Paul Makonda: Maskini Ukizulumiwa Haki Usikimbilie Mahakamani" Mahakama Wajitafakari

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Ziara za Makonda zimebainisha kwamba Mahakama sio chombo Cha kupata Haki Kwa maskini ambao hawana pesa sana sana itahalalisha dhuluma kwao.

Kiufupi Makonda anasema Mahakama inauza Haki Kwa wenye pesa na nakubalina nae Kwa sababu sijaona maskini hata mmja aliyefaulu kupata Haki yake mbele ya wenye pesa.
---
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema ukidhulumiwa haki yako si vyema kukimbilia mahakamani mara kwa mara baada ya kukosa haki zao, maana mara nyingi mawakili bora wanafanya kazi na watu wenye pesa hivyo ni ngumu kuipata.

Makonda amesema hayo leo Jumamosi Februari 10, 2024 alipokuwa akizungumza na wakazi wa Njombe mjini, ikiwa ni baada ya kuahirisha mkutano huo jana kutokana na mvua.

My Take
Mfumo wa Mahakama ujitafakari sana Kwa jinsi maskini wanavyodhulumiwa.

- Makonda: Mungu amenipa mlango dhidi ya aliyenidhulumu nyumba
 
Mwenezi Makonda amesema Serikali ya Dr Samia ni sikivu hivyo Wananchi wenye matatizo wazungumze na Chama na Serikali yatamalizwa

Mwenezi amesema hayo mkoani Njombe

Mlale Unono 😀
 
ila ukweli ni kua kama mnawweza kuyamaliza nyumbani bora iwe hivyo,
 
Mwenezi Makonda amesema Serikali ya Dr Samia ni sikivu hivyo Wananchi wenye matatizo wazungumze na Chama na Serikali yatamalizwa

Mwenezi amesema hayo mkoani Njombe

Mlale Unono 😀
Sasa mboni idadi ya Majengo ya Mahakama inaongezeka yale Majengo yanajengwa kwa ajili ya nani na kwa faida gani?

Kwako Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
 
watoeni na mashekhe miaka 10 ndani bila kuhukumiwa ni aibu mbowe katoka
 
Unakuta majaji wanavaa masuti mazito mazito na magari ya umma ya bei mbaya, lakini hakuna lolote. Niliidharau sana mahakama wakati wa kesi ya Mbowe na ushahidi uliokuwa unatolewa ulikuwa ni ushahidi wa kutengeneza kabisa, na Bado eti mahakama ikamkuta na kesi ya kujibu! Pale ndio nilijua mahakama ni uozo kwa kiwango gani.
 
Ziara za Makonda zimebainisha kwamba Mahakama sio chombo Cha kupata Haki Kwa maskini ambao hawana pesa sana sana itahalalisha dhuluma kwao.

Kiufupi Makonda anasema Mahakama inauza Haki Kwa wenye pesa na nakubalina nae Kwa sababu sijaona maskini hata mmja aliyefaulu kupata Haki yake mbele ya wenye pesa.
---
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema ukidhulumiwa haki yako si vyema kukimbilia mahakamani mara kwa mara baada ya kukosa haki zao, maana mara nyingi mawakili bora wanafanya kazi na watu wenye pesa hivyo ni ngumu kuipata.

Makonda amesema hayo leo Jumamosi Februari 10, 2024 alipokuwa akizungumza na wakazi wa Njombe mjini, ikiwa ni baada ya kuahirisha mkutano huo jana kutokana na mvua.

My Take
Mfumo wa Mahakama ujitafakari sana Kwa jinsi maskini wanavyodhulumiwa.

- Makonda: Mungu amenipa mlango dhidi ya aliyenidhulumu nyumba

Yule mama aliyekamatwa ma nyama ya swala kilo 5 akapigwa mvua za kutosha na mahakama ya kanda ya iringa. Lakini yule mchina aliyekamatwa na meno ya tembo, na nyara nyingine za serikali aliamuriwa kulipa laki 2 tu na mahakama.

Makonda kakosea wapi?
 
Mahakama hizi za Maelekezo kutoka juu, kama alivyowahi kujisemea Rostom Azizi, unategemea upate haki?
 
Back
Top Bottom