democracy ya kiafrika tofauti na hii democracy ya kimarekani ambayo inatutesa hadi leo. Sisi waafrika tulikuwa tunaendelea vema tu na ilikuwa ni lazima tukienda kwa kubadilika na tungefika pazuri tu bila kuingiliwa.

Binti kuchaguliwa mume (Arranged Marriages) sio jambo la ajabu na limekuwapo vizazi na vizazi, unajua maudhui yake lakini? Vijana wa sasa mnadhani mahaba ndio msingi wa ndoa bora na imara matokeo yake mnaingia ndoani na kuamini ndoa itaimarishwa kwa kugegeda mke kutwa mara 12 na kumletea maua na zawadi plus kumtoa out kila weekend, ila unasahau kinachoendesha ndoa yenu ni social background yake na familia yake. Wazazi wako kwa kulijua hili na experience zao wanatazama binti na familia yake wanajua hapa kijana wetu atapata utulivu hata kama hajavutiwa na binti ila amani ya ndoa itakuwapo sababu family background ya binti inashabihiana na yetu. Sema hautanielewa sababu umeshadhalau desturi hii.
 
Nimezungumzia Mahari katika mfumo wetu wa kiafrika.

Mahari ya kiislamu haina shida kwa sababu anayetamka ni Mwanamke mwenyewe. Sasa itategemea Mwanamke anampenda mumewe kiasi gani. Na ninaimani kuwa Mwanamke akiambiwa ataje mahari yake lazima azíngatie moyo wake kwa hiyo Mumewe mtarajiwa.

Lakini akitaja mahari mtu mwingine lazima atazingatia maslahi yake hasa nini alikifanya kwa mtoto(uwekezaji) na hapo ndio biashara inapoingia ya kuuza Watu.
Mbali na aliwekeza kiasi gani atathaminisha muonekano wa binti yake. Sio ajabu huko Usukumani binti mweupe na mrembo bei yake ya kuuzwa ni kubwa mno tofauti na wanawake wengine. Hii pekee inatosha kueleza kuwa ni unyanyasaji wa hali ya juu.

Au unaambiwa Mwanamke ukimzalisha soko lake linashuka (hauziki kwa bei nzuri) au ukilala na Mwanamke unaweza kulipishwa pesa kwa kuharibu bidhaa ya Watu kwani itaathiri siku ya Kuuzwa.

Sasa bado utasema hapo Watu hawauzi wanawake. Labda kama Watu wameamua kuwa wanafiki.

Mtu akienda kununua Mwanamke utasikia akisema, kwanza binti amezalishwa, kwanza hana Bikra, binti yenu mwenyewe si mnamuona.
Hivi hiyo kweli ni Akili au Haki?
Hiyo si haki. Na kwamantiki hiyo jamii zetu zinahitaji elimu juu ya swala hili la mahari
 
Back
Top Bottom