Nini Hutokea Mahakama za Mwanzo

Mr Lukwaro

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
357
621
Primary Courts/ Mahakama za Mwanzo

1.0 UTANGULIZI

Mahakama ya mwanzo ni Mahakama ya chini kabisa katika mfumo wa Mahakama hapa nchini Mahakama hii inaanizishwa kwa mujibu wa fungu la 3 la sheria ya Mahakama za Mahakimu , Sura ya 11 ya sheria za Tanzania.
Mahakama hizi zinaendeshwa na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wakisaidiewa na wazee wa Mahakama wasiopungua wawili.
Mahakama hizo zinapokaa husikiliza na kuamaua mashauri mbalimbali ya jinai na madai.
Katika aina zote za mashauri wadaawa ni watu binafsi kwani waendesha mashitaka wa serikali au askari polisi hawaruhusiwi kuendesha mashitaka ya jinai katika mahakama za mwanzo. Aidha mawakili wa kujitegemea hawaruhusiwi kuwakilisha wateja wao.
Katika Mahakama ya Mwanzo , mashitaka ya jinai kwa kawaida huanzishwa au hufunguliwa na watu binafsi.

2.0 AKIDI YA MAHAKAMA YA MWANZO.

Mahakama ya mwanzo inakuwa imeundika ipasavyo inapokuwa imekaliwa na Hakimu na Karani wake.

2.1 UWAKILISHI

Je naweza kutumia wakili kusimamia shauri langu katika Mahakama ya Mwanzo?

-Mawakili wa waendesha mashtaka wa Serikali hawaruhusiwi kujitokeza na kutetea au kuendesha mashtaka katika mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo.

Ila wakili wa kujitegemea wanawezi kumwakilisha mtu katika kesi aidha ya jinai au ya madai kama sheria inavoelekeza

2.2 MAMLAKA YA MAHAKAMA YA MWANZO.

2.2.1 Mamlaka ya Kijiografia
** Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri lililotokea popote?

**Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri yatokanayo na matukio yaliyotokea ndani ya wilaya ambamo Mahakama hiyo imo.

2.2.2 Mamlaka katika mashaurii.

i). Je ninaweza kufungua shauri lolote katika Mahakama ya Mwanzo?
Hapana. Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza mashauri kama ifuatavyo:-

1). Mashauri yenye asili ya Madai,

2).Ndoa,

3). Uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi (iwapo marehemu, wakati wa uhai wake, aliishi kwa kufuata taratibu za kimila au taratibu za dini ya kiislamu),

4). Mashauri ya jinai ambayo yametajwa katika sheria kuwa yanawezwa kusikilizwa na Mahakama ya mwanzo.

5). Rufaa na masahihisho kutokana na maamuzi ya Baraza la Kata ( isipokuwa maamuzi katika mashauri yanayohusu migogoro ya ardhi).

ii). Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri lolote la madai?
Hapana. Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza madai ya aina zifuatazo:-

1. Mashauri ya madai yote bila kujali kiasi cha fedha au thamani ya mali iliyo kiini cha madai katika shauri husika iwapo sheria inayohusika katika madai hayo ni sheria ya mila au sheria ya kiislamu.

2. Mashauri yote ambayo mdai ni Mamlaka za serikali za Mitaa(Jiji, manispaa, Halmashauri za wilaya, Halmashauri za miji), ya fedha tasilimu au mikataba yasiyozid shilingi 50,000,000/= (Milioni Hamsini).

iii. Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri la mgogoro wa ardhi?
Mahakama ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza shauri la mgogoro wa ardhi. Migogoro ya ardhi inatakiwa kupelekwa katika Mabaraza ya Ardhi ya Kijijji, Kata au Wilaya kufuatia kiwango cha madai.

iv. Je ninaweza kufungua madai wakati wowote au kuna ukomo wa muda wa kufungua madai Mahakama ya Mwanzo?
Sheria imewka ukomo wa muda ambao mdai anaweza kufungua madai yake. Iwapo kipindi cha ukomo kitapita mdai hawezi kufunguat madai yake tena Mahakamani. Kipindi cha ukomo wa madai huanza kuhesabiwa tangu tukio linalounda chanzo cha madai na haki ya kudai lilipotokea kama ifuatavyo:
1. Madai ya kuvunja mapatano yasiyokuwa ya maandishi ni miaka mitatu (3).

