Iwapo mhukumiwa na wafuasi wake wataamini ni adhabu ndogo, watakuwa wanajidanganya. Kwa mtu aliyezoea kuropokaropoka, kama Zitto, adhabu hiyo ni kubwa sana.
Ni dhahiri hukumu hiyo imefungua ukurasa mpya nchini. Ni funzo tosha kuwa kila mtu anawajibika kupima uzito wa mawazo/maoni yake kabla ya kutamka. Kwamba uhuru wa mawazo una mipaka na haki uambatana na wajibu, kama inavyotakiwa katika Katiba ya JMT (1977).
Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Hilo linajukikana, Zitto atachukua tahadhari. Lakini revolutionaries hawafikiri kama wewe. Wao wamejitoa kutetea jamii no matter what happens. Basically wako na falsafa ya Ernesto Che Guevara aliyesema;
"I would rather die standing up than to live life on my knees."
Na akaongeza;
"If you tremble with indignation at every injustice then you are a comrade of mine"
Nakuhakikishia huyo Zitto Kabwe hata bado ataendelea kufanya ukosoaji hivyo hivyo. Hata Tundu Lissu ni wa aina hiyo. Hao wamejitoa sadaka kupambana na uovu na hawajali kufa kwa ajili ya kupigania haki.
Kwani Nelson Mandelea hakufungwa jela miaka 27 kwa sheria ya kibaguzi? Na hatimaye akawakomboa wana wa Afrika Kusini kutoka utawala dhalimu wa kibaguzi.
Je Nyerere hakufunguliwa mashtaka ya uhaini kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kisutu na hatimaye akawa Rais wa kwanza wa Tanzania?
Utamfunga jela, utamuua lakini hata wauaji nao huwa wanakufa. Yuko wapi Iddi Amin? Yuko wapi Saddam Hussein?
Ninachoweza kuongeza ni kwamba hizi harakati za za akina Zitto Kabwe na wenzie zina nguvu sana dhidi ya watawala wadhalimu. Angalia mwenyewe mauaji yaliyofanywa na WATU WASIOJULIKANA kati ya 2016 na 2018 kama vifo vya akina Ben Saanane au Azory Gwanda ni nani waliokomaa kuvikemea kama siyo wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu.
Na sasa hivi kumetulia hatusikii watu kutekwa na kuuliwa, haya ni matokeo ya kelele za akina Zitto Kabwe na wenzake. Hivyo vyombo rasmi vya habari vinaogopa na vinatishiwa kila leo na Dr Abbas na Mwakyembe kufutiwa leseni.
Nikuhakikishie kuwa hawa watawala wa awamu ya 5 ni waoga sana ndiyo maana wanatumia fedha nyingi kwenye security yao. Ila kumbuka kama Watanzania wote tunakuwa waoga namna hiyo hawa watu wataingia mpaka bedroom zetu wakabake wake zetu.
Tusiogope kukemea uovu kwa sababu eti watatukamata na kutuua, hata wao watakuta tu.