GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
28 Julai 2025

COMRADE PINDA AIWAKILISHA CCM KTK KONGAMANO LA VYAMA KONGWE VYA UKOMBOZI
MADA : KULINDALI MAFANIKIO YA VYAMA VYA UKOMBOZI BAADA YA UHURU, VINAENDANA NA HAJA YA VYAMA HIVYO KUBAKI MADARAKANI

African National Congress (ANC) itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kilele cha Vyama vya Ukombozi 2025 katika Hoteli ya Radison Blu, Kempton Park kuanzia leo tarehe 25 hadi 28 Julai 2025 chini ya mada: "Kulinda Mafanikio ya Ukombozi, Kuendeleza Maendeleo Jumuishi ya Kijamii na Kiuchumi, Kuimarisha Mshikamano wa Afrika."

Mkutano huu muhimu unathibitisha misingi ya kiitikadi ya vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika - ANC, MPLA, SWAPO, FRELIMO, ZANU-PF na CCM - na jukumu lao la kihistoria katika kupata uhuru, utu na maendeleo katika eneo lote la Kusini mwa Afrika.

Pia Kongamano linalenga kusisitiza umuhimu wa harakati hizi kuwa katika mpangilio unaotambua mabadiliko ya mazingira ya kisiasa na kimataifa yanayobadilika haraka.

Vyama vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika vilibadilisha hali ya kisiasa ya eneo hilo, kupinga utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, na kukaribisha utawala unaozingatia watu.

Tangu uhuru, vuguvugu hizi zimetekeleza sera muhimu kuhusu mageuzi ya ardhi, elimu, makazi, miundombinu na ulinzi wa kijamii.

Hata hivyo, mafanikio haya sasa yanakabiliwa kumegeka kutokana shinikizo jipya la mataifa ya kibeberu, migogoro ya kiuchumi, na majaribio ya kuingiliwa na ukoloni mamboleo.

Mkutano huu unatoa jukwaa moja la kukabiliana na matishio haya na kujumuisha majibu ya kimaendeleo ya kikanda yanayokitwa katika Pan-Africanism (Umajimuhi wa Kiafrika), internationalism na multilateralism.

Mkutano huo ni uingiliaji wa kimkakati katika uanzishaji upya wa mpango kazi (framework), kuimarisha mshikamano wa ndani ya chama, na kurekebisha harakati za ukombozi na matarajio ya kijamii na kiuchumi ya kizazi kipya......

SOMA ZAIDI :

 
Hivi, hiyo Amri ina apply kwenye mipaka ya Tanzania pekee au na hata nchi za watu kama kenya wakiamua kuwachapisha nako pia wamezuiliwa?
 
Kwa technologia ilipo watajulikana tu, labda wageuke mabubu. Tayari wameshatambua kutoa tu ushahidi wa uongo dhidi ya lisu unakuwa Adui wa taifa.
Tatizo ndugu zangu mnashindwa kutambua kua sheria inaruhusu ushahidi au shahidi asionekane. Ilo sio kinyume na sheria
 
Tatizo ndugu zangu mnashindwa kutambua kua sheria inaruhusu ushahidi au shahidi asionekane. Ilo sio kinyume na sheria
Najua lakini kwa kesi za mauaji ama za uhasama sasa uhaini tena wa kufanywa na mtu mmoja inakuwaje shahidi ajifiche kama ushahidi ni social media wanasemaje ni siri.
 
Saddest point ni kuwa hawa wote wanaoyafanya haya huwa hawana muda wa kusoma vitu kama hivi (hata robo yake). Wangekuwa wanafanya hivyo basi hii nchi ingelikuwa mbali sana kimaendeleo.
TL hapiganii wanae, mkewe, shemeji zake au washikaji wapate upenyo wa kula rasilimali za nchi, na kikubwa kabisa haongei zile lugha za 'kiprimitive' za kutetea wanyone dhidi ya 'matajiri' bali yeye anataka kuiona nchi ambamo jamii yake kila mtu anakuwa sawa mbele ya sheria ambazo tumezitunga wenyewe.
Eti huyu ndiye hatakiwi!
 
