Mahakama yabatilisha makubaliano ya mgawanyo mirathi ya Mengi

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Mahakama Kuu Kituo cha Haki Jumuishi, (Masuala ya Kifamilia) Temeke leo Alhamis ya tarehe 25 Agosti 2022 imebatilisha makubaliano ya wasimamizi wa mirathi ya marehemu Reginald Abraham Mengi na wasimamizi wa mirathi ya aliyekuwa mtalaka wake, marehemu Mercy Anna Mengi, kuhusu mgawanyo wa mali alizoziacha Mengi.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Ilvin Mugeta kufuatia shauri la mapitio namba 01 la mwaka 2022 lililiofunguliwa na mjane wa Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi na watoto wake, Jayden Kihoza na Ryan Shaashisha Mengi, wakiwakilishwa na wakili Audax Vedasto Kahendaguza.

Walikuwa wakipinga makubaliano ya wasimamizi wa mirathi ya Mengi, Abdiel Reginald Mengi na Benjamini Abraham Mengi; na Abdiel na Regina Reginald Mengi, wasimamizi wa mirathi ya mama yao, Mercy Anna Mengi.

Katika makubalianao hayo ya Novemba 11, 2021 walikubaliana kuhamisha zaidi ya Sh1.23 bilioni kutoka katika mirathi ya marehemu Mengi kwenda katika mirathi ya marehemu Mercy, kama gharama za Mengi kumtunza mtalaka wake wakati wa uhai wao.

Pia walikubaliana kuhamisha asilimia 50 ya mirathi ya marehemu Mengi kwenda katika mirathi ya Mercy kwa madai kuwa ni mali za wanandoa zilizostahili kugawanywa sawa baina yao.

Hizo ni pamoja na mali zilibakia katika umiliki wa marehemu Mengi baada ya kugawana na mtalaka wake mali kadhaa zilizokuwa zimeshaainishwa kama mali za wanandoa baada ya kutalikiana, ambazo Jacquline na watoto wake ni miongoni mwa warithi.

Mercy na Mengi walitalikiana Machi 13, 2015, kwa makubaliano nje ya mahakama kufuatia shauri la ndoa (talaka) lililofunguliwa na Mengi katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Februari 17, 2015.

Siku hiyohiyo makubaliano hayo yalisajiliwa na kuwa amri ya mahakama hiyo na amri ya talaka ilipitishwa na mali kadhaa zilizokuwa zimeorodheshwa kama mali za wanandoa ziligawanywa baina yao.

Pia walikubaliana kugawana mali za wanandoa zilizokuwa zimesalia, kufikia au kabla ya Juni 15, 2015, kwa sharti kwamba mdaiwa (Mercy) atastahili si zaidi ya asilimia 35 ya mali za wanandoa.

Hata hiyo mpaka Juni 15, 2015 hawakuwa wamewasilisha makubaliano ya mwisho, na hivyo shauri hilo likabakia bila kuhitimishwa mpaka Novemba 21, 2018, ilipotolewa taarifa ya kifo cha Mercy na baadaye ya kifo cha Mengi, Mei 10, 2019.

Ndipo Novemba 11, wasimamizi hao wa mirathi za pande mbili, walipoingia makubaliano hayo ambayo pia ualisajiliwa na kuwa amri ya mahakama hiyo, yaliyopingwa na Jacqueline.

Jaji Mugeta katika uamuzi wake amekubaliana na hoja za wakili Kahendaguza kuwa makubaliano hayo yaliyofanywa na wasimamizi wa pande zote wa mirathi hiyo ni batili.

Amesema kuwa kwa mujibu wa ibara ya sita ya makubalino ya talaka inaweka sharti la lazima kwa wadaawa kufikia maafikiano ya mali za wanandoa zilizosalia bila kugawanywa zilizokuwa zimeorodheshwa na zile ambazo zingebainishwa Juni kufikia au kabla ya 15,2015.

Amesema kwamba hadi Juni 15, 2015 wadaawa hawakuwa wamewasilisha taarifa ya makubaliano yoyote kuhusu mali hizo na kwamba kushindwa kutekeleza hilo kulifunga kesi na Mahakama ya Kinondoni haikuwa na mamlaka kuendeleza mwenendo huo.

“Hivyo ninaamua kwamba tunzo au makubaliano ya Novemba 11, 2021 yaliyofuatiwa na hati ya makubaliano iliyowasilishwa na wadaiwa kama wasimamizi wa mirathi ya marehemu Reginald Mengi na Mercy Anna Mengi ni batili.”amesema Jaji Mugeta na kuhitimisha:

“Ninatengua mwenendo uliosababisha kuwepo kwake unatupiliwa mbaliwa mbali kwa kuwa batili.”

Jaji Mugeta amezitaja mali hizo ambazo zilikuwa zimeorodheshwa ma hazikuwa zimegawanywa kuwa ni pamoja na shamba la ekari 50.8 eneo la USA- River, wilayani Arumeru, shamba la ekari 6 lililoko eneo la Weruweru, wilayani Hai.

Nyingine ni hisa 315,500 katika kampuni ya Bonite Bottlers Limited, hisa 752,500 katika kampuni za IPP Limited na hisa 4 katika kampuni ya The Guardian Limited.

Hivyo ameamuru kuwa mali hizi zinabakia katika mirathi ya marehemu Mengi kwa mujibu wa sheria.

Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, wadaiwa waliwakilishwa na mawakili Deogratias Ringia na Nakazael Lukio Tenga.
 
Uaambiwa kabla hujafa andika wosia, unaandika wosia ukifa wosia unapingwa na watu na watu wengine kwa hoja kwamba wakati unauandika hukua na akili tomamu na watu wengine wakuamulia nje ya uamuzi uliouacha wewe mwenyewe, wosia una maana gani sasa?
Hii sio njia sahihi.

Kama una jumba lina thamani ya mil 400 uko, uza, weka pesa kwenye joint acount ya wewe na mkeo. Weka fixed deposit. Ukifa ndugu wanaambulia vijiko tu.
 
Back
Top Bottom