Sheria za Urudishwaji wa mahari zimesahaulika

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
ORDERS

THE LOCAL CUSTOMARY LAW (DECLARATION) ORDER (1963)

(Section 12)

[1st August, 1963]

G.N. No. 279 of 1963

FIRST SCHEDULE
DECLARATION OF LOCAL CUSTOMARY LAW

SHERIA ZINAZOHUSU HALI YA WATU

MLANGO WA KWANZA

Mahari

Urudishaji wa Mahari - Sheria za Kawaida

37. A. Baba wa binti au mrithi wake anaweza kutakiwa kurudisha mahari wakati ndoa inapovunjika.

B. Mtu anayeweza kudaiwa kurudisha mahari ni yule aliyepokea mahari au mrithi wake.

38. Kiasi cha mahari kinachobidi kurudishwa na njia za kurudishia huamliwa na baraza.

39. Urudishaji wa mahari yenyewe ni lazima ufanyike mbele ya mashahidi zaidi ya mmoja kutoka kila upande. Mashahidi ni lazima wafuatane na baba mkwe na mume au mawakili wao wa halali huko barazani ili washuhudie kiasi cha mahari kinachorudishwa.

40. Deni la urudishaji wa mahari ni deni lililo muhimu kwa baba mkwe na uvunjaji wa sharti hili waweza kufikishwa mbele ya baraza la wenyeji kama kesi ya madawa.

41. Kama mahari ikiwa na mifugo mume anaweza kudai kwamba wanyama wale wale aliowatoa ndio warudishwe iwapo bado wamo mikononi mwa baba mkwe. Hali kadhalika baba mkwe anaweza kurudisha wanyama wale wale aliopokea, na mume ni lazima awapokee hata kama hali yao imekuwa dhaifu.

42. Iwapo baba mkwe hana hata mnyama mmoja kati ya wale waliolipwa kwa mahari, si lazima kwake kurudisha wanyama wa hali ile ile. Muda ambao mume na mke wameishi pamoja ni lazima ufikiriwe, lakini mume anaweza kukataa kupokea wanyama ambao hawana faida yoyote.

43. Kama mume akikataa kupokea ng'ombe wa mahari ambao ni haki yake, na kama baraza likikata shauri kwamba ukatazi wake si wa haki, basi baraza linaweza kutoa talaka papo hapo.

44. Mume hawezi kudai kwamba mahari aliyolipa irudishwe kwa kutoa vitu vile vile alivyotoa, isipokuwa kama vitu hivyo vimo mikononi mwa baba mke.

45. Watoto wa wanyama waliolipwa kwa mahari, kama wanyama hao walikuwa ng'ombe au mbuzi, wasirudishwe. Vivyo hivyo kama mahari yalilipwa kwa pesa haitawezekana kudai faida ya pesa hizo.

46. Kama ndama ambaye hajaacha kunyonya ikibidi arudishwe na mama yake, basi huhesabiwa kama ni mmoja wa wale wanaorudishwa.

Urudishaji wa Mahari baada ya Kufariki kwa Baba Mke

47. I. Nyumba ya mke mmoja

A. Baba ya binti akifa mrithi wake mkubwa ndiye atakayerudisha mahari.

B. Kama baba hakuacha watoto wa kiume na mabinti wake ndio waliorithi mali yake, ambalyo pia ina mahari zao, basi mume anaweza kudai mahari toka kwa binti mkubwa wa marehemu.

C. Kama mahari imepokelewa na rafiki akiwa kama mdhamini wa mke, yule mke ni wajibu wake kurudisha (tazama kifungu cha 24).

II Nyumba yenye wake waliopalikwa.

A. Mume ni lazima adai mahari kutoka katika nyumba iliyopokea mahari yake.

B. Kama baba mkwe mwenyewe ndiye aliyepokea mahari hiyo wakati akiwa hai ni mrithi wake ndiye mwenye wajibu wa iuyarudisha bila kujali ni nyumba ipi alikotoka yule mke.

Urudishaji wa Mahari iwapo yule Binti anaolewa mara nyingine

48. Kama baba mkwe hajamaliza urudishaji baada ya binti wake kuachika, ni lazima alipe deni lake mara tu akipokea mahari nyingine kwa ajili ya arusi ya pili.

49. Ni lazima ikubaliwe kwamba wanyama na/au mali nyingine yoyote ya mahari ya mara ya pili ipelekwe barazani na wala sio nyumbani mwa baba mke. Mume wake wa kwanza au mdhamini wake ni lazima aitwe barazani siku ile ile ili apewe haki yake mbele ya baba mkwe.

50. Kama kiasi kilicopo hakitoshikulipa deni lote, kile kiasi kinachobaki kinakuwa ni deni la muhimu, lakini mke ni lazima apewe talaka yake (tazama kifungu cha 59).

51. Kama baba mkwe hafuati utaratibu wa kifungu cha 49 basi anaweza kuwa na hatia ya kulipa faini kiasi kisichopungua shilingi 100/-.