MTANYOOKA TU WAHUNI NYIE MANATAKA KUHARIBU TAIFA MUANGALIWE TU MTU ANAHAMASISHA UASI AANGALIWE TU? LISSU NI MUHAINI ANYONGWEEE
Siku namiliki šŸ”„ naanza na upinde kama nyie
 
Najua lakini kwa kesi za mauaji ama za uhasama sasa uhaini tena wa kufanywa na mtu mmoja inakuwaje shahidi ajifiche kama ushahidi ni social media wanasemaje ni siri.
Wanaosema ni Social media wao awapo ata mahakamani. Tujua kua Lissu si malaika inawezekana akateleza akakosea kwahiyo tusimuone kama malaika
 
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP),
Ushahidi unaotolewa mafichoni utaaminika vipi kwa upande wa utetezi na kwa umma wa Watanzania??

Pili, kama taarifa za ikulu huwa zinavuja itakuwa hizo za mahakama? Ndani ya mahakama hakukosekani wazalendo
 

Inasikitiisha sana hivi vyama kongwe dola vinafanya kila aina ya mbinu chafu kubaki madarakani.

Tutasikia ushahidi huo mzito, kiasi kile watachosema madhahidi hao wa Jamhuri sisi sote tutabaki mdomo wazi na ndiyo maana wameamua kuwaficha baada ya kuwatumia kuangamiza upinzani.
 

View: https://youtu.be/56XqzmlvhgQ?si=585Ih_Q5_OuCV7uk
Mahakama kuu chini ya Jaji Hussein Mtumbwe imekubali ombi la DPP kuwa mashahidi watakaotoa ushahidi dhidi ya kesi ya uhaini wa Tundu Lissu watoe ushahidi wakiwa:

1. Wamefichwa sura zao zao...

2. Wasijulikane utambulisho wao..

3. Wasijulikane wanatoka wapi, umri wao, wanapoishi nk

4. Chombo chochote cha habari kisichapishe habari zao isipokuwa kwa ruhusa ya mahakamašŸ¤”

#Hawa jamaa wanatumia kila aina ya legal manipulation ili kumwaga damu ya huyu mwamba kwa kumnyonga hadi afe...

#Je, Mungu Jehovah ataruhusu hili litokee...?

#Inajulikana kuwa Tundu Lissu hawezi kukubaliana na hili na kwa hiyo atakata rufaa. Watesi wake nao wanajua hili. Na bila shaka ndiyo furaha yao kwani lengo la kumweka gerezani kwa muda mrefu linatimia...

#Kwani haina shaka kuwa, mtindo wa kupiga kalenda kesi utaendelea mpaka muda wanaoutaka wao...

LAAKINI UKWELI BADO UMESIMAMA PALEPALE KUWA: Hakuna kesi ya uhaini hapo. Ni hila na uongo tu ulioingizwa mahakamani na kuchezea judiciary system yetu..!
 
Nikiwaambia kuwa miaka yangu ya mbeleni nataka nisomee ulozi kwa kiwango cha dunia mnashangaa. Ningekuwa fundi ningemshamalizana na hao waendeshaji wa kesi siku nyingi sana.
 
Kesi ambayo mshitakiwa akikutwa na hatia atanyongwa hadi kufa kwa nini mashahidi wawe wa GIZANI. Nini kitakata kufichwa?

Hapa kateni rufaa - ngoma hadi ifike rufani.
 
Muenendo wa kesi ni wa hovyo sana kuwahitokea tangu uhuru.
Uhaini mnaodai wa kutamka "tutakinukisha" upo kwa clips, sasa hao mashahidi wanatoka wapi kama sio wa kutengenezwa?
 
Wakati mwingine mashahidi wa siri wataweza kufanya watu waanze kutafuta mchawi na hivyo kulaumiana bila sababu.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…