2. Kurejesha shauri lililofutwa kwa kutohudhuria Mahakamani kwa wadaawa ni wiki sita tangu kufutwa kwake.

v. Je naweza kufungua vipi shauri la madai katika Mahakama ya Mwanzo?
Shauri la madai katika Mahakama ya Mwanzo huanza na mdai kuwasilisha madai yake kwa Hakimu ambaye huyaandika madai hayo katika fomu maalumu ijulikanayo kama Hati ya Madai ambayo husainiwa na mdai na hakimu au karani wa Mahakama.
Baada ya kusaini hati ya madai, mdai anatakiwa kulipa ada ya kufungua shauri ya shilingi 5000/= kwa madai yasiyozidi kiasi cha Tsh. Milioni moja na ada ya shilingi 10,000/= kwa madai yanayozidi kiasi cha Tsh. Milioni moja na ahakikishe anapatiwa stakabadhi ya malipo.
Kisha shauri hufunguliwa kwa kupewa nambari na kuingizwa kwenye kitabu cha kusajili mashauri au Rejesta.

2.3 Mashauri ya Ndoa

i). Je ni aina gani ya mashauri ya ndoa yanaweza kufunguliwa Mahakama za mwanzo?
Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza mashauri yafuatayo ya ndoa:-

1. Maombi ya talaka,

2. Matunzo ya mwanandoa au watoto wa ndoa,

3. Maombi ya kutengana,

4. Maombi ya kubatilisha ndoa, na
5. Maombi ya kulea watoto baada ya kutengana au talaka.

ii. Je ni taratibu zipi za kufungua shauri la ndoa?
Utaratibu wa kufungua shauri la ndoa ni kama la kufungua shauri la madai. Hata hivyo kama shauri la ndoa linahusu maombi ya talaka mwombaji anatakiwa kuwasilisha wa kushindwa kuwasuluhisha wanandoa hMalipo ya kufungua shauri la ndoa kuoma talaka ni shilingi 5000/= stakabadhi ya serikali ya malipo hutolewa.

2.4 Mashauri ya Mirathi.

i. Je Mahakama ya mwanzo ina uwezo wa kusikiliza mashauri ya mirathi?

Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka na uwezo kisheria wa kuteua msimamizi wa mirathi iwapo tu marehemu wakati wa uhai wake aliishi kwa kufuata taratibu za kimiila au taratibu za dini ya kiislamu na hivyo sheria zitakazotumika ni ama zile za kimila au zile za dini ya kiislamu.

ii. Ni utaratibu gani unatumika kufungua shauri la mirathi ?
Utaratibu wa kufungua shauri la mirathi katika mahakama ya mwanzo ni kama ifuatavyo:-

1. Ndugu wa marehemu wanatakiwa kupendekeza jina la mtu ambaye wanapenda asimamie mirathi.

2. Ni muhimu pia kuwa na hati ya kifo au uthibitisho wa kifo cha marehemu.

3. Mtu aliyependekezwa na ndugu wa marehemu hujaza fomu Na. 1 ambayo inatolewa na Mahakama.

4. Baada ya kujaza fomu 1 anatakiwa kulipa shilingi 5000/= za kufungulia mirathi. Na apatiwe stakabadhi.

5. Kisha shauri la mirathi hupewa namba na kuingizwa kwenye kitabu cha kufungulia mirathi.

6. Mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza mirathi na kubandika matangazo.

iii. Ni hatua zipi mtu anayetaka kupinga mtu aliyependekezwa na ukoo au ndugu wa marehemu asichaguliwe anatakiwa kuchukua?
Ndugu wa marehemu anayetaka kupinga kuteuliwa kwa mtu aliyependekeza na wana ukoo kusimamia mirathi ya marehemu. Anatakiwa kufika katika Mahakama ya mwanzo na kutoa sababu zake za kupinga mwombaji wa mirathi asikilizwe kwa siku iliyopangwa.

iv. Je kuna haja gani ya kufungua mirathi kama marehemu aliacha wosia?
Ni muhimu na ni mahitaji ya sheria hata kama marehemu aliacha wosia kufungua mirathi. Mtu aliyetajwa na marehemu kusimamia wosia wake ndiye anayetakiwa kufungua mirathi akiomba kuthibishwa. Baada ya kuthibishwa anatakiwa kugawa mirathi kwa kufuata wosia.