Urudishaji wa Mahari kama Ndoa ikivunjika

52. Ndoa inapovunjika bila ya kutoka sababu maalum kwa mke au mume:

A. Kama hawakuzaa, maisha ya ndoa tu ndiyo yafikiriwe katika kuweka kiasi cha mahari ambayo itarudishwa.

B. Kama walizaa watoto, wawe wawili wanatoa sababu za kautaka kuachana, basi ni juu ya baraza kufikiri ni yupi aliye na makosa kati ya mke na mume au yupi kati yao ndiye chanzo cha kuvunjika ndoa.

53. Wakati inapotokea kwamba mmoja au wote wawili wanatoa sababu za kutaka kuachana, basi ni juu ya baraza kufikir ni yupi aliye na makosa kati ya mke na mume au yupi kati yao ndiye chanzo cha kuvunjika ndoa.

54. Ni uwezo wa baraza kubadili masharti yaliyomo katika kifungu cha 52 A na B na kufikiria kiasi cha mahari kinacobidi kurudishwa, nayo ni lazima ifuate kosa lenyewe.

55. Baraza linapochungua juu ya shauri hili pia huchungua maisha ya ndoa.

56. Kama mume ndiye mwenye makosa yule mke anapewa talaka mara tu baada ya baraza kukata shauri. Habari ya urudishaji wa mahari hufikiriwa pekee.

57. Kama mume alimtesa mke wake kwa makusudi ya kupata chokochoko ya kuachana, basi baraza linaweza kuamua kwamba sehemu tu au chochote kisilipwe hata kama hawakupata mtoto.

58. Kama mke ndiye mwenye makosa, hawezi kupewa talaka mpaka baba yake amalize kurudisha mahari yote au kama hana vifaa vya kumwezesha kufanya kama alivyoamriwa na baraza mara moja, basi kiasi kinachobaki kinakuwa kama deni la muhimu kwa yule baba.

59. Kama mke mara kwa mara anafanya matendo mabaya ambayo mume yanamuudhi sana, hasa inapokuwa ni namna ya kumuudhi ili aweze kumwacha, baraza litashauri kwamba mahari yote au sehemu tu inabidi kurudishwa, hata kama mke na mume walipata watoto. Kama mume alikuwa hajamaliza kulipa mahari yote, baraza ni lazima lipime na likadirie hesabu ya malipo ya mahari yote kama ilivyokubaliwa na baba mkwe na bwana arusi.

60. Wakati mmojawapo anang'ang'ania kuachana bila ya kutoa sababu yeyote, ni yeye ndiye atakayedhaniwa kuwa mwenye makosa.

61. Upande ule ulio na makosa ndio hauna budi kulipa gharama zote za baraza na gharama ya hati ya Talaka.

Kama Mjane akirudi Kwao

62. Mjane huulizwa kama anapenda kuchukuliwa na ndugu wa marehemu. Kama kikataa, mahari hairudishwei naye (mjane) ana uhuru kwenda kuishi na ndugu zake.

63. Mjane ni lazima apewe hati ya kuthibitisha ujane wake na kwamba ametengana kabisa na jamaa ya marehemu mume wake.

64. Kama mjane anakubali kuishi kama mke wa mmoja wa ndugu wa marehemu, na shauri likikubaliwa na baraza la ukoo, basi anakuwa mke halai wa ndugu hule.

65. Mahari yale yaliyolipwa na marehemu hufikiriwa kama kwamba yamelipwa na ndugu yule.

Mjane mwenye Watoto walio hai au Waliokufa

66. A. Mjane anayo haki ya kumchagua ndugu mmoja wa marehemu na kuishi naye kama mume wake, au anaweza kudai kuishi na watoto wake katika nyumba ya marehemu na atakuwa mmojawapo katika jamaa ya marehemu.

B. Hata hivyo apewe hati ya kuthibitisha kuwa yeye ni mjane. (Tazama kifungu cha 63).

67. Ingawaje mjane wa namna hiyo anatazamiwa kuishi na watoto wake tu, lakini hakuna ndugu aliye na haki ya kumfumania.

68. Iwapo mjane kwa ung'ang'anizi wake anishi na mtu ambaye si ndugu ya jamaa wa marehemu, baraza la ukoo lina haki ya kumwonya na kama halikufaulu linaweza kumridisha kwa baba zake na pia kumnyang'anya watoto wake.

69. Kama mjane akibeba mimba ya mtu ambaye si ndugu wa marehemu baraza la ukoo linaweza kuchagua ama kumrudisha yule mjane kwa baba zake au kumkubali mtoto atakayezaliwa kuwa ni mmoja katika watoto wa marehemu.

70. Kama baba wa yule mtoto ni ndugu ya marehemu, basi mtoto siku zote hukubaliwa kuwa ni mmoja wa jamaa hiyo.
 
Back
Top Bottom