v. Nini wajibu wa msimamizi wa mirathi?
Msimamizi wa mirathi anayo majukumu matatu makuu kama ifuatavyo:-

1. Kukusanya mali na madeni ya marehemu

2. Kulipa madeni ya marehemu na gharama za kusimamia mirathi na

3. Kugawa mali za marehemu zilizosalia kwa wraith na kasha kupeleka taarifa la mgao mahakamani.

Ikumbukwe msimamizi wa mirathi si mrithi wa marehemu labda kama atarithi mali kwa mujibu wa sheria inayosimamia mirathi husika.

2.5 Mashauri ya Jinai.

i. Je Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya jinai?
Mahakama ya mwanzo ina mamlaka wa kusikiliza na kuamua baadhi ya mashauri ya jinai yanayotokana na makosa yaliyobainishwa kwenye jedwali la kwanza la Sheria za Mahakama za Mahakimu. Hata hivyo Mahakama ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayotokana na makosa ya kubaka, unyang’anyi wa kutumia nguvu, mauaji, uhujumu uchumi, rushwa , kugushi , uhaini na mengine mengi. Aidha , mahakama hiyo inao uwezo wa kutoa adhabu zilizoidhinishwa na sheria kwa kiwango kilichoidhinishwa na sheria kwa mujibu wa jedwali la tatu la Sheria za Mahakama za Mahakimu.

ii. Ni utaratibu gani.
unatumika katika kufungua na kusikliza mashauri ya jinai?
Shauri la jinai linaweza kufunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo kwa njia kuu mbili kama ifuatavyo:-

1. Njia ya kwanza ni kupitia polisi. Mlalamikaji anatakiwa kupeleka lalamiko polisi ambao huandaa hati ya mashtaka na kumfikisha mlalamikiwa Mahakamani.
2. Na njia ya pili ni ya kwenda moja kwa moja Mahakamani na kuwasilisha lalamiko kwa Hakimu ambaye huandaa hati ya mashtaka ambayo husainiwa na mlalamikaji pamoja na Hakimu. Baada ya hatua hizo mbili shauri hupewa nambari na kuingizwa katika kitabu cha mashauri ya jinai. Hakuna ada inayohitajika katika kufungua shauri la jinai.

2.6 Mashauri ya Rufaa na Masahihisho.

🔥i. Je Mahakama ya mwanzo inamamlaka yoyote ya kusikiliza rufaa?

Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri ya rufaa, na kufanyia masahihisho maamuzi ya kutokana katika Baraza la kata na au kuthibitisha adhabu ya kifungo iliyotolewa na Baraza la Kata lililomo katika mamlaka ya Mahakama hiyo. Hata hivyo haina mamlaka ya kupokea na kusikiliza maamuzi ya rufaa ya Baraza la Kata yanohusiana na migogoro ya ardhi.

ii. Je ni utaratibu upi wa kukata rufaa kutoka Baraza la kata kwenda Mahakama ya mwanzo?

Rufaa dhidi ya uamuzi wa Baraza la kata huwasilishwa kwa maandishi ndani ya siku sitini (60). Mahakama ya Mwanzo inaweza pia kuitisha kumbukumbu za mwenendo wa shauri kutoka baraza la kata na kukagua ili kujiridhisha iwapo uamuzi wa baraza haukiuki Sheria ya Bunge au Sheria ndogo, misingi ya haki asilia na mamlaka ya Baraza.
 
Courts \ Primary Court
1.0 UTANGULIZI

Mahakama ya mwanzo ni Mahakama ya chini kabisa katika mfumo wa Mahakama hapa nchini Mahakama hii inaanizishwa kwa mujibu wa fungu la 3 la sheria ya Mahakama za Mahakimu , Sura ya 11 ya sheria za Tanzania.
Mahakama hizi zinaendeshwa na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wakisaidiewa na wazee wa Mahakama wasiopungua wawili.
Mahakama hizo zinapokaa husikiliza na kuamaua mashauri mbalimbali ya jinai na madai.
Katika aina zote za mashauri wadaawa ni watu binafsi kwani waendesha mashitaka wa serikali au askari polisi hawaruhusiwi kuendesha mashitaka ya jinai katika mahakama za mwanzo. Aidha mawakili wa kujitegemea hawaruhusiwi kuwakilisha wateja wao.
Katika Mahakama ya Mwanzo , mashitaka ya jinai kwa kawaida huanzishwa au hufunguliwa na watu binafsi.

2.0 AKIDI YA MAHAKAMA YA MWANZO.

Mahakama ya mwanzo inakuwa imeundika ipasavyo inapokuwa imekaliwa na Hakimu na Washauri wa Mahakama wasiopungua wawili.

2.1 UWAKILISHI

Je naweza kutumia wakili kusimamia shauri langu katika Mahakama ya Mwanzo?
Hapana, Mawakili wala waendesha mashtaka wa Serikali hawaruhusiwi kujitokeza na kutetea au kuendesha mashtaka katika mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo. Vivyo hivyo wakili wa kujitegemea hawezi kumwakilisha mtu katika kesi ya madai.

2.2 MAMLAKA YA MAHAKAMA YA MWANZO.

2.2.1 Mamlaka ya Kijiografia
** Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri lililotokea popote?

**Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri yatokanayo na matukio yaliyotokea ndani ya wilaya ambamo Mahakama hiyo imo.

2.2.2 Mamlaka katika mashaurii.

i). Je ninaweza kufungua shauri lolote katika Mahakama ya Mwanzo?
Hapana. Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza mashauri kama ifuatavyo:-

1). Mashauri yenye asili ya Madai,
2).Ndoa,
3). Uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi (iwapo marehemu, wakati wa uhai wake, aliishi kwa kufuata taratibu za kimila au taratibu za dini ya kiislamu),
4). Mashauri ya jinai ambayo yametajwa katika sheria kuwa yanawezwa kusikilizwa na Mahakama ya mwanzo.
5). Rufaa na masahihisho kutokana na maamuzi ya Baraza la Kata ( isipokuwa maamuzi katika mashauri yanayohusu migogoro ya ardhi).

ii). Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri lolote la madai?
Hapana. Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kusikiliza madai ya aina zifuatazo:-

1. Mashauri ya madai yote bila kujali kiasi cha fedha au thamani ya mali iliyo kiini cha madai katika shauri husika iwapo sheria inayohusika katika madai hayo ni sheria ya mila au sheria ya kiislamu.
2. Mashauri yote ambayo mdai ni Mamlaka za serikali za Mitaa(Jiji, manispaa, Halmashauri za wilaya, Halmashauri za miji), ya fedha tasilimu au mikataba yasiyozid shilingi 50,000,000/= (Milioni Hamsini).
3. Mashauri ya madai ya madeni ya fedha au mikataba yasiyozidi shilingi 30,000,000/=(milioni thelathini).

iii. Je Mahakama ya mwanzo inaweza kusikiliza shauri la mgogoro wa ardhi?
Mahakama ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza shauri la mgogoro wa ardhi. Migogoro ya ardhi inatakiwa kupelekwa katika Mabaraza ya Ardhi ya Kijijji, Kata au Wilaya kufuatia kiwango cha madai.

iv. Je ninaweza kufungua madai wakati wowote au kuna ukomo wa muda wa kufungua madai Mahakama ya Mwanzo?
Sheria imewka ukomo wa muda ambao mdai anaweza kufungua madai yake. Iwapo kipindi cha ukomo kitapita mdai hawezi kufunguat madai yake tena Mahakamani. Kipindi cha ukomo wa madai huanza kuhesabiwa tangu tukio linalounda chanzo cha madai na haki ya kudai lilipotokea kama ifuatavyo:
1. Madai ya kuvunja mapatano yasiyokuwa ya maandishi ni miaka mitatu (3). 2. Kurejesha shauri lililofutwa kwa kutohudhuria Mahakamani kwa wadaawa ni wiki sita tangu kufutwa kwake.

i. Je Mahakama ya mwanzo inamamlaka yoyote ya kusikiliza rufaa?

Wazee wa mahakama walishaondolewa hawapo siku hizi. Na mawakili wa kujitegemea washaruhusiwa
 
Good
 
Back
Top Bottom